Majaliwa: Tanzania itajitegemea kwa 80% katika bajeti

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa alisema Tanzania inaweza kujitegemea kwa zaidi ya asilimia 80 katika bajeti yake kutokana na vyanzo vyake vya ndani. Amesema kutokana na rasilimali zilizopo, Tanzania inaweza kukidhi bajeti yake kwa asilimia 80 bila kutegemea msaada kutoka nje na kwamba suala la kukabiliana na ufisadi na ukwepaji kodi ni endelevu.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema hayo juzi mjini Lamadi wakati akihutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku sita mkoani Simiyu. “Tanzania inaweza kujitegemea kwa asilimia 80 kwa mapato yake kutokana na rasilimali na vyanzo vyake vya ndani.

Hili linawezekana. Ndio maana tumeamua kubanana,” alieleza Waziri Mkuu. Alisema ndio maana wameamua kupambana na ufisadi na ukwepaji kodi kwa nia ya kuhakikisha wanapata fedha za kuwatumikia Watanzania kwa fedha za ndani kupitia mapato yake.

Alisema hata uamuzi wa kupitisha fedha zote katika Mfuko Mkuu wa Serikali ulikuwa na nia ya kutambua mapato yake yote ili fedha hizo zikasaidie kuleta maendeleo ikiwamo kuisimamia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kubana mianya yote ya ukwepaji kodi.

Alisema hali hiyo imesaidia kwani mapato yameongezeka kutoka Sh bilioni 1.3 Desemba mwaka jana, Sh bilioni 1.5 Januari mwaka huu na mwezi uliopita, alisema ana hakika zitavuka zaidi.

Alisema kutokana na hali hiyo, serikali ndio maana inagharimia mambo yake mengi likiwamo suala la elimu bure, na kwamba licha ya kuwapo kwa changamoto mbalimbali, watahakikisha Watanzania wanapata huduma mbalimbali zilizoboreshwa.

Aliyekuwa Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum akiwasilisha bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2015/16, Juni mwaka jana, alisema jitihada za kuongeza mapato zimelenga kuisaidia Serikali kupunguza utegemezi wa bajeti ya Serikali kwa fedha za wahisani.

Alisema kiwango cha utegemezi kimepungua kutoka asilimia 24 mwaka 2004/05 hadi asilimia 17 mwaka 2010/11. Alisema pia kwamba utegemezi huo umekuwa ukipungua mwaka hadi mwaka. Mwaka 2015/16 ilitarajiwa upungue kwa asilimia 6.4.

Kuhusu suala la mipaka kati ya hifadhi na vijiji, Waziri Mkuu alisema amekwishaagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kusimamia suala hilo na kuhakikisha wanaliangalia limalizike kwa busara.

Lakini ameagiza wananchi hasa katika wilaya za Busega na Bariadi kutoingia tena katika hifadhi ambako inadaiwa wanapokonywa ng’ombe wao na askari wa Wanyamapori kwa kutozwa Sh milioni tano hadi 10.

Amewaonya askari hao wa Wanyamapori kuacha tabia hiyo na kwamba mwananchi yeyote mwenye taarifa za askari anayeshiriki vitendo hivyo, kupeleka jina lake kwa vyombo husika.
 
Suala la elimu bure hilo haliwezekani. Serikali haina uwezo wa kufanya hivyo,na sio kifedha naongelea hapa bali miundo mbinu na mipango madhubuti ya kutoa elimu bure.

Ningemwelewa magufuli kama angekuja na afya bure kwa watoto na wazee.
Hapa angeweza kubypass time ba kueelewa ni elimu gani na kwa wakati upi,na cost yake katika kuwapatia bure kwa wananchi.
Pia,vipaumbele vingekuwa katika kujenge sera na mifumo mipya katika usimamizi na utekelezaji.
Mambo kama umeme,maji,makazi na internet yanatakiwa yawe muhimu sana. Then next term ndio angeanza na mambo mengine makubwa.
 
Bajeti ya mwaka huu ilikuwa 22tri
Makusanyo ya TRA kwa Mwezi ni 1tri
Kwa mwaka ni 12tri
Je hiyo tofauti ya 10tri ndio 16% ambayo tutaomba msaada?
Nisaidieni tu
Makusanyo yetu ni 12tri kwa mwaka (makadirio)
 
KWANI MAPATO YA SERIKALI NI KODI TU YA TRA MKUU??????????????????
 
Huyu anamdanganya nani? Mbona watu tunajua mahesabu vizuri...km Nchi inaweza kukusanya 1.2Trilion in average we do expect to raise 14 Trilion anually And bajet yetu ina total around 22 Trilion sasa apa kuna defeciet ya around 8-10 Trilion ambapo ni pungufu kwa 35-40%...Sasa PM anaposema tutafikia 80% anamdanganya nani? otherwise bajeti iwe ni 15-16Trilion kwa mwaka apo ndo 80%....
 
MAPATO YA SERIKALI NI FEDHA ZINZIKUSANYWA NA TRA PEKEEEEEEEEEEEEEE???????????????
NYUMBU
 
Suala la elimu bure hilo haliwezekani. Serikali haina uwezo wa kufanya hivyo,na sio kifedha naongelea hapa bali miundo mbinu na mipango madhubuti ya kutoa elimu bure.

Ningemwelewa magufuli kama angekuja na afya bure kwa watoto na wazee.
Hapa angeweza kubypass time ba kueelewa ni elimu gani na kwa wakati upi,na cost yake katika kuwapatia bure kwa wananchi.
Pia,vipaumbele vingekuwa katika kujenge sera na mifumo mipya katika usimamizi na utekelezaji.
Mambo kama umeme,maji,makazi na internet yanatakiwa yawe muhimu sana. Then next term ndio angeanza na mambo mengine makubwa.
Usiseme elimu bure haiwezekani. Uwe na imani itawezekana. Angalau utaratibu umeshaanza. Pale penye mapungufu wananchi watachangia huku serikali ikijizatiti na amini siku moja elimu yote itakua bure.
 
M
MAPATO YA SERIKALI NI FEDHA ZINZIKUSANYWA NA TRA PEKEEEEEEEEEEEEEE???????????????
NYUMBU

Mi nahisi we ndio unastahili kuitwa nguruwe kabisa,, kwaiyo kuna mapato mengine tofauti na yanayotangazwa na mamlaka ya mapato tanzania????ebu yataje kwa faida yetu sisi we kitimoto
 
MFANO MDOGO:FEDHA ZA KIGENI ZINAZOTOKANA NA KUUZA VITU NJE YA NCHI AU UTALII YANAKUSANYWA NA TRA WE NYUMBUUUUUUUUUUUUUUUU.?????????????
 
Hujui unachobisha halafu unatukana wenzio una hatari sana
 
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa alisema Tanzania inaweza kujitegemea kwa zaidi ya asilimia 80 katika bajeti yake kutokana na vyanzo vyake vya ndani. Amesema kutokana na rasilimali zilizopo, Tanzania inaweza kukidhi bajeti yake kwa asilimia 80 bila kutegemea msaada kutoka nje na kwamba suala la kukabiliana na ufisadi na ukwepaji kodi ni endelevu.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema hayo juzi mjini Lamadi wakati akihutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku sita mkoani Simiyu. “Tanzania inaweza kujitegemea kwa asilimia 80 kwa mapato yake kutokana na rasilimali na vyanzo vyake vya ndani.

Hili linawezekana. Ndio maana tumeamua kubanana,” alieleza Waziri Mkuu. Alisema ndio maana wameamua kupambana na ufisadi na ukwepaji kodi kwa nia ya kuhakikisha wanapata fedha za kuwatumikia Watanzania kwa fedha za ndani kupitia mapato yake.

Alisema hata uamuzi wa kupitisha fedha zote katika Mfuko Mkuu wa Serikali ulikuwa na nia ya kutambua mapato yake yote ili fedha hizo zikasaidie kuleta maendeleo ikiwamo kuisimamia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kubana mianya yote ya ukwepaji kodi.

Alisema hali hiyo imesaidia kwani mapato yameongezeka kutoka Sh bilioni 1.3 Desemba mwaka jana, Sh bilioni 1.5 Januari mwaka huu na mwezi uliopita, alisema ana hakika zitavuka zaidi.

Alisema kutokana na hali hiyo, serikali ndio maana inagharimia mambo yake mengi likiwamo suala la elimu bure, na kwamba licha ya kuwapo kwa changamoto mbalimbali, watahakikisha Watanzania wanapata huduma mbalimbali zilizoboreshwa.

Aliyekuwa Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum akiwasilisha bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2015/16, Juni mwaka jana, alisema jitihada za kuongeza mapato zimelenga kuisaidia Serikali kupunguza utegemezi wa bajeti ya Serikali kwa fedha za wahisani.

Alisema kiwango cha utegemezi kimepungua kutoka asilimia 24 mwaka 2004/05 hadi asilimia 17 mwaka 2010/11. Alisema pia kwamba utegemezi huo umekuwa ukipungua mwaka hadi mwaka. Mwaka 2015/16 ilitarajiwa upungue kwa asilimia 6.4.

Kuhusu suala la mipaka kati ya hifadhi na vijiji, Waziri Mkuu alisema amekwishaagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kusimamia suala hilo na kuhakikisha wanaliangalia limalizike kwa busara.

Lakini ameagiza wananchi hasa katika wilaya za Busega na Bariadi kutoingia tena katika hifadhi ambako inadaiwa wanapokonywa ng’ombe wao na askari wa Wanyamapori kwa kutozwa Sh milioni tano hadi 10.

Amewaonya askari hao wa Wanyamapori kuacha tabia hiyo na kwamba mwananchi yeyote mwenye taarifa za askari anayeshiriki vitendo hivyo, kupeleka jina lake kwa vyombo husika.
maneno yake ni sawa maana fedha za waisani huwa hazifanyi kazi yoyote huwa zinaiishia kwenye mifuko ya wakubwa
 
Hapa ndipo nnapomsifu Kikwete, bajeti yake ya mwisho tumejitegemea 90%.

Kwanini tusiendeleze au kuboresha?
 
It easy said than done!
Tatizo sio
%age ya kujitegemea lakini ni kupatikana fedha kwenye Wizara kama zinavyopitishwa
 
Lazima tutambue vyanzo vya mapato sio kodi tu inayayokusanywa na TRA, kuna utalii, uvuvi, madini, misitu, tozo mbalimbali, penalties etc... Ukweli ni kwamba nchi inaweza kujitegemea kwa asilimia . Tuna source nyingi za mapato
 
Back
Top Bottom