Ni shule gani mkuu?Nakumbuka mwl m1 alituambiaga definition ya maisha ya boarding:
Maisha ya boarding ni mjumuiko na mkusanyiko wa shida na tabu na chembechembe ndogo sana za raha.
R.I.P mwl mtanzania ( hiyo ndio nickname yake )
St Cuba Kaka's mkuu hahaha...Ni shule gani mkuu?
Nimepita pale 2012 nilikua Ruhinda bweni la mwisho kabisa kuelekea pyramid....asee asikwambie mtu ile n JKT mchaka mchaka kwenda bugashani,BLTC bado issue ya kulima,ukienda kuangalia mpira nje ya shule jiandae kula nyama zilizoganda...Nyakato mamaMaisha ya "nyakato secondary", bukoba ni moja kati ya naisha ya boarding ambayo sitokuja kuyasahau. Namukumbuka yule teacher aliyekuwa akisema hii ni JKT siteti namba moja duh!
Nimepita pale 2012 nilikua Ruhinda bweni la mwisho kabisa.
mkuu na Mimi nilikuwa naishi RUHINDA. Siku hizi nyakato imebadilika sana.
iHawalimi tena na kupangiwa zamu za kuhudumia banda la nguruwe?? Kwenda ulokoni na kuangalia mpira kwa mzee katemana....Kuna kipind linapita gharika la ukaguzi wa simu asee hata kama una SIM card inakula kwako
Umenikumbusha nilisoma Shule moja ya jeshi baada ya brother kuondoka niliitwa nikawa natembea tu,daah nilikula buti kadhaa na mp,kufika bwenini wakaja form two na 3 kupokonya vitu nilikuwa na sukari na mikate,kesho yake baada ya assemble,gwaride namm nilichelewa kidogo wenzangu walikuwa wanajua baadhi ya matendo,nilikula buti na wale makoplo sitasahau kabisa,ndani ya siku moja sina hamu na ilikuwa no way uwasiliane home hadi uende kwenye call box za ttcl.Walikimbia wengi sana ile form one but nilijikuta nimekuwa sugu Staki tena kuhama na ndo Shule iliyonitoaWakuu wazima,
Maisha yanatembea kwa spidi sana, enzi hizo boarding schools zilikuwa ni sehemu ya mafunzo ya maisha mtaani, yaani ukipiga miaka minne boarding basi tayari una cheti cha kupambana popote dunian na kukabili maisha yoyote, ilikuwa si mchezo, jinsi ya kupata msosi ni noma, ukienda kwenye kulala nako si mchezo, walimu sasa wa shule za boarding enzi hizo walikuwa wanajua kulea na kunyoosha hasa, hata uwe mtukutu vipi ukipelekwa boarding unanyooka, wazazi wenye watoto watukutu boarding ndo ilikuwa tegemeo Lao.
Nakumbuka form one enzi zile ilibaki kidogo tu nikusanye virago nirudi home maana ni km Guantanamo hivi shuruba zake, kila kitu tabu tupu yaani..
Tukumbushane visa ulivyofanyiwa au kuwafanyia wenzako enzi ukiwa boarding .
Twende pamoja tukikumbushana lile life la jeshi ukiwa boarding.