Majaliwa: Sitaki kusikia mwekezaji anacheleweshwa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa serikali kutekeleza majukumu yao kwa wakati, waondoe urasimu kwani hataki kusikia mtu yeyote anayetaka kuwekeza nchini anakwamisha kutokana na utendaji wao.

Majaliwa ameongeza kuwa, serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuanzisha wizara maalum ya uwekezaji, kupambana na rushwa, kuimarisha upatikanaji wa ardhi, ujenzi na ukarabati wa miundombinu na kufuta tozo 173, ili kuhakikisha wawekezaji wanafanya kazi kwa ufanisi.

“Nia ya serikali ya awamu ya tano ni kuvutia wawekezaji, na wewe [mtumishi] ndiye facilitator [muwezeshaji],” amesema Majaliwa.

Akizundua Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Iringa amesema ni wazi kuwa uwekezaji wa aina yoyote unachochea upatikanaji wa ajira na kukuza matumizi ya teknolojia, hivyo watumishi wenye dhamana wasiwe vikwazo.

Amebainisha kuwa viashiria mbalimbali vinaonesha matunda ya jitihada za serikali ikiwa ni pamoja kukua kwa uchumi na kupungua kwa mfumuko wa bei ambao umefikia tarakimu moja.

Kiashiria kingine ni kuongezeka kwa mapato yanayokusanywa na serikali na kudhibiti matumizi yake kwa kuondoa shughuli zisizo na maslahi kwa umma.

Amefafanua kuwa Iringa ni sehemu bora zaidi ya kuwekeza kutokana na kuwa ardhi nzuri, uwepo wa maji ya kutosha, hali ya hewa ya kuvutia, uwepo wa nguvu kazi ya kutosha, barabara za lami.

“Mimi mwenyewe kuna siku nilipita kule Isimani, nikaona eneo nikalitamani, [Waziri] Lukuvi akaniambia hilo tayari,” amesema Majaliwa akieleza nia yake ya kuwekeza Iringa, mkoa alioubainisha kuwa ni eneo la kupumulia Makao Makuu ya Nchi, Dodoma.
 
Wawekezaji gani hao?Wale wanaofilisiwa kila siku kupitia ile sheria dhalimu ya uhujumu uchumi?Kuna mwekezaji ambae anaweza kuthubutu kuwekeza katika nchi ambayo muda na dakika yoyote ile unafilisiwa?
 
Mimi huwa nikiingia sehemu yoyote ya biashara halafu nikiona ukuta ulivyochafuka na vibali huwa nakata tamaaa kwa kweli najiona nitawezaje kufanya haya yote. Mwaka unaisha unajikuta busy kukimbilia vibali badala ya kufanya biashara.

Hivi kweli tumeshindwa vipi kuja na kibali kimoja basi, kama walivyofanya kwenye road licence kutia katika mafuta japo unaweza kujikuta unalipa zaidi lakini sababu unatia katika mafuta uhisi kitu unaona kuna nafuu. Jamani mje na kibali kimoja tu kuta zimejaa makaratasi ndio uchochoro wa rushwa huu.
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa serikali kutekeleza majukumu yao kwa wakati, waondoe urasimu kwani hataki kusikia mtu yeyote anayetaka kuwekeza nchini anakwamisha kutokana na utendaji wao...
Hivi kuna mwekezaji mwenye akili zake atakuja kuwekeza?

Bora aende Yemen
 
Huu nao ni uongo, mbona yule wa Oman hela zake mmezizuia BOT toka mwaka 2018, alitaka kufungua kiwanda cha Dawa Arusha, hadi sasa anataka kwenda kuwekeza Kenya?

Tutakua consumers all our time.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom