Maisha yetu ni reflection ya akili zetu.

Maisha yetu ni reflection ya akili zetu.

jf user

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2018
Posts
777
Reaction score
625
Maisha yetu ni reflection ya akili zetu, (We Become What Think About) tunachowaza akilini mwetu ndicho kinachojionesha katika maisha yetu ya kawaida.

Hakuna yeyote ninayemfahamu aliyepata maendeleo ya maana kwa kupitia ushirikina. Wengi wanaoamini ushirikina wana maisha ya chini na ya kimasikini sana. Akili ya binadamu iko kama bakuli, inabeba kila kitu, inabeba mawazo, fikra mbalimbali (chafu na safi) kilichomo katika akili za wengi ni kile kilicholishwa na kukaa kwa muda mrefu sana kwenye bakuli (akili). Mwenendo wa maisha ya mtu fulani unayoyaona leo, yawe maisha yenye mtazamo hasi au chanya, hicho kitakuwa kielelezo cha akili yake. Aina ya maisha anayoyaendesha leo ndicho alicholisha kwenye akili yake. Kama akili yako imelishwa kwamba uchawi au ushirikina utakusaidia na utakupatia maendeleo, na kwamba huhitaji kufanya kazi, basi hivyo ndivyo akili yako itakavyofanya kazi. Akili zetu zina nguvu kubwa sana kuliko tunavyodhania. Akili zetu zinaweza kutufanya tufanye mambo makubwa mno hata kujishangaa wenyewe haijalishi mambo hayo ni hasi au chanya. Kama akili zetu zililishwa kwamba, ili ufanikiwe, weka bidii, usikate tamaa, jitume LAZIMA utafanikiwa.

Kama kweli uchawi au ushirikina ungekuwa unalipa, basi timu zetu za mpira za Simba na Yanga zingetamba sana barani Africa na duniani. Kila siku Simba na Yanga zingekuwa zinazifunga sana timu kubwa TP Mazembe, Man U, na kadhalika, lakini haiwezekani, kwasababu timu zinashinda na kuendelea kufanya vizuri kwasababu ya juhudi mbalimbali za muda mrefu, kama kujiwekea malengo, kufanya mazoezi, kujituma, nidhamu ndio siri ya ushindi na mafanikio.

Usiruhusu kuilisha akili yako vitu vichafu (uchawi, ushirikina, wizi) kwasababu maisha yako ni reflection ya akili yako. Kama unataka kufanikiwa chochote maishani mwako kwanza kabisa LISHA AKILI YAKO mambo safi, kuwa na fikra chanya, amini kwamba unaweza kupata unachotaka. Weka malengo, weka juhudi kubwa, weka ubunifu pamoja na nidhamu, utashangaa jinsi unavyoweza kupanda na kuvutia mambo mengi mazuri upande wako na hatimaye kupata ushindi na mafanikio makubwa maishani mwako.

Kama mtu amefanya kazi kwa Mhindi kwa miaka mingi akilipwa fedha kiduchu, au mfano huyo mama anayelalamika kwamba mumewe ana elimu ya Chuo Kikuu lakini anafanya kwenye 'Internet Cafe' analipwa fedha kidogo na Mhindi na hawana mafaniko yoyote. Kwahiyo kosa ni la nani?! Kosa sio la Mhindi, na wala SIO kwasababu ETI Wahindi ni 'chuma ulete', nani alimzuia kuondoka kwenda mahali pengine kutafuta mafanikio - ni akili yake tu.

Kosa ni la hao wafanya kazi na kinachowaumiza ni;

1) Imani waliyojijengea kwamba wao hapo walipo ndipo wanapostahili na ni haki yao kupata hicho wanachopata;
2) Wana hofu, hivyo wanaogopa kufanya maamuzi magumu, kwamba wakijaribu kuondoka labda hawatafanikiwa na tayari wameshaathirika kisaokolojia (akili yao imeshalishwa hivyo) kwamba hawawezi na hawataweza.
3) Aidha wamerogwa, au kuna nguvu za kiimani na kishirikina wamefanyiwa

Ili kujenga uhalali wa maisha haya ya chini, ya kimasikini, yasio na mafanikio wanayoishi, ndo wanakuja na hoja hafifu kwamba 'chuma ulete' au 'msukule' n,k, ukweli ni kwamba wengi ni wavivu, wana hofu ya kufanya maamuzi magumu.

Kuanzia leo hebu jaribu hii;
Kila siku dakika chache kabla kulala na dakika chache kabla kuamka, jiambie maneno chanya kwamba unataka upate kitu fulani, au ufanikiwe kitu fulani, jiambie kutoka ndani kabisa ya moyo wako na kwa dhati kabisa, hakikisha unafanya hivi kila siku dakika chache kabla ya kulala na dakika chache mara tu baada ya kuamka, kwa kwa siku thelathini utashanga nguvu unayoiweka kwenye akili yako na hatimaye itajitokeza kwenye maisha yako ya kawaida.

Ilishe akili yako vitu vizuri ili upate na uishi maisha ya mafanikio.
 
Ushauri wako mkuu hauna tofauti na hao wanaomini uchawi kuwa utawasaidia.

"hakikisha unafanya hivi kila siku dakika chache kabla ya kulala na dakika chache mara tu baada ya kuamka, kwa kwa siku thelathini utashanga nguvu unayoiweka kwenye akili yako na hatimaye itajitokeza kwenye maisha yako ya kawaida."

Sasa kufanya hivyo kuna mahusiano na gani maendeleo ya mtu au kuna tofauti gani na uchawi maana hapo pia et unaamini akili inaweza kukusaidia?
 
Kusema ni rahisi kuliko kutenda kufikiri ni kitu kigumu kuliko vyote hapa dunia ndo maisha ya watu hayafanani kwavile hatuwezi kufikiri sawa
JAH BLESS,
 
Maisha ni mapambano hivyo silaha zote muhimu.....[emoji1783][emoji1783][emoji1783]
 
Back
Top Bottom