Maisha yangu na mahusiano

PAND PIERI

Senior Member
Joined
Jul 30, 2020
Posts
183
Reaction score
275
Raha ya JF ni kusema unachokiwaza, ulichokipitia au kureferesh mind bila kuogopa kwa Sababu hatujuani. Mimi mpaka Sasa nina 27 yrs lakini nimekuwa kwenye mahusino na wanawake/wasichana watano tu, najua mabaharia mtanilaumu kuwa nimewangusha lkn hiyo ndio hali halisi hatulingani na tunatofautiano kwenye kuchagua mtu wa kudate nae.

Wa kwanza tulianza nikiwa A -level, Huko nyuma (O -level) nilikuwa mdomo zege kwa hiyo sikuona haja ya kujisumbua wakati Sina hata swaga wa kuconvince dem, huyu aliniacha baada ya mwaka moja Sababu kubwa kuniacha aliniambia siendani nae,yeye alipenda wanaume wanao vaa mimodo(wa kisasa ) wakati mm nimetoka huko kijijini nina mabwanga makubwa kubwa na hata kuvaa modo sijazoea/ ilinishida,niliumia Sana lkn ilibidi nikubali hali halisi na namba yake sijafuta hadi leo .

Wa pili tulikutana chuo, binti wa kichaga mrembo kweli kweli,huyu alipenda hela kuliko masomo yupo radhi asiende chuo hata wiki mbili ili mradi Mishe zake za utafutaji /biashara zisome, ilibidi niwe mwalimu wake baada ya kutoka kwenye Mishe zake nampigia pindi, assignment namfanyia na saa zingine ikiwezekana namfanyia hadi test, nilimpenda coz alikuwa yuko free nikitaka sex naletewa immediately ,tulidumu kwa miaka miwili .Tuliachana baada ya kuona mapicha picha kutoka kwa her business partner,ikabidi nitembee taratibu kuliko kusubiri stress,

Wa tatu ilitokea tu naweza kusema kimasiara, huyu mdada mrembo alipandia ubungo /Riverside kwenda kimara, alipendeza Sana.Kumbe kipindi anatoka alisahau nauli nyumbani akadhani ameweka kwenye pochi kumbe hola,imefika muda wa konda kukusanya riziki yake,mdada kucheki pochi hola,akamwambia konda "samahani Kaka nimesahau nauli naomba unipe namba yko nitakutumia " weeee konda aliwaka Kana kwamba hakuona uzuri wa yule dada mtoto wa kinyamwezi na matusi juu pamoja na kumdhalilisha yule dada.

Nikamlipia yule dada nauli ili konda apunguze maneno,nashuka tu yeye anashuka na kunishukuru Sana, nikamwambia Wala ucjali akaniomba namba ..tukawa Kama marafiki hivi kama wiki moja then strong relationship ikaanza tena Kali ..huyu nilimwacha alikuwa na mchumba wake office wa jwtz mwenye nyota tatu,lkn huyo mchumba wake kwa Sasa ni mume wake halali wa ndoa, hakai kwake Mara nyingi anasafiri kikazi.binti wa kinyamwezi amebaki kuwa my best friend.

Wa nne ni dada wa kingoni lkn ni mke wa mtu, huyu dada nilipoajiriwa sikuwa na uzoefu yeye ndio alikuwa ananipa experience kwenye department yetu,alinifundisha kazi na maujanja kibao hadi nikaona maisha ya kazi nyepesi .Huyu dada mumewe alihamishwa Dodoma (makao makuu) yeye akabaki Dar,siku moja akamfanyia mumewe suprise akamfumania mumewe na mwanachuo wa Udom ,si unajua tena wanawake wakifumania wanaume wanakuwa na kelele cjui walikuwaje huko Dodoma, kesho yake akarudi Dar.

Ilikuwa jpili saa kumi na mbili akanipigia simu na kuniuliza nilipo nikamwambia nipo ghetto ,akasema ana shida na mm nimfuate ,kufika kwake barabarani akaniambia turudi ghetto.Hapo kanisimulia A-Z ilivyotokea huko Dodoma baada ya hapo akaoga na kuingia kupumzika kitandani,mm nikadhani labda akipoa atarudi kwake kumbe mwezangu anampango wa kumkomoa mumewe ...hahahah yani tulilala nae kesho yake akaomba likizo bila malipo akaa kwangu hadi likizo ikaisha ndipo akarudi kwake baada ya mumewe kwenda kwao na wazazi wake kumwita kuwasuluisha.Amebaki mshauri wangu na rafiki yg wa ukweli.

Wa tano ni binti wa kijita,huyu tulikutana kwenye mwendo kasi ,alinikanyaga maksudi nikamuliza akanijibu hovyo na Mimi nikamchenjia tuliposuka tu nikamfuata tukaongea vzr tukamaliza utofauti na kupeana namba, nimekaa nae miezi sita anapenda bata, kwa muda niliokuwa nae sikubahatika kununua hata kitu Cha maana, maisha yetu yalikuwa ya bata sana ,hana plan ya maisha siku zote ni kujirusha tu, nilishindwa hayo maisha nikajiondoa mapema.

Wa sita ni mrembo wa kisukuma, tuna miaka miwili kwenye mahusino, nimepiga hatua kubwa kimaendeleo tangie nianze nae mahusino, ameniconvince nikamiliki viwanja na maendeleo kadhaa, ni bahiri (hana matumizi mabaya ya hela) ana malengo makuwa ni mpiganaji Sana ,hana mawazo ya Kula bata hata kidogo,amenibadilisha kimaono ,kiimani na kifikra.
 
mkuu hiyo list fupi?!! dah kwangu nimekua na mahusiano na wasichana wawili tu mpaka sasa
wakwanza nilianza nae toka utotoni ila mambo yakabadilika mwaka jana, kwa sasa nipo na mwengine mpaka sasa hivi.
Mkuu watu wana list ndefu wanaona hata aibu kusema.
 
Hata Huyo mtaachana nimekucheki weeee nimegundua ukikaa sana kwenye mahusiano ni 2yrs
 
List fupi
πŸ˜‚πŸ˜‚ Hii komenti yako imenishutumu Sana maana huyu ana 6 umekomenti list fupi nikajifikiria Mimi hata hao 3 hawafiki it means list ni fupi zaidi..
Ntaongeza juhudi kidogo nifike kwenye list fupi na sio list fupi zaidi..πŸ˜…
 
Sawa mkuu najua nimewaangusha lkn ndio ukweli,kuna dogo mmoja ana 25 yrs yeye aliniambia kila mwezi lazima alale na mwanamke tofauti na mpz wake akikosa anamalizia kwa wanao jiuza na amejiwekea hivyo Kama utaratibu kwa hyo kipato chake kinaishia kwa mademu na mavazi.
 
Wewe mbinguni moja kwa moja kwa umri huo nilikuwa nimegonga kama59
 

Sio ujanja, akili za mabaharia changanya na za kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…