Maisha yanazidi kuwa magumu kote duniani

Maisha yanazidi kuwa magumu kote duniani

Ndio maisha magumu kote. Lakini hao mahomeless Marekani wanajitakia tu kwasababu waneamua kuishi hivyo. Kazi zipo nyingi tu Marekani na ulaya ni maamuzi tu. Ukijituma hata kidogo huwezi kukosa Dola 300 kwa wiki ama 1200 kwa mwezi baada ya kodi na iyo umefanya kazi kwa kawaida tu. Ukitoa kodi ya nyumba 400-600 ukabaki na 600 ya matumizi unaishi vizuri kabisa Hadi unasave.

Mbona wahamiaji wengi kutoka nchi maskini wakienda Marekani au ulaya siyo homeless?

Pia Kuna shelter za watu homeless nyingi tu ila Hawa watu hawapendi kwenda kwasababu Kuna sheria ukiishii humo licha ya malaz na msos bure Ndo maana wanaprefer kulala nje.

Maisha ya huzuni Sana ya kujitakia.
 
Hivi huyu Putin kweli anasababisha wote tunasota, hivi hatuwezi kuungana wote tukaenda kumnyonga hapo KIREMLIN!?
 
Hivi huyu Putin kweli anasababisha wote tunasota, hivi hatuwezi kuungana wote tukaenda kumnyonga hapo KIREMLIN!?
Hapo ndo ukubali Kremlin ina nguvu sana kuliko tunavyoaminishwa na propaganda za magharibi
.
Mtu kawekewa vikwazo na bado anasumbua.
 
Hata Kama anaingiza hela nyingi ila zote zinaishia kwenye chakula anaishia kuwa homeless kuna maana gan sasa! Si Bora mi napata pesa kidogo lkn Nina uhakika wa kula na kulala nyumban kwangu
Mkuu waneamua tu kuishi hivyo. Anaona aibu kufagia ama usafi ambapo ukifanya tu kawaida hukosi 1200 USD. Kodi SI zaidi ya 600. Chakula mtoni siyo ishu kabisa. Kuna sehemu Hadi bure unapewa. SEMA Kam mvutaji Sana wa sigara itakugharimu.

Sasa unakuta hao homeless ni raia kabisa Wana documents zote Lakini wanaish maisha ya huzuni yakujitakia.
 
Hapo ndo ukubali Kremlin ina nguvu sana kuliko tunavyoaminishwa na propaganda za magharibi
.
Mtu kawekewa vikwazo na bado anasumbua.
Tukiamua wote kupeleka majeshi kumdunda, bado atatusumbua tu?

EU yote na USA, pamoja na sisi Afrika tunaoumia na kupanda kwa bei, bado tutamshindwa?
 
Maisha hayajawahi kuwa magumu, ugumu wa maisha uja pale mind akili inapogota kureasoning au umestaki, unaweza iboost au iformat kwa kuiingizia taarifa mpya kutoka vyanzo mbalimbali vya taarifa za maarifa mapya then unapata mwanga mpya unasonga.
Na ndio maana Sasa hivi wajanja Ndo wanazidi kuwa matajiri. Ni akili tu. Wee jiulize unaishi kwenye nchi ajira zipo nyingi Tena za kumwaga halafu wewe ni raia Bado unalala nje. Unashindwa hata kukodi tu kastudio apartment ya dollars 300-400 kwa mwezi kama haka chini? Unabaki kushangaa WTF? Ukifanya kazi masaa 7 kwa siku kwa siku 5 kwa wiki hukosi 1200-1300 USd kwa mwezi. Utoe 400 kwenye kodi unabaki 900. kwenye iyo 900 toa 70 ya nauli umeme 35 internet 25. Unabaki 760
ORIGINAL (3).jpeg
ORIGINAL.jpeg
ORIGINAL (5).jpeg
ORIGINAL (6).jpeg
 
Maskini wa Marekani anaweza kuingiza pesa nyingi kuliko mtu wa kipato cha Kati hapo Tanzania. Sasa wewe kaa hapo jidanganye wote mnapitia ugumu sawa.
N kweli lakn ,kwao vitu n gharama kubwa kuanzia matibabu ,msosi hadi pango la nyumba.

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
N kweli lakn ,kwao vitu n gharama kubwa kuanzia matibabu ,msosi hadi pango la nyumba.

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
Kuna kazi nyingi zakuingiza kipato cha kuhimili hizo gharama kama ukiwa mchapa kazi. Kumbuka pia ubora wa matibabu/hudumu za afya, misosi na nyumba upo juu kuliko sisi. Leo hii unaweza kuwa na Tshs million 500 hapo Tanzania na ukafa kwa malaria.
 
Na ndio maana Sasa hivi wajanja Ndo wanazidi kuwa matajiri. Ni akili tu. Wee jiulize unaishi kwenye nchi ajira zipo nyingi Tena za kumwaga halafu wewe ni raia Bado unalala nje. Unashindwa hata kukodi tu kastudio apartment ya dollars 300-400 kwa mwezi kama haka chini? Unabaki kushangaa WTF? Ukifanya kazi masaa 7 kwa siku kwa siku 5 kwa wiki hukosi 1200-1300 USd kwa mwezi. Utoe 400 kwenye kodi unabaki 900. kwenye iyo 900 toa 70 ya nauli umeme 35 internet 25. Unabaki 760 View attachment 2329941View attachment 2329942View attachment 2329943View attachment 2329944
Unaongea kirahisi rahisi tu kijana
 
Ukiangalia mwenendo wa kiuchumi duniani utagundua hali ya maisha kwa sasa ni mbaya. Si Marekani,China,Ujerumani au Uingereza kote kimeumana. Bei kubwa ya mafuta na gesi,chakula,ukame na uhaba wa maji safi, na"Rent" yote haya yamepelekea kupandisha sana gharama za maisha.

Leo Marekani miji kama ya Florida na Califonia kuna idadi kubwa ya Homeless people kutokana na watu kushindwa kumudu kodi ya nyumba(rent). Uingereza kuna mgomo wa wafanyakazi wa reli wakidai nyongeza ya mishahara ili kukabiliana na ukali wa maisha.

Nimekaa na kutafakari nikagundua sababu zinazosababisha dunia kuingia kwenye huu ugumu wa maisha.

1. Nchi kuwekeza pesa nyingi kwenye miundo mbinu ya kisasa. Siku hizi serikali za nchi nyingi duniani zimewekeza mabilioni ya dola kwenye miundombinu mipya ya kisasa km bandari,reli,viwanja vya ndege,barabara n.k na hivyo kuwasababishia wananchi mzigo mkubwa wa kodi.

2. Nchi kubwa kuendekeza vita vya kijinga na kutafta ubabe usio na maana. Kuna muda najiuliza hii vita ya Urusi na Ukraine ilikuwa na sababu gani za msingi km sio ubabe wa Urusi na NATO. Angalia ilivyoharibu hali ya uchumi wa dunia.Mbolea,Chakula,mafuta gesi vyote havishikiki.

3. Nchi kubwa kufanya uwekezaji mkubwa(mega investments) kwenye sayansi na technologia.

Kutokana na ushindani mkubwa uliopo baina ya Urusi,Marekani,China na washirika wao mabilioni ya pesa yamewekezwa kwenye sayansi na technology ili kila upande uwe juu ya mwingine. Kuna ushindani mkubwa wa silaha,anga za juu,mawasiliano n.k.

Marekani kwa mfano wametengeneza Telescope kubwa ya kutazama anga za juu itwayo James Webb Telescope(JWT) ambayo hadi inakamilika imegharimu dola bil.10 zaidi yaTrillion 20 za Kitanzania. Hapo unazungumzia karibu theluthi mbili ya bajeti yetu ya mwaka mzima. Vipi km pesa hii ingepelekwa kwenye kununua chakula na kuboresha huduma za maji ingeokoa watu wangapi duniani?

4.Mabadiliko ya tabia ya nchi. Hapa tunarudi palepale kwenye Ubabe wa kijinga. Nchi zinazoongoza kwa uchafuzi na uharibifu wa mazingira duniani kila mmoja hayuko tayari kupoteza. Ndio maana kila wakikubaliana kutia saini mkataba wa kupunguza gesi chafu kesho unasikia yule kagoma.

Wiki kadhaa zilizopita Ulaya wamekumbwa na joto na ukame mkali la hadi nyuzi joto 40 sababu kuu ni mabadiliko ya tabia ya nchi. Dunia inaangamizwa na maslahi ya wachache.

Kwa kifupi ugumu huu wa maisha kwa kiasi kikubwa umesababishwa na ubabe na ubinafsi wa mataifa makubwa uliopitiliza na ndo chanzo cha maumivu haya yote.

Nawasilisha.
Dunia ipi wee mwana fiisiieemuuu?
 
Back
Top Bottom