Majaji wa Bongo Star Search

Majaji wa Bongo Star Search

Daktari wa Meno

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2019
Posts
509
Reaction score
1,617
Hellow Tanzania, Hellow JF.

Naomba kutoa dukuduku langu kuhusu hawa wanaojiita/kuitwa majaji wa BSS. Mimi siyo mtazamaji sana wa mashindano hili ila mara kadhaa huwa naona video clip za washiriki mbalimbali kwenye Instagram Page ya BSS.

Sipendi namna ambavyo hawa majaji wanavyojishaua mbele ya washiriki pale ambapo mtu kafanya kitu ambacho hakijawabariki. Mfano: mshiriki akiboronga utaona namna wanavyomsakama kwa kejeli mbalimbali ambazo hazina maana yoyote, naona ni vyema kusema umejitahidi au sijapenda ulichofanya kuliko kuanza kujishaua mkijiona mnajua sana muziki kuliko wengine.

Kumbukeni nyodo ambazo mlizionesha kwa Harmonize wakati akishiriki shindano hilo miaka kadhaa iliyopita, kwenu alionekana hawezi ila kijana aliamini katika yeye mwenyewe. Acheni kujifanya nyie ni wakosoaji wazuri wa wenzenu kitu ambacho siyo. Madame Rita sidhani kama ana uwezo hata wa kuandika muziki achilia mbali kuimba ila akianza kujichekesha na kukejeli washiriki utasema ni latest version ya Beyonce kumbe hakuna chochote ajuacho.

Master Jay hivyohivyo naye kaambukizwa ushambenga wa wanawake na kuanza kuwa kama wao.

Tujifunze kupitia wenzetu ambao wako mbali na sisi kwenye muziki, je wanafanya kama sisi au ni style yenu wenyewe? Kama ni style yenu kwangu mimi naona mnawapa washiriki hofu, wanaenda jukwaani wakijua wakikosea watachekwa na kukejeliwa.

Mtanzania ukimpa tu kinafasi cha kukosoa mwenzake atajifanya ni mtu kutoka mbingu/sayari nyingine kwa namna ambavyo anajiona anajua.
 
Kuna kaukweli kiasi naona washiriki wanakua na kahofu coz wanajua wakizingua tu watapewa maneno(kejeli), ila kuna washiriki wengine hawako serious kabisa ,kuna mmoja aliimba wimbo wa kanyaga dah, nilicheka sanaa, hajui hata anaruka ruka tu, huyo hata Mimi ningempa manenoo
 
Ni sahihi kabisa.Ndugu mtoa mada nakuunga 100%.ni kama ulikuwa kwenye mawazo yangu na ni siku mbili nimetoka kulitafakari hili.

1-Mtu apewe nafasi ya kuonesha jambo,awe nacho kipaji au asiwe nacho nae anastahili kupewa moyo kwa kile anachokiamini.Kwao inaweza kuwa mchezo wa kujibu bila kujari hisia za washiriki ila kwa mshirika amefika pale kama njia moja wapo ya kutafuta mafanikio.Tusizisemee vibaya. juhudi za watu kwa kuwakatisha tamaa.

2-Kwa majaji kinaweza kuwa si kiwangi bora au pengine ni kiwango kidogo mshiriki anachoonesha but,atleast amejaribu kufanya.Kama BSS ni kutafuta vipaji,kwanin hawawi chachu ya watu vipaji kukuwa?wanaangalia kuweza ikiwa hawajui mazingira waliokulia watu licha ya kuwa wanavipaji.Waliwahi kukiri kuwa harmonize huyu sio yule,hapo ni baada ya kumkejeri,je kama ANGEYABEBA YALE ANGEKUWA WAPI?ni wangap wameshindwa kufikia ndoto zao kwa kuaminishwa na majaji hawawezi ikiwa wanaweza?

Rai yangu.
Ni vizuei kwa washiriki kutiwa moyo ili waweze kujipanga zaidi na zaidi.wengi tumefanya vizuri shuleni kwa kauli tu ya mwl "unajitahidi sana,usiniangushe mitihani hii".Neo huimarisha ndoto ya mtu na neno huua ndoto ya mtu.haina haja ya kuwajibu vibaya kisa kuwafurahisha watazamaji,mnacheza na hatma za watu wanaoamini katika ndoto zao.Ni nyinyi wenyewe mnasema ukiamini unaweza,kwann hamuwaongezei watu imani au hamtaki waweze?.Acheni ubinafsi kwa kucheza na hatma za watu kwa mlengo wa kunogesha.
 
BSS haina mvuto tena majaji wenyewe wazee wa miaka na miaka kwanini wasipishe majaji wapya? Sijawahi wazaga kuangalia upumbavu wa bss
Aisee huo muda wa kuangalia s Bora nipige usingiz
 
Wakisoma Thread Watakuelewa Lakini Hata Wasiposoma Wataambiwa Kuwa Wajirekebishe Haraka Sana Kabla Hazijaja Siku Mbaya Kwao
 
Back
Top Bottom