Ambiele Kiviele
JF-Expert Member
- Dec 29, 2014
- 15,267
- 29,906
Maisha Matam sana ukikutana na Mtu anaye jua thamani yako
Mume wake hakuwa akimjali, kila siku alikuwa akimsababishia maumivu ya kihisia.
Siku moja mke akamtizama mumewe aliyekuwa akicheza kwa furaha na binti yake mdogo wa miaka minne.
Mke akamuuliza mumuwe: Utafanya nini kama siku moja binti yetu ataolewa na mwanaume atakaemfanya awe analia kila siku na kujuta kuolewa?
Mwanaume kwa kujiamini akajibu:
Nitakula nae sahani moja huyo mwanaume kwa kweli, nitamjeruhi.
Huyu ni binti yangu, damu yangu, ndio kila kitu kwangu!
Huku machozi yakimtoka mke akamwambia mumewe huku amepiga magoti;
hata mimi nina baba yangu anayenipenda, hafurahishwi na haya unayonitendea kila siku!
Kwanini unaniumiza sana? Kwanini hutulii na mimi, nifanye na mimi nifurahie ndoa kuliko kila siku kujuta kwanini niliolewa!
Hii ilimgusa sana mume wake, na akaahidi kubadikika na akamwambia kuwa atakuwa mume bora ambae angetamani hata binti yake atakapokuja kuolewa huyo mume awe kama yeye.
______________________________________
Enyi wanaume
wapendeni wake zenu, tengenezeni ndoa zenu, ndoa yenye furaha na amani ni msingi wa kujenga familia iliyo bora, ambapo kupitia familia hiyo tunaweza kujenga taifa lililo bora kimaadili.
Watoto zenu wanajifunza sana kupitia jinsi mnavyoishi ndani ya nyumba.
Oneshaneni upendo, hii itawapa matumaini watoto zenu juu ya taasisi takatifu ya Ndoa.
Ukibadilika na kuwa mume bora hauwezi pungua nguvu za kiume, ila utakuwa baba unayeheshimika kwa mke na kwa watoto.
N:B Ahsanten kwa kuja