Maiti yazuiliwa hospitali ya Muhimbili ikidaiwa fedha

Pistol

Senior Member
Oct 13, 2015
194
86
Hospitali ya Taifa Muhimbili imegoma kuruhusu mwili wa marehemu Bi Hilda Lukas miaka 30 aliyefariki dunia June 26 katika hospitali hiyo, akisumbuliwa na ugonjwa wa utumbo kutoboka huku ikidai lazima fedha yote wanayomdai marehemu ilipwe ambayo ni sawa na shilingi milioni moja na laki moja na nusu kwa mujibu wa ndugu wa familia kama gharama za kumuhudumia mgonjwa huyo.

Mama wa marehemu Bi Anna Zuaro na Bibi wa marehemu wameiomba serikali na wadau mbalimbali kuona namna wanavyoweza kuwasaidia kwani wao mpaka sasa hawana fedha za kuuondoa mwili wa mpendwa wao, huku gharama za kuuhifadhi mwili huo katika chumba cha kuhifadhi maiti zikizidi kuongezeka.

Kwa maafisaa wa Muhimbili wanakiri marehemu Hilda Lukas alikuwa amelazwa katika wodi ya kibasira chumba namba 9 ingawa haikuwa rahisi kuzungumza na maafisa hao.

Uongozi wa mtaa wa Chang’ombe umesema umefanya juhudi nyingi tu zikiwemo za kuchangisha wananchi na wadau mablimbali lakini mpaka sasa bado hawajaweza kukamilisha kiasi hicho cha fedha kinachohitajika Muhimbili ambapo gharama za mochwari pekee mpka sasa ni shilingi 210,000.

Chanzo: ITV
 
Mungu awatie nguvu wafiwa maana kila kukicha maombolezo bado yapo.

Ni vyema kusaidiana pia ktk mambo haya.
 
hamna utaratibu wa msamaha kwa wasio na uwezo!

kuzuia maiti sio maadili mema... japo siku hizi watu wanawadai hadi marehemu.
 
Hivi mbona hospital ya serikali inakuwa kama binafsi vile kuna vitu vingine ubinadamu utumike wao wanawaza fedha tu. Mmemtibu amekufa Bora mngekatalia mgonjwa kuliko mahiti
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili imegoma kuruhusu mwili wa marehemu Bi Hilda Lukas miaka 30 aliyefariki dunia June 26 katika hospitali hiyo, akisumbuliwa na ugonjwa wa utumbo kutoboka huku ikidai lazima fedha yote wanayomdai marehemu ilipwe ambayo ni sawa na shilingi milioni moja na laki moja na nusu kwa mujibu wa ndugu wa familia kama gharama za kumuhudumia mgonjwa huyo.

Mama wa marehemu Bi Anna Zuaro na Bibi wa marehemu wameiomba serikali na wadau mbalimbali kuona namna wanavyoweza kuwasaidia kwani wao mpaka sasa hawana fedha za kuuondoa mwili wa mpendwa wao, huku gharama za kuuhifadhi mwili huo katika chumba cha kuhifadhi maiti zikizidi kuongezeka.

Kwa maafisaa wa Muhimbili wanakiri marehemu Hilda Lukas alikuwa amelazwa katika wodi ya kibasira chumba namba 9 ingawa haikuwa rahisi kuzungumza na maafisa hao.

Uongozi wa mtaa wa Chang’ombe umesema umefanya juhudi nyingi tu zikiwemo za kuchangisha wananchi na wadau mablimbali lakini mpaka sasa bado hawajaweza kukamilisha kiasi hicho cha fedha kinachohitajika Muhimbili ambapo gharama za mochwari pekee mpka sasa ni shilingi 210,000.

Chanzo: ITV
Tuwekee namba hapa ya muhusika jamani. Hivi Uchungu wa kufiwa hautakiwi uendane na kero yoyote!
 
Juzi tu hapa kuna mzee alikuwa anaomba msaada akakomboe maiti ya mwanae inayoshikiliwa na hospital huko India.

Hii issue iko dunia nzima.
 
Duh eti wanashikilia maiti. Huo ni uchuro kwa mila zetu za kiafrika hata kisheria. Maiti hata mahakamani kwenyewe haihukumiwi sembuse hospitalini, tena ya umma ???!! Mwacheni marehemu aende zake akazikwe na kupumzika kwa amani tafadhali.
 
Huu ni unyama na upumbavu. Unaposhikilia maiti hospitali inazidi kugharamika madawa ya kuhifadhia mwili. Hata kama kuna madai juu ya mwili kwa nini asiitwe mwanasheria akawaandikisha deni wafiwa ili wakazike kisha malipo yatafanyika pesa ikipatikana?

Hii nchi ina bahati mbaya kila taasisi. Kufiwa kunauma sana.
 
Usiombe hili jambo likukute,kama ingekuwa wote tunabusara. ..hili lilitakiwa kumalizwa mapema tu.
 
Hivi mbona hospital ya serikali inakuwa kama binafsi vile kuna vitu vingine ubinadamu utumike wao wanawaza fedha tu. Mmemtibu amekufa Bora mngekatalia mgonjwa kuliko mahiti
Lipa pesa longolongo baadae..
*mahiti = maiti
 
Huu ni unyama na upumbavu. Unaposhikilia maiti hospitali inazidi kugharamika madawa ya kuhifadhia mwili. Hata kama kuna madai juu ya mwili kwa nini asiitwe mwanasheria akawaandikisha deni wafiwa ili wakazike kisha malipo yatafanyika pesa ikipatikana?

Hii nchi ina bahati mbaya kila taasisi. Kufiwa kunauma sana.
Yap thats the point..angeitwa Mwanasheria wa hospitali wakaandikishana watu wakazike.
 
Back
Top Bottom