Maisha yako ni nini?

Maisha yako ni nini?

Rugaikamu

Member
Joined
Aug 8, 2017
Posts
37
Reaction score
20
Dunia ni nyumba iliyojaa kila aina ya mabadililo na imebeba wanadamu wa kila tabia, nashukuru wazazi huwa hawako mbali siku zote kuniambia watendayo walimwengu wema, ubaya na kipi chema kipi kipindi nikuwapo.
Walinifundisha vitu muhimu kuhusu Mimi.

1.Mwili
Wakaniambia mwili wako ni sawa na hekalu ambalo mfalme ni wewe una uwezo wa kulijenga na kulibomoa hekalu wewe mwenyewe.
Nikauliza nitalibomoaje mwenyewe "walimwengu wana kupambana kila hali kuharibu na kukuangamiza mwili wako"
Na kukufanya ukose tumaini LA mafanikio.
Nikauliza kivipi akajibu kwa mfano.

"MTU mmoja na alikuwa anakunywa soda alinunua kwa fedha yake akanywa akamaliza akaweka chupa chini na kukanyaga wa mtu mwengine akapita kandokando yake akamuliza mbona wakanyaga chupa na soda umenywea humo kwa majivuno akajibu yule MTU wa kwanza hii ni chupa tu"its just an empty bottle".nikamuliza una maana gani na mfano huo.
Akanijibu mwanangu watu hutumia gharama nyingi kuutafuta kuharibu mwili wako kukudanganya, kifedha.
Na akiupata huwa hauna thamani mwili wako na kubaki kama chupa tupu.
Chunga sana mwanangu na usiwe chupa tupu ufike kwenye dirisha LA kutoka.

2.Akili
Akili mwanangu ni sehemu ya kuchunga maana mola wako alikujalia wewe akili mwanadu pamoja na utashi katika viumbe vyote.
Tumia utashi wako na akili yako yote na siku zote tambua wewe ni zaidi ya kila MTU nikakuzaa wewe.

3.NAFSI
mwanangu katika kitu kigumu wakati upo unakuwa nilikuwa nakufundisha kidogo upate kuelewa nafsi yako.
Lakini leo nakwambia mwanangu nafsi INA nyakati nyingi kimjumla naweza nikasema furaha na huzuni.

Furaha
Mwanangu furaha ya nafsi inajitokeza baada ya mafanikio ni furaha ya kweli.
Ila furaha inayotokana na ujinga inafanya nafsi iote tamaa ya upumbavu chunga mwanangu.

*Huzuni
Mwanangu hapo ndipo nilishindwa kukuambia kuwa huzuni ni baada ya nafsi Kupotea na kutaka kushibisha nafsi kwa maovu.
Nafsi INA tabia ya kushiba na kula ila chunga mwanangu ishibishe nafsi kwa yaliyo ya mafanikio.

Kuliko ukashibisha nafsi kwa kufanya starehe za kipumbavu usiwe na tamaa kupita kiasi ifunze nafsi yako kutosheka mwanangu hata kama huna.

BY RUGAIKAMU MUGANDA
 
Hii post ikisalia jukwaa hili sijui
 
Back
Top Bottom