Maiti yatakiwa ijaze form | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maiti yatakiwa ijaze form

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Inkoskaz, Feb 24, 2012.

 1. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  MJANE Specioza Kamala ameendelea kusotea mafao ya mume wake aliyefariki miaka 13 iliyopita, huku mwaka huu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ikimwandikia marehemu barua ya kumtaka ajaze fomu ya kulipwa mapunjo ya mshahara baada ya kupanda daraja.

  Marehemu Richard Mutakulemberwa aliyekuwa mwalimu katika shule ya sekondari Kahororo iliyopo Manispaa ya Bukoba, alikutwa na mauti August,19 mwaka 1998 wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Kwa mujibu wa barua iliyosainiwa na T.Kagumisa kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ambayo Fikra Pevu ina nakala yake, pamoja na mambo mengine inamtaka marehemu kujaza fomu kutokana na utaratibu mpya wa malipo ya malimbikizo.

  [​IMG]Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk Shukuru Kawambwa

  Pia barua hiyo ya Januari 4, 2012 iliyotumwa kupitia shule aliyokuwa akifundisha marehemu ya Kahororo inamtaka kufuata maelekezo kwa mujibu wa barua hiyo ili madai yake yaweze kushughulikiwa.

  "Tafadhali mara upatapo barua hii jaza na utume kwa Katibu Mkuu fomu halisi na nakala moja (photocopy), pia ambatanisha barua yenye maelezo sahihi ya madai,nakala ya barua ya kupandishwa na kukubali cheo na ‘salary slip' ya karibuni," inaeleza sehemu ya barua hiyo kwenda kwa marehemu.

  Pia mbali na barua hiyo kumtakia marehemu ushirikiano mwema katika kukamilisha zoezi hilo, inamkumbusha kuwa nyaraka zote lazima zipite kwa mkuu wake wa kituo na kutumwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

  Naye mjane wa Marehemu, Specioza Kamala mbali na kusikitishwa na hali hiyo, alisema tangu kufariki kwa mume wake mwaka 1998 ameendelea kufuatilia madai ya mume wake bila mafanikio na hata kufika Wizarani huku akipewa kauli za ahadi.

  Alisema kuwa mbali na kuwa alishapata barua hiyo aliyoandikiwa marehemu mume wake, anachokumbuka ni kuwa mme wake alifariki kabla hajalipwa mapunjo ya mshahara baada ya kupandishwa daraja ambayo ameendelea kuyafuatilia bila mafanikio na kuwa mirathi ya marehemu ilishatolewa.

  "Alipanda daraja mwaka 1996 na kufariki kabla ya kulipwa mapunjo yake ya mshahara,suala hili nilishawaeleza hata watu wa Utumishi wa Umma kutoka Dar es salaam na kunielekeza niende Wizarani na baada ya kwenda walisema faili lake halipo," alisema mama huyo ambaye pia ni mwalimu katika moja ya shule za msingi Mkoani Kagera.

  Alipoulizwa kama suala hilo liliwahi kufika katika Ofisi za Chama cha Walimu Mkoani hapa, Katibu wake wa Mkoa Aaron Masalu alisema halijafika katika ofisi hiyo huku akilihusisha na mfumo mbovu wa utunzaji wa takwimu za watumishi.

  Pia alidai vyombo vinavyomshughulikia mwalimu havina utaratibu mzuri wa mawasiliano na kusema kuwa sasa wakati umefika wa mwalimu kushughulikiwa na chombo kimoja tofauti na ilivyo sasa.

  Alisema mbali na kuwa utaratibu uliopo unaweza kuchelewesha malipo ya mhusika au kuyakosa kabisa alidai suluhisho ni kuwa namwajiri mmoja ambapo hivi sasa walimu wanashughulikiwa na Tamisemi,Utumishi wa Umma na Wizara yenyewe.

  Imeandikwa na Phinias Bashaya-Kagera
   
 2. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  nyakati za kutambua kaki ndo iwe vazi la taifa ndio huu.
   
 3. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Duh! mpaka sasa hivi bado serikali inashindwa kutoa ushirikiano kwa Mjane ikiwa ni kukumbuka na kuthamini mchango wa Mwl. Richard Mutta.

  kwakeli inasikitisha sana, japo mleta thread hii namshukuru, kwani amenikumbusha mwl. wangu wa somo la Civics(1993-1996).
  tulizoea kumuita Mwl. Mutta na henzi hizo chini ya mwl. Mutta Kahororo ilisifika kwa kiwango cha Ufaulu, Usafi ikiwa ni pamoja na kuwa na mpangilio mzuri wa mabweni kama vile Azimio, Umoja,Mapinduzi na Jitegemee.
   
 4. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Urasimu mwiingi, na kumbukumbu kidoogo. Serikali bado ina shughuli pevu ya kujipanga vizuri na kuwa na kumbukumbu sahihi, ili itoe haki kwa raia wake wote.
   
 5. M

  Mpigaji JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2012
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wizara ya Elimu inaongoza kwa MADUDU!Kuna watu wanaacha kazi kwa maandishi,wanaendelea KULIPWA MISHAHARA YA BURE zaidi ya Miaka 5!!

  Hawana mfumo mzuri wa kutunza kumbukumbu za Watumishi!Mwajiriwa anajiendeleza kielimu, akimaliza anapangiwa kituo kipya!Wanaripoti vituo vipya,wanalamba posho ya Kujikimu, nauli pamoja na mizigo!Kisha wanaingizwa katika Malipo ya Mishahara upya!Watu wanasepa kurudi katika vituo vyao vya zamani!! Wakipokea mishahara mara mbili!!
   
 6. mujusi

  mujusi JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2012
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 237
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hii kwa upande mwingine inawezekana kabisa na ikaangukia katika ile sehemu ya watumishi hewa. kama kumbukumbu zinaonyesha bao yu hai basi ujue kuna mtu ankula mshahara wake mpaka nae atakapokufa. kwenye zoezi la uhakiki madeni wengi wameomgezea madeni na wengine kuweka watu ambao hawapo.

  Sio vizuri kuionea Serikali kwa utendaji wake na juu ya uhakiki wa madeni ya Waalimu mabo kama haya yapo mengi na wezi wengi ambao jioni tunakunjwa nao Bia nahuku kuikashifu Serikali.

  Pengine hata huyu mjane madai yake yanacheleweshwa labda huko shuleni au manispaa bado wanaonyesha anapokea mshahara.
  Bila ushirikiani wa wananchi wizi na usumbufu bado utaendelea na kuiona serikali ina makosa kila siku kumbe wenye makosa ni wabadhirifu ambao ndio waume zetu, dada zetu, marafiki zetu na wake zetu.
   
 7. Z

  Zedikaya Senior Member

  #7
  Feb 25, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa nini wasichukue hiyo posho hali wakati wanaajiriwa hawakupewa hela ya kujikimu na mishahara hawakulipwa yote waliolimbikiza,
  walitakiwa kusomeshwa na mwajiri lakini hawakusomeshwa na ruhusa yenyewe wamepata kwa mbinde huku mishahara ikifungwa,
  ingekuwa wewe ungeacha kwenda kuzichukua,
  think twice br/sister kabla ya kuweka maj***u yako hapa,
  wezi wa hela wako wazi akina lowasa, rostam ,chenge,kikwete na familia yake, ccm wote nk,
  wamekushinda unaanza kuonea waliokwisha onewa na kunyonywa
   
 8. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  tuache kulalamika ,tufanye yanayostahili kufanywa.tusitafute sababu kwa kuwa fulani anaiba nasi tuibe..NO! lets be realistic and act accordingly!
   
 9. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2012
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  heading ilinishitua sana... kumbe ungehariri isomeke
  marehemu atakiwa kujaza form.
   
 10. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Maiti ni physical dead body wakati marehemu ni status
   
Loading...