Majambazi Tabata Matumbi


Kizimbuzi

Kizimbuzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2013
Messages
1,407
Likes
227
Points
160
Kizimbuzi

Kizimbuzi

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2013
1,407 227 160
Watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa kwa kupigwa na kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kudaiwa kuvamia duka la bidhaa mbalimbali eneo la Tabata Matumbi jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuiba.

Inadaiwa kwamba baada ya kumjeruhi muuza duka na kushindwa kutumia bastola waliyokuwa nayo majambazi hao wamejikuta wakikamatwa na kuadhibiwa na wananchi hao.

ITV ikiwa katika eneo la tukio imeshuhudia majambazi hao wakipigwa na kuchomwa moto kabla ya polisi kufika na kuchukua miili ya majambazi hao na kuipekela katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ikiwa imekwishaungua vibaya.


Source: ITV, facebook Page
 

Forum statistics

Threads 1,251,143
Members 481,585
Posts 29,759,056