Maiti wadaiwa kuibiwa mali ajali ya meli Zanzibar

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,187
32,855
Mali nyingi za marehemu waliokufa katika ajali ya MV Spice Islanders hazijuulikani zilipo yakiwemo mapambo ya dhahabu kama pete, cheni na herini na pesa tangu kutokea ajali hiyo Septemba 10, mwaka huu.

Uchunguzi wa NIPASHE umebaini idadi kubwa ya watu waliopewa maiti zao kwenda kuzika wamekutwa vitu hivyo vimeondolewa na wengine kubakia na alama vidoleni za kuonyesha kuvuliwa pete za dhahabu.

Imeelezwa kwamba baadhi ya maiti zilizokuwa zikifikishwa katika kituo cha Maisara baadhi ya waokozi walikuwa wakizivua maiti hizo mapambo wakidai zinahifadhiwa, lakini hadi sasa vitu hivyo au fedha hazifahamiki zilipohifadhiwa.

“Mie nilivyouliza nilijibiwa maiti huwezi kuiacha na mapambo ya dhahabu wakaniambia wanawavua kasha wanakabidhi Polisi, lakini sijasikia zimehifadhiwa wapi,” alisema mmoja wa waokozi.

Imeleezwa baadhi ya watu walionekana wakifanyakazi ya kufungua vidani na kuvua pete maiti, zilipokuwa zikifikishwa kwa utambuzi katika kituo cha Maisara kwa madai maiti hairuhusiwi kukaa na mapambo lakini hadi jana hakuna taarifa ya kukusanywa vitu hivyo na kukabidhiwa katika vyombo husika.

“Mie ndugu yangu alikuwa nakwenda kujenga Pemba nyumba alikuwa na kiango kikubwa cha pesa alichoniambia pesa kazifunga kwenye mkwiji wa kanga bahati nzuri maiti yake tumeipata mkwiji haupo,” alisema Time Baraka, mkazi wa Tomondo.

Alisema hadi sasa hawajapokea taarifa yoyote kuhusu mali zilizookolewa kufuatia ajali hiyo ambapo vikosi mbalimbali vilishiriki kuokoa abiria pamoja na wananchi hasa wa Nungwi ambao walifanya kazi hiyo muda mfupi baada ya kuripotiwa kuzama.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, alisema hadi juzi hajapokea taarifa yoyote ya kupatikana mapambo ya dhahabu au fedha na kuhifadhiwa kabla ya kupewa wahusika.

Hata hivyo, alisema katika kituo cha Nungwi anazo taarifa za kupatikana nguo ambazo zimehifadhiwa pamoja na mafriji mawili na magodoro ambavyo viliokotwa na wavuvi katika mwambao wa bahari ya Mkoani na tayari vimekabidhiwa Polisi.
CHANZO: NIPASHE

 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom