Majaliwa: Watanzania iombeeni serikali. Asema kazi ya kutumbua majipu ina mtihani mkubwa

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
12651306_1036941359703655_1837652123866561594_n.jpg
 
hiii kauli ya Majaliwa ni ya kushindwa kazi,uwezi ukasema asiyeweza kazi aache mwenyewe hii ni kuonesha kwamba hana uwezo wa kuchukua hatua,hasa ukizingatia kwamba wala rushwa wakubwa ni viongozi wa serikali hii na viongozi wa ccm ndio maana mpaka sasa hawajaguswa na akijitokeza mtu kuwanyooshea kidole wanakushambulia serikali nzima kama walivyofanya bungeni kwa kumtoa mbunge aliyejaribu kuzungumzia wizi wa Escrow
 
Ukiona wameanza kudai maombi kwa bidii ujue Tayari yameshawashinda kwahiyo wanajificha kudai kuombewa ili badae mkiona kimya nakuwauliza watawaambia.....tuliwadai maombi Hamkutuombea ....hii ndio Danganyika
 
Inawezekana kweli wanatumbua majipu? Maana ni jambo la aibu watuhumiwa wa ESCROW ndio viongozi wa bunge, waliokuwa wasimamizi wa bandari na reli leo ni waziri,
Hizi story za kukomesha ufisadi ndani ya serikali ya Ccm ni ngumu sana maana hawana moyo wa dhati.
 
Inawezekana kweli wanatumbua majipu? Maana ni jambo la aibu watuhumiwa wa ESCROW ndio viongozi wa bunge, waliokuwa wasimamizi wa bandari na reli leo ni waziri,
Hizi story za kukomesha ufisadi ndani ya serikali ya Ccm ni ngumu sana maana hawana moyo wa dhati.
sio ccm tu hata ndani ya cdm ni shidaaaa....sikujua kama watampa lowasa nafasi kiasi kile wakati alikuwa ktk list of shame
 
Kwani wamefanya nini zaidi ya kuwafukuza watu kazi. Uombewe kwa kumfukuza mkurugenzi wa NIDA kazi? Mkitaka muombewe rudishisheni hela ya escrow. Waiziri mkuu kanikumbusha mzee Pinda sijui kapotelea wapi.
 
Chini ya siku 100 tayari waomba waombewe Mungu!!! Kuna miezi karibia 57 mbele yao safari ni ndefu. Inabidi wao waombe sana Mungu na kumuomba msamaha Mungu kwa wingi sana sababu hata kama mtu ana madudu yake kwa ubinadamu unatakiwa umsitiri aibu zake na Mungu atakustiri ya kwako na kukupa nguvu. Kuna mengine viongozi huwa wanafanya sio sawa bora ubandue na ubandike lakini sio kufedhehesha watu. Nakubali ni kazi nzuri wanayofanya ila kwa njia ya makosa. Mungu ni huyo huyo wote tunaomba kwake msaada.
 
Suala la kushughulika na majipu inahitaji ushirikiano baina ya viongozi wa serikali (rais, waziri mkuu, mawaziri) na taasisi muhimu kama takukuru, polisi na mahakama bila kusahau wanasiasa wa vyama vyote.
Lakini JPM na Majaliwa mmeonyesha ubabe kwa mambo yasiyohusu majipu mfano BUNGE LIVE, na mahubiri yenu daima kejeri, kibri na mnaonyesha dhairi lengo lenu kukandamiza demokrasia na haki za binadamu kwa kivuri cha kutumbua majipu.
Kiongozi wa nchi anapaswa kuwa mkali kwa MAJIPU sio kwa WAKOSOAJI, daima anayekukimbiza ndio anayekusaidia kuwa makini.
 
Kikulacho ki nguoni mwako sasa sijui wanataka waombewe nini ?? Kuweni specific ni maombi ya nini mnataka mfanyiwe na Watanzania, Halafu ni Watanzania wapi hao kwenye maombi Watanzania ni kitu kimoja ila linapokuja swala la Zanzibar ,Raisi hana mamlaka na kinachoendelea Zanzibar ,ungesema Watanganyika wakuombee ungeeleweka
 
Ukiona wameanza kudai maombi kwa bidii ujue Tayari yameshawashinda kwahiyo wanajificha kudai kuombewa ili badae mkiona kimya nakuwauliza watawaambia.....tuliwadai maombi Hamkutuombea ....hii ndio Danganyika
Nadhani wanayafikia yale makubwa.
 
Hata kama ningekua mchungaji nisingewaombea hata kwa mchuzi hada watende haki iliyo mbele yao, na,maanisha haki ya Zanzibar, wazanzibari wanataka haki na haki imeshikiliwa huku Bara na wanaojua ama kuhisi kitakachotokea kule.

Kwa nini wasifikirie kwa makini kama kweli wanahitaji hayo maombi au wanatuhadaa tu watanzania na haya maigizo yao??

Viongozi wakubwa wa Zanzibar wa ccm wanac teuliwa Chamwino alafu ndo wakapigiwe kura kile Zenji, kwanza viongozi huku wajiridhishe nao kwanza, sasa kama ndo hivi kwa nini wasimwambie ti Seni aachane na huo udikteta wake ambao hauendani na Hesha ambayo ameshajitengenezea kwa Wazanzibari?????????
Eti wanataka maombi yetu, thubutuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom