Maisha yamenipiga sana ila ninataka kutengeneza 50m kabla ya mwaka huu haujaisha

Nimesoma mazuri tu mabaya baki nayo mwenyewe
Nimejiunga jf toka 2015 lkn sijawahi kuanzisha thread. Huu ni uzi wangu wa kwanza na ninauandika nikiwa natiririkwa na machozi kutokana na kwamba hali mbaya mtaani.

Baada ya utangulizi huo niseme tu kuwa nimekaa nimetafakari sana kuhusu hatima ya maisha yangu haya magumu na nimefikia uamuzi wa kuwa milionea ndani ya mwaka mmoja tu kuanzia sasa. Tiririka nami jinsi nitakavyofanikisha ndoto yangu na naomba maoni yako!

MIMI NI NANI?
mimi ni kijana mwanaume mwenye miaka 24. Ni msomi wa degree ya ualimu niliyomaliza mwaka jana 2018. Baada ya kuhitimu nilirudi nyumbani kwa wazazi. Nimetafuta shule za kufundisha bila mafanikio. Nimetuma maombi shule nyingi sana lkn sijafanikiwa hadi sasa sina kazi.

Nimeona ni muda mwafaka sasa kufanya biashara.

MPANGO WANGU.
kwanza sina mtaji wa kufanya biashara kubwa. Mfukoni nina laki moja na nusu ti ambayo naamini baada ya mwaka mmoja itakua imenizalishia milioni 50 za kitanzania. (unaona kama haiwezekani, ila mimi naona inawezekana sana).

kwanza nitatoka mkoa nilipo na kwenda mkoa mwingine ambapo hakuna watu wanaonifahamu. Nafanya hivi kwa sababu najua wazi kuna baadhi ya kazi sitaweza kuzifanya nikiwa nimezungukwa na watu wanaonifahamu kama msomi wa degree. kuna aibu fulani hii nitakuwa nayo ambayo nahisi itanichelewesha kufikia malengo yangu.

Huko ninakoenda nimeshafanya maandalizi ya kupokelewa na kijana mmoja hivi tulisomaga naye chuo ambaye nimemwomba anihifadhi kwenye chumba chake kwa miezi kadhaa na ameridhia.

Nikifika kule cha kwanza nitafanya research kama wiki moja hivi kwa ajili ya kufungua genge la kisasa la kuuza matunda na mbogamboga za aina zote. Nitatafuta eneo lenye mkusanyiko wa watu wengi kisha nitatengeneza genge hilo kwa kutumia maturubai. Gharama sio kubwa nafahamu haitazidi elfu 50. Hapa sitanunua kiwanja kwa ajilo hiyo.

Baada ya hapo nitaanza kuuza bidhaa zangu. Hapa nitauza kila aina ya matunda unayoyafahamu na mboga za aina zote. sitaishia hapo nitaweka miwa, viazi, nazi, n.k. kwa siku 30 za mwanzo nategemea kupata laki sita kama faida nikiwa na maana kwa siku nitakua napata wastani wa elfu ishirini. Najua namna ya kuwanasa wateja. pia bidhaa zote nitakua nazichukua mashambani ambapo naamini bei itakua rahisi na faida itakua kubwa.

Baada ya huo mwezi wa kwanza wa biashara nitaongeza bidhaa za nafaka kwa maana ya mchele, sembe, maharage n.k . Nitafanya biashara hii kwa miezi minne tu na nina uhakika wa kupandisha mtaji wangu kutoka 150k hadi 4M.

Hatimaye nitamuweka mtu kwenye hiyo biashara ya genge ambaye nitatumia mbinu zangu kumfanya asiniibie sana. kisha naondoka na milioni nne zangu narudi nilipotoka maeneo ya nyumbani.

Nina leseni ya udereva hivo nitatafuta suzuki carry / kirikuu kwa njia ya kukodi ambapo hapa mjini huwa wanafanya unapeleka 20k kwa siku. Tutaandikishana mkataba niwe nampelekea kwa wiki.

Nikishapata kirikuu, nazunguka masokoni na maduka ya rejareja, migahawani na mahotelini niwe nawapelekea mchele mzuri ule super kabisa kwa bei pungufu kidogo ya bei waliyozoea. Lazima wanikubali tu kwan hakuna mtu asiyependa bidhaa nzuri kwa bei rafiki.

Kazi yangu itakuwa ku-link mashamba na masoko. Naingia shambani nachukua gunia za kutosha, naleta mjini kusambaza kwa wateja wangu. kutoka mashambani hadi mjini nitatumia malori ya mizigo kwa kulipia ila huku mjini nakua nasambaza kwa kirikuu ambapo mimi ni dereva vilevile mimi ni muuzaji. Nina mwili wa mazoezo kiasi kwamba kubeba magunia ni jambo rahisi kwangu.

kwa mishe hizi za kufanya kazi zaidi ya masaa 15 kwa siku nina uhakika wa kuingiza faida ya laki mbili kwa siku kwa mwezi milioni sita.

wakati huo huo nitachukus sehemu ya faida ya biashara hii na kufungua restaurant ndogo ila ya kisasa maeneo ya chuo. Nitaweka wadada wazuri wenye makalio makubwa wawe wafanyakazi wa mgahawa huu bcoz najua vijana wa chuo wanavyopenda mambo haya.

mgahawa huu utakua ktk usafi wa hali ya juu na chakula kitakua kitamu sana sana. Utofauti wangu na migahawa ya eneo hilo ni kwamba nitaweka utaratibu wa free delivery kwa wanachuo wakiwa hostel.

kwa kuwa nina biashara ya mchele na nafaka zingine basi naamini nitakuwa napata faida kubwa kwenye mgahawa huu kwani ni mimi mwenyewe najiuzia mchele.

Nitatumia social media kutangaza biashara zangu. kwa upande wa mgahawa kuna uwezekano wa kufikia wateja 1000 kwa siku. wengi wao naamini ni wale wa free delivery hostel. sasa kwa kila mteja nikipata faida ya 300/= maana yake ni laki tatu kwa siku kwa mwezi milioni tisa. inawezekana kabisa. delivery nitakua naifanya kwa kirikuu kwa sababu nitakua natenga muda wa kudili na business ya mchele muda wa lunch na dinner naenda kusambaza chakula. Hapa kazi tu!

kwa kifupi ndani ya mwaka mmoja:

1. biashara ya matunda niliyoanza nayo itakua imeniingizia faida ya 6M.

2. usambazaji mchele itakua imeniingizia 25M

3. mgahawa utakua umeniingizia 19m

Karibuni kwa maoni..msinitukane wala kunibeza, naomba mnishauri kama hizi fikra zinatimilizika au ni za kusadikika tu. Haya ni makadirio ya juu hata nikipata milioni 20 nitakua somewhere.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenikumbusha story za hadithi za Halinacha na Habunwasi! Wakati huo alikuwa anatembeza vyombo vya udongo sahani, glass, vikombe, n.k. katembea sana kachoka huku njaa inauma! Kaanza kujipa matumaini na kupanga story ndefu na nzuri ya kujipa matumaini. Basi, mwishoni kasema ataoa binti mrembo atamwandalia chakula na kumletea ale! Atafanya kumlingia na kudeka kutokana na historia ya jinsi alivyopata hiyo hela kwa taabu. Sasa huyo binti mrembo akimsisitizia na kumuomba ale chakula ndipo atainua mguu na kupiga teke hicho chakula. Kumbe hile ananyanyua mguu na kupiga teke akapiga teke vile vyombo vya glass na kuvunjika vyoote na ndoto zake zikaishia hapo.
Mleta Uzi anza kwa kufanya unachokiamini kuliko kuleta hadithi ambazo kwa wenye uzoefu wa maisha tunaona hujui unalopanga kufanya.
 
Tunataka mrejesho
Nimejiunga jf toka 2015 lkn sijawahi kuanzisha thread. Huu ni uzi wangu wa kwanza na ninauandika nikiwa natiririkwa na machozi kutokana na kwamba hali mbaya mtaani.

Baada ya utangulizi huo niseme tu kuwa nimekaa nimetafakari sana kuhusu hatima ya maisha yangu haya magumu na nimefikia uamuzi wa kuwa milionea ndani ya mwaka mmoja tu kuanzia sasa. Tiririka nami jinsi nitakavyofanikisha ndoto yangu na naomba maoni yako!

MIMI NI NANI?
mimi ni kijana mwanaume mwenye miaka 24. Ni msomi wa degree ya ualimu niliyomaliza mwaka jana 2018. Baada ya kuhitimu nilirudi nyumbani kwa wazazi. Nimetafuta shule za kufundisha bila mafanikio. Nimetuma maombi shule nyingi sana lkn sijafanikiwa hadi sasa sina kazi.

Nimeona ni muda mwafaka sasa kufanya biashara.

MPANGO WANGU.
kwanza sina mtaji wa kufanya biashara kubwa. Mfukoni nina laki moja na nusu ti ambayo naamini baada ya mwaka mmoja itakua imenizalishia milioni 50 za kitanzania. (unaona kama haiwezekani, ila mimi naona inawezekana sana).

kwanza nitatoka mkoa nilipo na kwenda mkoa mwingine ambapo hakuna watu wanaonifahamu. Nafanya hivi kwa sababu najua wazi kuna baadhi ya kazi sitaweza kuzifanya nikiwa nimezungukwa na watu wanaonifahamu kama msomi wa degree. kuna aibu fulani hii nitakuwa nayo ambayo nahisi itanichelewesha kufikia malengo yangu.

Huko ninakoenda nimeshafanya maandalizi ya kupokelewa na kijana mmoja hivi tulisomaga naye chuo ambaye nimemwomba anihifadhi kwenye chumba chake kwa miezi kadhaa na ameridhia.

Nikifika kule cha kwanza nitafanya research kama wiki moja hivi kwa ajili ya kufungua genge la kisasa la kuuza matunda na mbogamboga za aina zote. Nitatafuta eneo lenye mkusanyiko wa watu wengi kisha nitatengeneza genge hilo kwa kutumia maturubai. Gharama sio kubwa nafahamu haitazidi elfu 50. Hapa sitanunua kiwanja kwa ajilo hiyo.

Baada ya hapo nitaanza kuuza bidhaa zangu. Hapa nitauza kila aina ya matunda unayoyafahamu na mboga za aina zote. sitaishia hapo nitaweka miwa, viazi, nazi, n.k. kwa siku 30 za mwanzo nategemea kupata laki sita kama faida nikiwa na maana kwa siku nitakua napata wastani wa elfu ishirini. Najua namna ya kuwanasa wateja. pia bidhaa zote nitakua nazichukua mashambani ambapo naamini bei itakua rahisi na faida itakua kubwa.

Baada ya huo mwezi wa kwanza wa biashara nitaongeza bidhaa za nafaka kwa maana ya mchele, sembe, maharage n.k . Nitafanya biashara hii kwa miezi minne tu na nina uhakika wa kupandisha mtaji wangu kutoka 150k hadi 4M.

Hatimaye nitamuweka mtu kwenye hiyo biashara ya genge ambaye nitatumia mbinu zangu kumfanya asiniibie sana. kisha naondoka na milioni nne zangu narudi nilipotoka maeneo ya nyumbani.

Nina leseni ya udereva hivo nitatafuta suzuki carry / kirikuu kwa njia ya kukodi ambapo hapa mjini huwa wanafanya unapeleka 20k kwa siku. Tutaandikishana mkataba niwe nampelekea kwa wiki.

Nikishapata kirikuu, nazunguka masokoni na maduka ya rejareja, migahawani na mahotelini niwe nawapelekea mchele mzuri ule super kabisa kwa bei pungufu kidogo ya bei waliyozoea. Lazima wanikubali tu kwan hakuna mtu asiyependa bidhaa nzuri kwa bei rafiki.

Kazi yangu itakuwa ku-link mashamba na masoko. Naingia shambani nachukua gunia za kutosha, naleta mjini kusambaza kwa wateja wangu. kutoka mashambani hadi mjini nitatumia malori ya mizigo kwa kulipia ila huku mjini nakua nasambaza kwa kirikuu ambapo mimi ni dereva vilevile mimi ni muuzaji. Nina mwili wa mazoezo kiasi kwamba kubeba magunia ni jambo rahisi kwangu.

kwa mishe hizi za kufanya kazi zaidi ya masaa 15 kwa siku nina uhakika wa kuingiza faida ya laki mbili kwa siku kwa mwezi milioni sita.

wakati huo huo nitachukus sehemu ya faida ya biashara hii na kufungua restaurant ndogo ila ya kisasa maeneo ya chuo. Nitaweka wadada wazuri wenye makalio makubwa wawe wafanyakazi wa mgahawa huu bcoz najua vijana wa chuo wanavyopenda mambo haya.

mgahawa huu utakua ktk usafi wa hali ya juu na chakula kitakua kitamu sana sana. Utofauti wangu na migahawa ya eneo hilo ni kwamba nitaweka utaratibu wa free delivery kwa wanachuo wakiwa hostel.

kwa kuwa nina biashara ya mchele na nafaka zingine basi naamini nitakuwa napata faida kubwa kwenye mgahawa huu kwani ni mimi mwenyewe najiuzia mchele.

Nitatumia social media kutangaza biashara zangu. kwa upande wa mgahawa kuna uwezekano wa kufikia wateja 1000 kwa siku. wengi wao naamini ni wale wa free delivery hostel. sasa kwa kila mteja nikipata faida ya 300/= maana yake ni laki tatu kwa siku kwa mwezi milioni tisa. inawezekana kabisa. delivery nitakua naifanya kwa kirikuu kwa sababu nitakua natenga muda wa kudili na business ya mchele muda wa lunch na dinner naenda kusambaza chakula. Hapa kazi tu!

kwa kifupi ndani ya mwaka mmoja:

1. biashara ya matunda niliyoanza nayo itakua imeniingizia faida ya 6M.

2. usambazaji mchele itakua imeniingizia 25M

3. mgahawa utakua umeniingizia 19m

Karibuni kwa maoni..msinitukane wala kunibeza, naomba mnishauri kama hizi fikra zinatimilizika au ni za kusadikika tu. Haya ni makadirio ya juu hata nikipata milioni 20 nitakua somewhere.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
milionea wa kesho tunaomba mrejesho huku mkuu..... mambo ni magumu sana mtaani!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna possibilities tatu hapa. 1) kafanikiwa na yuko bize na biashara hana tena time na Jf kutuaminisha tulichompinga. 2) kajaribu kufanikisha ndoto kakutana na kisiki now kafyata mkia. 3) hakunyanyua hata kidole kufanikisha alichojaribu kutuaminisha.
 
Don’t get trapped into your own romantic desire for getting rich quickly. Wealth increases gradually in a number of years even in decades. Getting rich quickly schemes will not help you. Come again with long term goals to get rich not just in within a year, that’s a lie.
 
Back
Top Bottom