Maisha ya 'kitamthilia' yamemuharibia!

Maisha ya 'kitamthilia' yamemuharibia!

Tatizo wanawake siku hzi tunadanganyana sana kwenye hizi semina hizi
Et usifanye majukumu ya mke kwa mtu ambaye sio mumeo
Sasa atajuaje km unafaa kuwa mke km hujiongezi!
Kama ipo ipo tu
Kuna walosugua marumaru hawajaolewa
Na wapo waliofika wakanyoosha miguu wakaolewa
Kwanza mtu km unampenda kila unachofanya unafanya tu kwa mapenzi bila kuhesabu km mke au sio mke
Mnakula wote hata kupika hupiki???
Mnalala wote hata shuka ulizochafua hufui??
Mnakaa wote humo ndani ukienda...unakaaje sehemu chafu??.aagh jaman

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo vipi ladies and gentlemen. Hope mko poa, me too. Moja kwa moja kwenye mada.

Nina bro wangu kipindi cha nyuma kuna mahali alikuwa anapenda kukaa na kunywa bia mbili tatu kila akitoka kazini mida ya jioni. Hapo maeneo "ki'frame" tu, kinamilikiwa na maza ambae ni mtumishi wa umma aliyeamua kujiongeza. Sasa huyu maza ana mabinti wawili, mmoja yupo alikuwa anasoma chuo India na mwingine yupo form four boarding school flani hapa bongo!

Sasa basi, kipindi cha likizo yule binti wa form four huwa anakuwaga na mama yake pale pub au siku nyingine anakuwaga mwenyewe bila ya maza. Bro yeye kama kawaida kila jioni lazima apitie pale ikapelekea kuzoeana sana na yule binti. Binti alikuwa mrembo wa sura japo alikuwa mwembamba but kashepu kapo.

Kweli bwana.. bro wakawa wamezoeana kupelekea kutongozana na kukubaliana kuwa pamoja but mpaka amalize form six. Kweli bro akawa ndio kama mchumba wake maza nae akajua, dada mtu nae akajua maisha yakaendelea mpaka dogo akamaliza six. Bahati nzuri akafaulu vizuri tu na kudahiliwa chuo kimoja maarufu sana hapa Dar.

Basi maisha yakaendelea.. nakumbuka mara ya kwanza kupiga shoo ni binti alivyokuwa mwaka wa pili. Then maisha yakaenda vizuri mizawadi ya birthday kama yote. Bro alikuwa anasubiri mtoto amalize chuo afanye michakato ya engagement then mambo mengine yafuate.

Binti akamaliza chuo vizuri na kama tunavyojua kuanzia 2015 ukimaliza chuo huna guarantee ya kupata kazi. Basi ndio hivyo dogo alimaliza mwaka 2018 yupo home mpaka leo. Mahusiano yanaendelea japo kuna kutoelewana hapa na pale kama tunavyojua wanaadamu sio kila siku tutakubaliana vitu lazima tupishane kidogo.

Wameendelea fresh kwenye mahusiano ikafika kipindi mpaka kwenye harusi wanaenda wote yaani mambo yalikuwa ni fire. Chakushangaza ilivyoingia 2020, bro ananiambia me huyu demu simtaki. Nikamuuliza ishu ni nini? Akasema sio "wife material". Mimi nikawa namsisitiziza asimfanyie hivyo kwa sababu wametoka mbali kama vipi amwambie tu vitu asivyovitaka ili abadilike. Kweli wakaendelea but mshikaji moyo wake haupo tena kwa yule binti.

Sasa juzi kati ndio nilipata muda wa kuongea na bro kwa muda mrefu, akaniambia kuwa yule binti yeye interest zake ni kwenda kwenye birthday parties tu. Mara kwenda club na rafiki zake, mara kwenda beach. Akienda geto kwa jamaa hafanyi chochote hata kukunja nguo hawezi. Akiwa home kwao yeye ni kulala tu; hafanyi chochote.

Ananiambia kuna siku alienda geto kukawa kuna nguno kwenye sofa za kukunja, bro akamuomba amsaidie kugunga vigungo then yeye azikunje, binti akasema nimechoka zangu zenyewe ananikunjiaga mama. Jamaa anasema binti hajawahi hata kufagia au hata kufuta vumbi akienda home kwa mshkaji.

Anasema kuna siku alienda kwa kina binti, akamkuta dada yake na binti yule aliyekuwa anasoma India by that time alikuwa amesharudi. Akamkuta anafua. Akasema hilo beseni ambalo alikuwa anafulia mtoto wa kike huyo lili kuwa chafu utasema ni la madogo wa boys boarding school.

Kwa kifupi bro amesema wale mabinti walikosa malezi bora kutoka kwa maza wao so wamekuwa mabinti wavivu na kupelekea kukosa sifa za kuwa wife material. So akaachana nae. Maza akawa anampigia simu hakupokea mpaka sasa hivi amawablock familia nzima. Na pale pub maza alishapafunga kitambo sana. So kila mtu na maisha yake.

Sasa juzi kati mwezi wa pili bro alikutana na manzi ambae kipindi cha nyuma walikuwa wanafanya kazi pamoja. Huyo manzi alikuwa secretary kwenye hiyo kampuni. Na kipindi hicho hakuwahi kumtongoza, walikuwa kawaida tu salamu za hapa na pale. Basi walivyokutana wakabadilishana namba then wakaanza kuchat na kupelekea kutongozana!

Kweli bwana... chemistry ikakubali equations zikareact na kubalance on the spot. Amesema yaani huyo binti ni balaa. Advertise siku ya kwanza kuja geto alianza na usafi kwanza na kufua mapazia kila kitu. Na kupika juu. Bro anasema anasubiri korona iishe afanye mambo.

Kwa hiyo ndio hivyo. Mabinti mjifunze kuwajibika na kufanya mambo mazuri yanayotakiwa na jamii. Sio kuishi kama upo bongo movie. Utazeekea nyumbani. Au utakuwa unapigwa na kuachwa.

Maisha ya tamthilia sio mazuri.
"I can't do your laundry I ain't your mama"...Jlo kawadanganya wacha wazeekee nyumbani
 
Ukiona watoto wa kike wapo hvyp ujue ht mama yao enzi zake alikuwa hvyo. Hiko kibinti bado hakijajitambua na inaonekana ht umri wake hajapevuka enough kuwa s'bodys wife. Amuache aendelee kula usichana, yeye aoe hiko kifaa kingne chenye nia ya kuolewa
Mama yao ndio kachangia watoto kuwa hivyo. Nakubaliana na wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alikuwa anasoma boarding. Hakuwahi kupata muda wa kumchunguza hivyo vitu kwa muda huo. Kumbuka mwanafunzi atakujaje geto!!!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Okey, tutoe miaka ya sekondari. Amegraduate 2018 hii ina maana ameanza chuo 2015, hebu tuanzie 2016 walipoanza kukulana....kwa hiyo kutoka 2016 amekuja kugundua 2020 kuwa yuko hivyo?? Hata hivyo siamini eti unaweza usijue tabia ya mpenzi wako mnayewasiliana kwa karibu hadi awe amekuja nyumbani
 
Ukiona watoto wa kike wapo hvyp ujue ht mama yao enzi zake alikuwa hvyo. Hiko kibinti bado hakijajitambua na inaonekana ht umri wake hajapevuka enough kuwa s'bodys wife. Amuache aendelee kula usichana, yeye aoe hiko kifaa kingne chenye nia ya kuolewa
It's not always the case, wazazi wengine wanahisi kuwadekeza watoto ndio malezi ya kisasa
 
Tatizo wanawake siku hzi tunadanganyana sana kwenye hizi semina hizi
Et usifanye majukumu ya mke kwa mtu ambaye sio mumeo
Sasa atajuaje km unafaa kuwa mke km hujiongezi!
Kama ipo ipo tu
Kuna walosugua marumaru hawajaolewa
Na wapo waliofika wakanyoosha miguu wakaolewa
Kwanza mtu km unampenda kila unachofanya unafanya tu kwa mapenzi bila kuhesabu km mke au sio mke
Mnakula wote hata kupika hupiki???
Mnalala wote hata shuka ulizochafua hufui??
Mnakaa wote humo ndani ukienda...unakaaje sehemu chafu??.aagh jaman

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeongea mawazo yangu kabisaaa...eti mtu anasema siwezi kufua nguo za boyfriend kwani mume wangu huyo? My dear mbona chupi unavua kwani mumeo huyo? Fanya kwa mapenzi tu sio kwa lengo la kuonekana waifu matirio maana hapo napo ukiachwa utaumia ulivyokuwa unainamisha mgongo. Unafanya kwaajili yako mwenyewe usikae sehemu chafu au kuwa na mtu mchafu.
 
Ukiona watoto wa kike wapo hvyp ujue ht mama yao enzi zake alikuwa hvyo. Hiko kibinti bado hakijajitambua na inaonekana ht umri wake hajapevuka enough kuwa s'bodys wife. Amuache aendelee kula usichana, yeye aoe hiko kifaa kingne chenye nia ya kuolewa
Mis powers hata mashoga mnachangia sana kutowapa mafunzo marafiki zenu juu ya uhalisia wa maisha, nyinyi mnapokuwa pamoja mna discuss fashion na celebrities tu, hii ni Africa mwanamke bila ya kuwajibika kwa mume kwa mambo madogo madogo haitokuwa rahisi kuolewa. Mwezi wa November mwaka Jana rafiki yangu alipokea posa kwa mdogo wake, December ikawa harusi, tarehe 18 mwezi huu Demu karudi kwao na talaka, kuulizwa nini kasema nimeachwa sijui kupika Jambo ambalo rafiki yangu alilipigia kelele sana kwa mama yake dogo afundishwe kupika lakini hawakutilia umuhimu. Mwanaume anahangaika kutafuta mazaga, anarudi home anakuta umepika mataptap, aisee!!! Mambo hayo mtufanyie kama sisi twenye uvumilivu ila sio wengine asee
 
Chukueni Tahadhari.
Tumieni sabuni na SATANAIZ!
IMG_20200426_191745.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom