Mohamed Ismail
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 228
- 249
Ikasokotwa bonge la bangi kama la Bob Marley baadae ikawashwa, nikasikia mmoja wao anasema kwa sauti kubwa kuwa Mwenge huwa hauruki kijiji. Basi nikajisemea moyoni leo ndio arobaini yangu imefika. Ikafika zamu ya mtu aliyekuwa karibu yangu huku mimi nikitetemeka kwa ndani. Mara aliyekuwa amekabidhiwa ule msokoto akanigusa begani, alivyonigusa nilishtuka sana hadi watu wakagundua kama kuna kitu. Hapo rafiki yangu ametulia ananiangalia kwa chini chini je nitachukua hatua gani?...akaanza kujisemesha huyu miyeyusho huwa ni chizi sana anawazingua tu. Mwanangu ni chizi sana.
Kama unavyojua akili za bangi wote wakaanza kucheka kwa nguvu kama kitu kikubwa, hapo na mimi baada ya kuona wakicheka nikapata nguvu kidogo na mimi nikaanza kucheka huku nimeshika ule msokoto wa bangi.
Baada ya kucheka nikawatungia story hapo hapo huku nikiwa naongea kama mtu ambaye bangi imemkolea. Story yangu ikawa kama hivi....
Jamaa alivyonishika begani kanikumbusha mbali sana enzi hizo nikiwa darasa la tatu. Siku moja tulikuwa kichakani tunavuta bangi basi mwenzetu mmoja akawa amepuliza pafu kama mbili. Baada ya bangi kumkolea alinipiga bonge la bao mgongoni huku akipaza sauti kwa kupiga kelele kuwa anataka mtu wa kujitolea wa kumtahiri... huku wengine tukawa tunacheka basi jamaa akaona isiwe issue alivua akatoa dudu lake nje na kutoa kiwembe cha kuchongea penseli kuwa anataka mtu wa kutahiri la sivyo atajitahiri mwenyewe.
Basi na mimi jamaa alivyonigusa nikapata flashback ya miaka hiyo ndio maana nikashtuka na kucheka sana. Baada ya kuwapa simulizi hiyo acha wote waanze kucheka na wengine wadondoke hadi chini. Hivyo basi nikawa nimewanyima nafasi ya kunizingatia kama bangi navuta au sivuti. Nikampasia mwenzangu huku tukiendelea kupiga story za hapo na pale.
Story za bangi bana nakumbuka mmoja alikuwa kidato cha sita kwa wakati huo akawa anasema yeye akipata mkopo wa chuo kikuu kitu cha kwanza lazima anunue bastola. Huwa nikikumbuka najua kweli bangi siyo chai ndio maana wahenga wakasema bangi nibangue.
Tulivyokuwa tukirudi shule rafiki yangu akaniambia umenishinda tabia kweli nimeamini huwezi kuvuta. Maana hiki kijiwe hakuna mtu ambaye alifika pale akakosa kuvuta hata mimi ndio sehemu niliyojifunzia kuvuta. Mimi nikamuambia tu kuwa akili yangu hainitumi kuvuta bangi ndio maana sipo tayari kuvuta . Wewe kuwa na amani vuta kimpango wako mimi siwezi na akili yangu ni hii hii. Tukabadilisha story huku tukikazana kuwahi jioni muda wa chakula na siku hiyo ilikuwa Ijumaa ambayo ni siku ya kula nyama. Na nyama ilikuwa mara moja kwa wiki hivyo tulijitahidi kurefusha tambo zetu ili tuwahi saa 12 tusije tukakosa nyama. Maana siku ya nyama ilikuwa vurugu mechi watu lazima wagombane kwenye mstari na ukichelewa lazima uambulie mifupa au mchuzi na mchuzi wenyewe mweupe unaona maganda ya nyanya yanaelea tu.
Shule tulizidi kuizoea na tukawa ndio tupo mwishoni kumaliza form one ili mwakani tuingie kidato cha pili. Tukajiandaa na mitihani ya kufunga mwaka. Na mimi nilikuwa ni aina ya watu ambao kusoma mpaka kesho iwe mtihani sikuwa na desturi ya kusoma siku ambazo siyo za mitihani hivyo prepo kwangu ilikuwa hadithi. Na sisi ilikuwa kampeni yetu kama siafu kufuatana tukimaliza kula chakula tunaenda juu ya mawe tutataniana hadi saa sita usiku hapo ndio kila mtu anaenda kulala kitandani kwake. Wanafunzi wenzetu walikuwa wanasema hawa waacheni wamekuja kukua. Tulikuwa tunaonekana wadogo kwa umri lakini udogo wetu ulikuwa ni maumbo tu maana tulikuwa na akili ambazo usingeweza kutudhania.
Kipindi cha kukaribia kufunga shule kulikuwa na tabia ya wizi wa nguo na vitu. Kuna baadhi ya wanafunzi walikuwa wanasubiri muda wa kufunga wanaiba nguo za wenzao ili wakirudi nyumbani kwao wakazivae na wengine walikuwa wanauza ili wapate hela. Shule ilifuga kila aina ya watu. Kuna watu walikuwa wana funguo ambazo ni kama master key kila kufuli wanafungua. Kumbuka shule yetu ya ufundi wengine walikuwa wanachonga mashoka kwa ajili ya kuvunja matranka ya watu. Ambao tulikuwa na ndugu karibu na shule ikikaribia kipindi cha kufunga shule unaanza kuhamisha nguo zako. Maana wengine walikuwa kama mateja hata boxer na chupi wanakuibia. Lakini ilikuwa ukikutwa kipigo unachokipata kilikuwa cha zaidi ya Kamanda Mroto cha Mbwa koko....lakini bado haikusaidia kukomesha tabia ya wizi wengine walikuwa wanashirikiana na wanakijiji katika kuiba.
Basi tulifanya mitihani yetu salama na tukafunga shule na kila mtu alikuwa anafurahia kurudi nyumbani. Ambao walikuwa wanatumia usafiri wa treni walikuwa wengi wao wanakata tiketi wakisikilizia tarehe za wanafunzi wengine wa shule za wasichana wanaondoka lini. Hivyo basi kwenye treni ilikuwa ni bonge la adventure maana mnawekwa kwenye behewa la wanafunzi shule kibao. Hii ilikuwa na raha yake. Wenzangu na mimi tuliokuwa tumetokea Bukoba tulikuwa tunasafiri kwa kutumia meli za Mv Victoria au Mv Serengeti. Ilikuwa kupanda meli ni kuanzia saa moja jioni. Basi humo kwenye meli ilikuwa raha sana mnakutana na wanafunzi mbalimbali kutoka shule tofauti na waliokuwa wepesi wa kutongoza ndani ya usiku huo mmoja wa safari kashapata girlfriend. Wengine wanakunywa pombe wengine wanavuta sigara hapo hapo kuna vikundi vikundi vya wanafunzi. Na asilimia kubwa mkiwa wanafunzi hata kama mmetoka shule tofauti lazima muelewane na muanze kusimuliana habari za shule na kila mtu anajitahidi kusimulia uzuri wa shule yake. Safari zake zilikuwa na raha yake iwe ni kwenda nyumbani au kurudi shule. Rafiki yangu Disa najua hawezi kusahau safari yake ya kwenye meli maana ndio alimpata mlimbwende wake wa kwanza.
Basi kipindi hicho cha likizo tulikuwa tunawasiliana kwa email na rafiki zangu. Maana shule yetu tulipata msaada wa huduma ya computer na internet ambao tulikuwa interest tulifungua email kwa wakati huo na tukawa tunatumia kuchat. Basi na mimi nyumbani kwetu huduma ya internet ilikuwa inapatikana hospitali ya Ndolage. Nikikutana na mtu namuambia naenda internet kucheki email mtu anakushangaa anakuona unajua vitu vingi basi na sisi ambao tulikuwa tunachaguliwa shule za kwenda mbali vitu kama hivyo ndio vilikuwa vinawahamasisha watu wasome kwa bidii na wafaulu ili na wao wajue mambo ya Email. Nakumbuka kwa kipindi hicho nilikuwa naenda kucheki kama nimetumiwa message na Andrew, Gahutu, Vance na tulikuwa tunaenjoy sana. Na mzee wangu nilikuwa nikitaka kumuomba hela nimuambia naenda internet cafe maana alijua huko ninajifunza vitu vingi.
Kipindi cha likizo nilikitumia kusoma tuition na uzuri nilikuwa na speed kubwa ya kujifunza likizo ya mwezi mmoja nikijiongezea na mwezi mwingine basi narudi nimemaliza topic zote za kidato ambacho naingia. Likizo iliisha basi tukarudi kidato cha pili. Wengi wetu walikuwa wanawahi kwa ajili ya kuwapokea form one. Maana shule ukisikia kutesa form one mara nyingi huwa ni form Two ambao huwa wanalipiza kisasi kwa kuwa na wao wameteswa. Mimi sikuwa miongoni mwa kupenda kutesa watu kwanza nguvu sikuwa nazo na wala sikutaka kutumika kama chambo kwa form one. Maana walikuwa wana tabia madarasa ya juu kumtumia mtu mdogo na ukiwa form one si utadharau ukiona siyo sawa mnalingana sasa kinachofuatia watakufuata wote na kukupiga. Mimi sikuwa mtu wa namna hiyo.
Kuna siku nilikuwa bwenini form one mmoja alichelewa nikawa nimempokea. Wakati wa kumpokea nikamuambia hapa kuna watu wana majini basi rafiki yangu Edger akaja akawa anapiga makelele nikamnongoneza yule form one kuwa huyu jamaa ana majini na huwa anaishi ziwani. Basi yule form one akaamini alikuwa akimuona Edger anakimbia basi mimi roho yangu nafurahi. Form one ni form one tu alikuja kuzoea baada ya miezi miwili.
Siku ya Jumatatu ilikuwa ni master parade ambapo mnakaguliwa kila kitu lazima uwe na tai, uniform safi na umevaa soksi. Basi mimi na wenzangu tulikuwa tunatega wanatufungia bwenini. Tukiwa bwenini wenzetu wako parade tukawa tunapiga kelele tunajisahau. Nikawapa wazo wenzangu kwamba hapa akija mwalimu tunakimbilia kwenye ile dari ya juu hawezi kujua. Mara paap! Mwalimu akaja akasikia sauti zetu alivyotuita wote tukakimbilia kwenye dari wenzangu wakawahi wakajificha kwenye dari. Mimi fasta nikakimbilia uvunguni. Mwalimu akaja na viongozi kufanya msako wakaanzia mwanzo wa bweni hadi mwisho hawakuona mtu. Ila mwalimu alikuwa katuona kupitia dirishani akawa anawaambia wenzake kuwa hawa watu wamo humuhumu hawajaenda popote. Basi walimu wakaanza tena msako kitanda kimoja baada ya kingine hapo mimi nilikuwa chini ya kitanda nimejibanza kama mjusi. Mara mwalimu akawa ananipiga na kiboko mgongoni kuwa ameniona ananiambia nitoke. Kumbe alikua hajaniona basi woga wangu nikatoka nilipigwa hapo fimbo kama mvua. Nikisikia serikali inazuia matumizi ya fimbo kwa shule zetu hizi sijui. Ila baada ya kunikamata mimi, Mwalimu akawa bado ana hamu ya kuwapata wengine. Nikapigwa fimbo nitaje wenzangu walipo nikamuambia mwalimu walikimbia sijui wameenda wapi.
Mwalimu akatoa maagizo kuwa mlango ufungwe warudi tena baadae kufanya ukaguzi. Basi Andrew na Baraka walikuwa darini muda wote. Andrew alikuwa na umbo dogo alipita juu ya dari akadondokea nje ya bweni na mwili wote alikuwa kajaa vumbi usingeweza kugundua sura yake kwa alivyokuwa alipendeza kuwa mfano wa shetani.
Baraka naye alikuwa ana mwili mkubwa alipojaribu kutoka alinasa kwenye dari huku kichwa na kifua viko juu huku miguu imeelea chini. Hawezi kushuka wala kupanda juu.
Na huku anasikia sauti ya mwalimu anakuja...
Je nini kilitokea? Na mlimwengu nitapewa adhabu gani? Je Andrew ndio kaepuka huo msala?
Tukiwa tunaenda kutimiza miaka 100 tangu Bwiru Boys ianzishwe.
Nitakuwa naeleza matukio niliokutana nayo shule.
Episode 6
Stay tuned
#BwiruboysAlumni
#MlimwenguMimi
#100yearsAnniversary