Maisha ya ndoa yangu na changamoto zake

Maisha ya ndoa yangu na changamoto zake

nur

Member
Joined
Mar 28, 2012
Posts
63
Reaction score
11
Namshukuru sana mungu kwa kunipa nafasi ya kuongea nanyi kwa maandishi. Mimi ni mwanaume miaka 33, nina watoto 2, elimu yangu ni chuo.

Mwaka 2004 nilianza kazi kama Mwalimu, mwaka 2005 nikaoa.

Maisha ya ndoa yalikuwa mazuri sana kwani kabla ya kuoana huwa kuna makubaliano mnafanya makubaliano hayo yakifikiwa huboresha ndoa, yasipo fikiwa huleta vidonda na hatimae kuvunjika kabisa, ndoa iliaoza vyema bila shida yoyote. Mimi natokea familia ya kawaida sana ambayo ina watoto 6 baba na mama wakulima tena wakawaida, mpaka namaliza kidato cha nne nilikuwa nadaiwa ada sh 115000 wakati mshahara ulikuwa 62000.

Ilibidi niingie mkopo ili kupata pesa hiyo. ugomvi ulianzia hapo na amani ya ndoa ikaisha. Kwasababu ya mazingira niliendelea kuvumilia baadae nikachoka. kuna mwanaume alikuwa nae kabla ya kuwa na mimi akaendelea nae.

Mwaka 2008 nikaanza kusoma nikapata credit ugomvi ukawa mkubwa kwanini nasoma 2010. Nikaenda chuo akaamua kuondoka na sasa kaolewa na ndoa ina miezi minne.

Karibu kwa ushauri.
 
Huyo mwanamke keshaolewa na wewe umeshajiendeleza!! Sioni ni ushauri gani unahitaji lakini unachotakiwa kujua ni kwamba ukiona mapenzi hayafiki mnapolenga basi ujue mmoja wapo kati yenu hakuwa na mapenzi ya dhati!! Anayekupenda hawezi kukuzuia kusoma maana angechukulia kwamba unamjengea yeye na watoto wenu maisha mazuri.

Kikubwa ni kwamba, jenga maisha yako na wanao ili wasipitie maisha uliyopitia wewe, huyo mwanamke hakufai tenaa!! Kwanza keshaolewa, hupaswi kumuwazia tena mke wa mtu
 
Wanaume tumeumbwa mateso, pole sana
Haina haya ya kuumuza kichwa try to make your own life,.....
 
pole kwanza kwa matatizo hayo.... unatafuta maendeleo mwenzako anataka ubaki kuwa chini....

ushauri ni kuachana nae tu na kuendelea na maisha yako maana huyo aliyekuwa mke wako kashaolewa na mwengine na inamaanisha hana muda wa kujisumbua wa kuwa na wewe au kuwasiliana na wewe.... wewe tengeneza mazingira mazuri ya watoto wako wakue katika maisha mazuri.

kwa sasa kaa chini jiweke sawa kimaendeleo then utafute waubavuni mwako mwengine mwenye hekima na heshima kwako..
 
Open new chapter move on with available opportunities, she wasn't meant to be your life companion. If your heart is still longing for her get ready to receive the unexpected.
 
pole mkuu,hongera kwa uvumilivu na kujituma
 
sijui nmesoma kwa haraka sana au mi ndio sijaelewa
 
Hii aina ya uandishi kwa siku ya leo naiona mara ya 3 sasa as if ni mtu mmoja, sasa na hili swala la watu kuwa na ID 7 napata mashaka
 
hii aina ya uandishi kwa siku ya leo naiona mara ya 3 sasa as if ni mtu mmoja, sasa na hili swala la watu kuwa na id 7 napata mashaka
labda anataka post yake ijae wachangiaji
 
Back
Top Bottom