Kuishi kwa kupanga uswahilini ni zaidi ya mafunzo ya kijeshi.Kwa sababu kama unatumia akili yako vizuri utajifunza:-
-kuishi kwa bajeti katika kila kitu chenye kuhitaji gharama,
-kula kwa kiasi,
-kuihimili tamaa,
-kuishi na jamii kulingana na hali zao kiuchumi,kitabia na mazoea yao,
-utajifunza kuongea,kuongeza misamiati mipya hadi tata na lugha mbalimbali,
-ukiwa mpole utajifunza hadi kuzozana na ikibidi kupigana kwa mbinu za ushindi tu,
-utajifunza ubishiubishi na uchonganishi,
-kuishi kiujanjaujuanja na mbinu za hakuna kulala na kadhalika wa kadhalika.
NOTA BENE:Si lazima uyapate yote kwenye upangaji.Unaweza ukawa navyo vyote ila hukuwa umepata uwanja wa kuonesha "vipaji" vyako.Ukiishi kwenye upangaji tena uswazi,tutakujua tu.