Majaliwa aondolewe Jeshi la Zimamoto na arudishe zawadi zote alizopewa

Yaani hii report badala ya kueleza chanzo cha ajali kinaeleza aliyefungua mlango 😅😅😅
Hapo kulikua na utata mkuu, watu walikua wanahoji huo mkanganyiko, dogo anapewa ushujaa usimuhusu huku mashujaa halisi wamewekwa pembeni, inakuingia akilini wewe? Hivi kama sio wahudumu kufungua mlango Majaliwa angepewa huo ushujaa wa mchongo? Umewahi kujiuliza hilo swali au unajiuliza kuhusu black box tu?
 
Ifahamike kwamba hatuna shida yoyote na huyu Kijana , maana sasa ni dhahiri kwamba ALITUMIKA ILI KUWEZESHA MIPANGO YA WATU WENGINE .

Lakini baada ya Jamii kustukia mchezo duni uliochezwa bado mnataka tunyamaze ? na ni kwanini tunyamaze ?

Ikiwa kama Waziri husika anasema baada ya uchunguzi kwamba dogo huyo hakufungua mlango wala nini , mnadhani sisi raia tuliokuwa nchi kavu tunawezaje kubisha ? Je waliotudanganya akiwemo Majaliwa na Chalamila walitaka kuficha jambo gani na kwanini ?

Sasa nasema Kama Mmbwai na iwe Mmbwai tu , huyu dogo arudishwe kuanika dagaa na arejeshe hela za watu waliomchangia kama Shukrani kwa ambayo HAKUYAFANYA , walooshirikiana naye kutudanganya watimuliwe haraka sana .

Hatuwezi kuishi kwa uongo miaka yote .
Je!
Nongwa yako ni jina la Majaliwa au kingine zaidi?

Je!
Akirudishwa kuanika dagaa,Marehemu nao watarudishiwa Uhai wao?

Je!
Huyo waziri unaemuamini wewe!
Yeye alikuwepo ndani ya ndege?

Je!
Ni Uongo kwamba Majaliwa hakupiga Kasia na kuwa mtu wa awali kuifikia ile ndege?

Je!
Ni Uongo kwamba Majaliwa hakuzimia na kudondokea Majini,kwa kupigwa na Kamba iliyokatika wakati wa jitihada zaidi za kufungua mlango mwingine wa Ndege?

Je!
Hao wanaojitokeza leo na kudai walisaidiana wao kuufungua mlango wa ndege!
Walikuwa wapi kuyasema hayo,mpaka pale walipoona Majaliwa alipojaaliwa Mapesa?

Je!
Wewe Erythrocyte ulikuwepo eneo la ajali au Umbeya wako wa Ki-Chadema ndio unaokuwasha?

Fanyeni Mambo ya msingi kuendeleza Chama chenu!

Acheni kudhani Chama kinaishi kwa Visasi na Majungu misibani!

Chadema mnakwama wapiiiii???

Majaliwa kishapata kazi.
Halafu wewe mpuuzi fulani unamuombea akose au anyang'anywe hiyo ajira ili upate nini?

Mnaheshimiwa ila hamuheshimiki,wala kuheshimu na kuwastahi wenzenu!

Eti mbwai iwe Mbwai.....

Kwa lipi sasa?
Au una Konyagi kichwani?

Huu ni Unyumbulistic

20220820_120415.jpg
 
Hapo kulikua na utata mkuu, watu walikua wanahoji huo mkanganyiko, dogo anapewa ushujaa usimuhusu huku mashujaa halisi wamewekwa pembeni, inakuingia akilini wewe? Hivi kama sio wahudumu kufungua mlango Majaliwa angepewa huo ushujaa wa mchongo? Umewahi kujiuliza hilo swali au unajiuliza kuhusu black box tu?
Mimi toka mwanzo sikuafiki kasia kufungua mlango na huyo Majaliwa kuwa shujaa ilihali mwenyewe alizinduka akiwa hospitali, ila sidhani kama kuna umuhimu au ulazima wa kugombania aliyefungua mlango wa ndege. Hii report ilipasa kueleza chanzo cha ajali na uzembe wa mamlaka husika katika hiyo ajali otherwise labda kama wanataka kututoa kwenye mjadala wa kadhia ya umeme na maji ili tuendelee kujadil script waliyompa Majaliwa.
 
Hii report ilipasa kueleza chanzo cha ajali na uzembe wa mamlaka husika katika hiyo ajali otherwise labda kama wanataka kututoa kwenye mjadala wa kadhia ya umeme na maji ili tuendelee kujadil script waliyompa Majaliwa.
Hayo ya chanzo atakuja kuyatolea maelezo waziri mwenye dhamana baada ya uchunguzi wa black box kukamilika, kwani yaweza ikawa uchunguzi wa black box bado haujakamilia au umeshakamilika ila yeye hakuita press conference ili kuzungumzia hilo au labda report ya chanzo ni nini bado haijakamilika ila report ya nani alifungua mlango imekamilika, ni hivyo mkuu
 
Back
Top Bottom