Mohamed Ismail
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 228
- 249
Tukiwa tunaelekea kupita geti la pili ilitokea gari la Landcruiser ambapo walishuka watu wakatuzunguka. Baada ya kutuzunguka tukapeana ishara kwa sura zetu tukawakimbia na kuelekea vichakani. Nadhani ninapozungumzia vichaka wale mliosoma shule za mjini kwenu ni kama hadithi za abunwasi. Bahati mbaya mmoja wetu alikuwa mzito yeye hakukimbia walivyomshika alibishana nao wakaamua kumuachia na inavyoonekana walikuwa ni walimu wa Bwiru Girls na waliamua tu kutuacha kwa kutuona tulikuwa tu watoto. Lakini safari yetu ikawa imefeli tukaamua kurudi shule maana hata tulipokuwa tunaenda tulikuwa hatupajui. Tukarudia maisha yetu ya kila siku kusoma na kucheza pamoja na kujifunza kuogelea ziwani. Wengi wetu tulijua kuogelea mapema kutokana na ile shauku ya kujua tukawa tunashindana na watu ambao wametokea sehemu zenye ukanda wa maji kama wakerewe. Lakini wale usingeweza kushindana nao maana nasikia wanaogelea na mamba eti. Maisha ya shule yalikuwa mazuri sana baada ya kuzoea mazingira na kwa bahati nzuri nilichaguliwa na Headmaster kuwa kamati ya kuokota takataka. Nikiona leo serikali inapingana na matumizi ya plastic wakati headmaster wetu miaka 10 na iliyopita alikuwa kashaanza vita na plastic. Tulichaguliwa tuliokuwa na miili midogo na tukapewa kazi moja ya kudili na mazingira hivyo kazi nyingine za shule kama kulima , kufagia na kuchota maji haikuwa kazi yetu. Lady jay dee anasema siku hazigandi mara paap! tukaenda likizo ya mwezi wa sita. Kipindi kama hicho unakuwa na hamu kweli ya kuonana na wazazi pamoja na ndugu na jamaa uliowaacha sehemu uliyotokea. Kwa bahati mbaya kipindi hicho wenye simu walikuwa wachache hivyo unalipia mia tano kudip namba ya mzazi wako. Tulikuwa tunasema kudip badala ya kubip. Na ukibahatika kuongea na mzazi mnakuwa kwenye foleni kabla ya kumaliza kuongea mwenye simu anakuambia ukate wakati hajapiga yeye. Kweli cha mtu mavi wenye simu waliringa kweli unatamani ununue ya kwako ila ndio huwezi. Andrew akawa anajifariji kuwa baba yake kamuambia akifaulu kidato cha tano naye atamnunulia simu yake. Mambo ya utoto bwana ni raha sana. Basi tukaenda nyumbani na awamu ya pili tukarudi mwezi wa saba. Wengine walikuwa wanajisifia watu wa kuvuta likizo mnafungua shule anazidisha hata mwezi mmoja na nusu hajarudi na kipindi hicho tulikuwa tunaona ujanja kumbe unapitwa na masomo.
Basi maisha yaliendelea na tukawa tayari tumeishazoea wenzangu na mimi hata kwenye debate tulikuwa tunahudhuria kuongea broken zetu English. Kipindi hicho ulikuwa mwaka wa uchaguzi basi aliyekuwa mbunge wa Ilemela alitoa offer ya kulipa muziki wa samira kwa ajili ya disko la shule . Viongozi wa starehe tuliwaita social prefect na kuwa social prefect lazima uwe brothermen na mjanja. Basi kwa wakati huo alikuwa Erasmus na Andrew ambao kwa ujanja wao waliweka kiingilio cha elfu moja. Basi tukawa tumeishapanga na wenzangu kuwa lazima tuingie disko kama shule imeliruhusu kwanini watu wengine watuzuie kwa mitazamo yao ya kiitikadi. Ila tukawa bado tunasitasita. Wale viongozi wa starehe walitutafuta mimi na Andrew wakaanza kutupanga kuwa nyinyi ndio wajanja lazima muingie sisi tukiondoka lazima tuwaachie madaraka. Kwetu sisi kutufuata watu kama wale tuliona sifa kubwa kumbe wao ilikuwa ni akili ya kijasiriamali wanawaza wapate bukubuku zetu za viingilio. Basi tukaweka viapo lazima tuingie disko ambalo walikuwa wanakuja Nganza. Siku ya disko ikawadia kwanza kabla ya disko niliazima kitabu cha form 2 ili nikariri topic kama za logarithms ili nikiingia ndani nikawa nacheza na msichana nimuambie niko form 2 na akiniulizia topic mmefikia wapi nimtajie. Basi uzuri akili yangu ilikuwa fast sana kukariri na bwiru sikuja bahati mbaya topic zote zilikuwa kichwani. Siku yenyewe ikafika kwa shule yetu siku ya disko ni kama sikukuu lazima ununue nguo mpya au uazime. Basi siku hiyo tukavaa tukapendeza basi rafiki zangu wakaja kunifuata bwenini ili tuingie pamoja. Nakumbuka wote walikuwa wamependeza sana ila mimi akili yangu nikawaza nikiingia nao kwa pamoja nitaonekana form one wakati nataka nionekane nipo kidato cha pili. Huku mabwenini watu wanaazimana unyunyu na kwa taarifa tayari coaster kama nne zimefika zimewabeba warembo wa Nganza, basi hapo hapo unaanza kufanya fasta ili uingie. Basi mimi nilijichelewesha maksudi waniache waliniacha ili niongozane na kundi moja walikuwa wanajiita BM, basi na mimi nikaongozana nao huku na memorize topic kichwani. Kwa muonekano naonekana naenda disko ila akili yangu kama naenda kufanya mtihani. Asikudanganye mtu form one ni form one tu nilivyoingia nao nilionekana. Basi kwangu ikawa furaha , utaratibu wa kufungua disko ukafuata. Ufunguzi ulikuwa wa aina yake ambapo mademu watano walivua kiatu kimoja kimoja na kupelekwa katikati ya ukumbi na kisha wavulana wanaokota kiatu na kumfuata mrembo alipo na kumchukua. Baada ya hapo unapigwa wimbo wa blues wanacheza pamoja huku wengine tukiwaangalia na kuwashangilia. Hapo mllimwengu mimi mshamba wa Kamachumu nipo nashangaa tu. Baada ya hapo waliokuwa wasanii wanaimba nyimbo zao. Asikuambie mtu walikuwa hodari sana sijui muziki wao uliishia wapi. Wengi wamebaki kuwa Engineers. Walikuwa ni Diamond wa sasa. Baada ya hapo wote tukaingia katikati na kuanza kucheza, ilikuwa ukicheza na msichana unahakikisha mwenzako anakuona ili baadae upate cha kusimulia. Form one tulikuwa tunaonewa unakuta unacheza na mdada vizuri mtu anakuja anakutoa kwa kikumbo. Kweli ubabe hujaanza leo. Hawahawa ndio wakipewa serikali wanakuwa mafisadi. Wengine walikuwa wanakuja na makopo ya soda tangu mwanzo wa disko hadi mwisho haliishi ili mradi tu aonekane tofauti. Basi disko likaisha tulimaliza wiki mbili tunajadili yaliyotokea huyu kacheza na nani na kama hawakukuona kama umecheza na msichana utazomewa sana.
Maisha yakaendelea ya shuleni kuna siku Rais wa awamu ya tatu alikuwa anakuja kuwaaga Wananchi wa Mwanza kwenye uwanja wa CCM kirumba. Wanafunzi wote wa sekondari ilikuwa ni agizo kwenda kumuaga Rais wetu. Tulienda wote na sherehe za kutoka nje ya shule tulikuwa tunazipenda maana hata vipindi havitakuwepo. Wakati wa kurudi rafiki yangu mmoja aliniambia kuna kitu inabidi tukitumie...nikamuuliza nini akanionyesha bangi mguuni kwake iliyokuwa kwenye soksi. Je mlimwengu anaenda kuvuta bangi?....Je nini kilitokea hapo?
Tukiwa tunaenda kutimiza miaka 100 tangu Bwiru Boys ianzishwe.
Nitakuwa naelezea matukio niliokutana nayo.
Episode 3.
Stay tyuned.
#mlimwengumimi
#bwiruboysalumni
#100yearsAnniversary