Maisha ya Somali ndani ya Tanzania

Maisha ya Somali ndani ya Tanzania

harakat

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Posts
2,887
Reaction score
1,359
Maisha ya Somali ndani ya Tanzania

siku chache zilizopita tumeshuhudia matukio ambayo hayaeleweki kwamba ni Tanzania au Somalia ila nikapata majibu kwamba hayo ni maisha ya Somalia na tunaomba Mungu aepushe maisha ya namna ile kule Somalia wala sio huku Tanzania.

Ni nini kinatokea hapa tanzania sehemu ambayo Tanzania ambacho kinataka kutuunganisha na somalia ni kwa nini tunayaruhusu haya kutokea tena kwa wingi na kwa kasi ya ajabu nikashindwa kuelewa .

watu wanashindwa kuelewa kwamba Damu hulupwa kwa damu na hata ikipita muda mrefu sana bado uzito wa damu husika huwepo tu.

Kuna watu wawili wameuwawa wakati wa harakati za kampeni ya jimbo la kinondoni huyu mmoja ni katibu wa CDM na huyu mwingine ni mwanachuo wa chuo cha usafirishaji mwaka wa kwanza ameuwawa akiwa kwenye daladala akielekea zake kwenye majukumu yake.

Hapa ni uhai umepotea na wala sio kitu kingine uhai huu ni wa garama mno hauwezi kurudishwa na binadamu yeyote .Vyombo vya Dola vimezungumzia suala moja tu la mwanachuo waliomuua na wamekiri kwamba ni bahati mbaya .Kweli inaelezeka ila wanasahau kwamba ni jukumu lao kuhakikisha kwamba suala la ulinzi na usalama wa raia na mali zao upo juu yao na sio tu inapotokea bahati mbaya kama hayo bali hata yale ambayo wanasema tu ni watu wasiojulikana umma unataka majibu tena yaliyosahihi na wala sio ya kubabaisha .

Siasa zetu hazijawahi kuwa na historia ya umwagaji damu kwa kuwa wote ni ndugu moja na katika Nchi hii hapajawahi kuwa na ubaguzi wa kikabila wala kikanda zaidi ya utani ambao huwa unajenga mahusiano na mafungamano yetu katika umoja na mshikamano na wala sio mifarakano.

Kuna baadhi ya nchi ambazo huwa na siasa za umwagaji damu utekaji nyara na mambo mengine ya aina hiyo lakini sio kwa Tanzania na hata kama ni kuzuia maandamno lazima viangaliwe vitu vinavyofanyiwa kazi ,kuna masuala ambayo ni ya kiuhalisia yanaonekana kuwa na mashiko haya lazima yafanyiwe kazi haraka hii ni kuzuia kutokea kwa machafuako au matumizi ya nguvu yasiofaa.

Imetokea mara kwa mara baadhi ya watu kuuwawa na maiti kuokotwa huko koko bichi suala hili halijatolewa ufafanuzi unaoeleweka,

Imetokea kushambuliwa na kujeruhiwa vibaya na silaha kwa Mbunge Lisu na hakuna hata anayeujuza umma juu ya kinachoendea zaidi ya kurushiana shutuma ambazo zinakosa mashiko ,amepotea Benn wa saa nane na hakuna majibu yaliyotolewa mpaka sasa, nashindwa kuelewa je ni Somalia ndani ya Tanzania au ni Tanzania ifananayo na somalia. nawasilisha
 
Back
Top Bottom