Mohamed Ismail
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 229
- 250
Baaada ya kupewa taarifa ya kufukuzwa shule ndani ya siku tatu niliishiwa nguvu na niliweza kulia sana kwamba ndoto yangu imeishia hapo. Tulimbembeleza sana yule mwanafunzi atusamehe na tukampa hela ili atusamehe. Kweli kuku mgeni hakosi kamba mguuni na kweli rushwa ni kazi kuimaliza, alichukua hela yetu hivihivi tunamuona. Yule hakuwa hata kiongozi bali alitumia ugeni wetu wa kutojua sheria kwake akaigeuza kuwa fursa. Nakumbuka siku nawasili shuleni kwa mara ya kwanza baba ndio alinipeleka na kuhakikisha nimeandikishwa. Wakati anaondoka aliniachia elfu Ishirini kwangu ilikuwa hela nyingi sana lakini ile anaondoka nikawa nalengwa na machozi kwa mbali kuona baba yangu ananiacha porini. Kumbuka hapo nimebeba hisia mbili moja ya kufurahia kupata hela nyingi huku nikiwa na huzuni ya kuachwa na baba porini. Maisha yakaendelea nikapangwa kuishi bweni la Kawawa. Mwanzoni tuliishi kwa furaha sana kwa sababu wanafunzi wa vidato vya juu walikuwa hawajarudi kutoka likizo. Kizaazaa kilianza baada ya kuwasili wanafunzi wengine wa vidato vya juu. Ilikuwa inaitwa kumkaribisha form one na kumkata mkia. Kulikuwa na adhabu za kila aina mara upige simu chooni, mara uambiwe kuwa lazima usome darasa la nane huwezi kusoma darasa la tisa bila kusoma la nane. Kwangu mimi nilikuwa na mwili mdogo hivyo basi hizo adhabu sikupata na bahati nyingine kuna kaka yangu alikuwa amemaliza pale na wengi walikuwa wanamfahamu. Hivyo basi kwangu ilikuwa ponapona yangu labda kuna adhabu ambazo huwezi kuzikosa za jumlajumla kuna baadhi ya wanafunzi wakorofi walikuwa wanakuja usiku mabwenini wanazima taa na kuanza kupiga fimbo form one wote. Ile hela niliopewa na baba yangu kama pocket money iliisha ndani ya wiki moja, nilikuwa nashindwa kula ugali wa shule hivyo basi ile hela nikawa nanunulia chakula nakunywa juice za yeboyebo mara kwa mara. Kweli fukara hana miiko baada ya kuishiwa ile hela nilianza kula ugali ule ambao niliutupa kwa mara ya kwanza na mpishi akaniambia ipo siku utaukimbilia. Ilikuwa ikigongwa kengele ya chakula nilikuwa nakimbilia ule ugali. Nilizoea maisha ya shule baada ya kipindi fulani kukawa na disko la welcome form one ambapo walikuwa wamekaribishwa Nganza girls. Nilikuwa natamani kuingia lakini nilikuwa naogopa viongozi wa dini yangu maana ilikuwa ukihudhuria disko wanakutenga na ilikuwa inaonekana form one kuhudhuria disko ni utovu wa nidhamu. Nikiwa na baadhi ya rafiki zangu tukawa tunajishauri tuingie au tusiingie lakini bado tukawa tunakosa msimamo wa kulipia. Baadae tukajipa moyo tukasema tutaingia tukiwa kidato cha pili. Siku ya disko wengi wetu ambao hatukuhudhuria tulienda dirishani kuchungulia na hata wale ambao walikuwa wanatumia kivuli cha dini kutoingia na wao tulichungulia wote. Nakumbuka ulipigwa wimbo wa Bizman wa Mademu wa kibongo..... jinsi walivyokuwa wanacheza nilitamani niingie maana kuna watu walikuwa mabingwa wa kushikilia viuno vya watu, bahati mbaya sikuwa na kiingilio na wasichana wote walikuwa wanavaa vizuri wanapendeza hivyo basi tuliokuwa dirishani tukiwachungulia tulifurahisha nafsi zetu sasa sijui wale waliokuwa ndani wanacheza nao ilikuweje.
Maisha yaliendelea na Mlimwengu mimi nikazidi kuzoea shule nikapata marafiki ambao muda wote tulikuwa pamoja kama Andrew, Gahutu, Baraka, Edger, Vance, Godrick na wengineo. Kwa sasahivi Godrick ni marehemu Mwenyezimungu amlaze mahali pema peponi. Tulikuwa tunacheza wote mpira wa miguu baadae tukaacha tukaanza kucheza volleyball. Tukiwa na akili zetu za kitoto tukapanga kwenda shule ya Bwiru girls . Tukaanza safari tukapita geti la kwanza vizuri tukawa tunaelekea kupita geti la pili mara paap ilikuja Land Cruiser watu walishuka na kutuzunguka. Je nini kilitokea baada ya hapo?
Tukiwa tunaenda kutimiza miaka 100 tangu Bwiru Boys ianzishwe. Nitakuwa naelezea matukio niliokutana nayo.
Episode 2.
Stay tuned.
#mlimwengumimi
#bwiruboysalumni
#100yearsAnniversary
Maisha yaliendelea na Mlimwengu mimi nikazidi kuzoea shule nikapata marafiki ambao muda wote tulikuwa pamoja kama Andrew, Gahutu, Baraka, Edger, Vance, Godrick na wengineo. Kwa sasahivi Godrick ni marehemu Mwenyezimungu amlaze mahali pema peponi. Tulikuwa tunacheza wote mpira wa miguu baadae tukaacha tukaanza kucheza volleyball. Tukiwa na akili zetu za kitoto tukapanga kwenda shule ya Bwiru girls . Tukaanza safari tukapita geti la kwanza vizuri tukawa tunaelekea kupita geti la pili mara paap ilikuja Land Cruiser watu walishuka na kutuzunguka. Je nini kilitokea baada ya hapo?
Tukiwa tunaenda kutimiza miaka 100 tangu Bwiru Boys ianzishwe. Nitakuwa naelezea matukio niliokutana nayo.
Episode 2.
Stay tuned.
#mlimwengumimi
#bwiruboysalumni
#100yearsAnniversary