Maisha ya Benaco na Rusumo pale Ngara

Humble African

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
4,779
14,377
Habari waungwana!?

Ningependa kujua hali ya maisha kwa namna ya utafutaji katika maeneo haya ya mpakani mwa Tanzania. Mzunguko wa kiuchumi ukoje? Gharama za maisha zikoje!? Panafaa kwa kuanzia maisha ya utafutaji? Vipi kuhusu upatikanaji wa vyakula!? Biashara ipi inalipa kwa kutoa pale na kupeleka Rwanda!?

Kwa wale wote waliowahi kupita au kuishi maeneo haya ya mpakani tupeni uzoefu wenu juu ya maisha na utafutaji wa riziki kwa ujumla!?

Karibuni!
 
mtafute mama maarufu pale anaitwa mama shilingi,kuna ukimwi balb sababu ya muingiliano,dunia nzima inapajua benaco,paliwahi kuwa na kambi kubwa ya wakimbizi kuliko zote duniani mwaka 1994 wakati wa genocide ya rwanda,hapo ni karibu na rwanda sio burundi
 
ni maeneo ambayo ikifika sa mbili usiku ni kama sa nane usiku, gesti ni chafu na magodoro yaliyochakaa, kuna ukimwi glade A. unapokuwa maeneo hayo kama mgen utajulikana fasta, kwa mavazi na lugha, chakula kikubwa ni ndizi. lugha ya hapo zinaingiliana na nchi jirani, mvua ni za kutosha, sifaham mengi mazuri ya hapo bali nafahamu hayo tu
 
Mkuu Benaco ni pazuri kwa Biashara, hasa biashara za vinywaji kama Bar maana wateja wengi ni wasafiri ( ma Dreva) maisha ya pale ni ya kawaida mkuu na hapajachanganya sana ki vile ni vi center vinavyokua taratibu.

Habari waungwana!?

Ningependa kujua hali ya maisha kwa namna ya utafutaji katika maeneo haya ya mpakani mwa Tanzania. Mzunguko wa kiuchumi ukoje? Gharama za maisha zikoje!? Panafaa kwa kuanzia maisha ya utafutaji? Vipi kuhusu upatikanaji wa vyakula!? Biashara ipi inalipa kwa kutoa pale na kupeleka Rwanda!?

Kwa wale wote waliowahi kupita au kuishi maeneo haya ya mpakani tupeni uzoefu wenu juu ya maisha na utafutaji wa riziki kwa ujumla!?

Karibuni!
 
Mkuu Benaco ni pazuri kwa Biashara, hasa biashara za vinywaji kama Bar maana wateja wengi ni wasafiri ( ma Dreva) maisha ya pale ni ya kawaida mkuu na hapajachanganya sana ki vile ni vi center vinavyokua taratibu.
Kwa hiyo panaweza kuwa sio sehemu salama kuanzia maisha ya biashara kwa mtaji wa tshs mil 17!? Maana kama uchumi wa eneo unaendeshwa na walevi ni hatari sasa!? Yaani uchumi haujapanuka kihivyo?
 
Mkuu....pale hali ya hewa ni nzuri kwa mwaka mzima......afu ipo karibu na mistu minene so kilimo pale ndo pakeeee
Kuna jamaa hapo juu anasema eneo linaendeshwa na madereva wa malori walevi! Je kwa hiki kilimo unaweza kutokamo vipi kwa mtaji wa almost tshs mil 17 hivi?
 
Benaco ni kajimji kadogo kwa sasa ilikuwa kambi kubwa miaka ya 1994 ya wakimbizi toka Rwanda

Ni njia panda ya kwenda Karangwe kupitia pori la kimisi kutoka njia kuu ya kutoka zero zero ambyo ni njia panda ya kwenda Ngara to mpakani Burundi Kobelo.

Kutoka Benaco mpaka Rusumo mpakani na Rwanda ni 26 to 30km hivi.

Kuna kituo cha Polisi hapo Benaco ila Biashara si kubwa kwa sasa baada ya kambi za Lukole A na B kufungwa za wakimbizi wa kutoka Burundi na baadhi ya Rwanda.

Kilimo kinafaa sana hapo Benaco na hata ufugaji ila usalama ni muhimu sana kwani kuna matukio ya uvamizi wa hapa na pale kutokana na miingiliano ya watu.
 
ni maeneo ambayo ikifika sa mbili usiku ni kama sa nane usiku, gesti ni chafu na magodoro yaliyochakaa, kuna ukimwi glade A. unapokuwa maeneo hayo kama mgen utajulikana fasta, kwa mavazi na lugha, chakula kikubwa ni ndizi. lugha ya hapo zinaingiliana na nchi jirani, mvua ni za kutosha, sifaham mengi mazuri ya hapo bali nafahamu hayo tu
Baridi kama kwenye jokofu
 
Kuna jamaa hapo juu anasema eneo linaendeshwa na madereva wa malori walevi! Je kwa hiki kilimo unaweza kutokamo vipi kwa mtaji wa almost tshs mil 17 hivi?
Ukitaka kuwekeza kwenye kilimo mkuu kwa mtaji Wa 17 M , ni bora ukasogea Wilaya ya Karagwe au Kyerwa, maana Wilaya hizo ni mhimu kwa mazao ya biashara kama Maharage, viazi , mahindi hata mtama pia, pia kama unamalengo ya kuhamia moja kwa moja unaanzisha na kilimo cha Kahawa na migomba, but kwa Benaco kujikita kwenye kilimo sana naona hapafai, hapo kwa biashara za Bar utaweza kutokana namuingiliano Wa wanyarwanda na Wa Tz,
 
Kwa hiyo panaweza kuwa sio sehemu salama kuanzia maisha ya biashara kwa mtaji wa tshs mil 17!? Maana kama uchumi wa eneo unaendeshwa na walevi ni hatari sasa!? Yaani uchumi haujapanuka kihivyo?[/QUOTE

Pale sana biashara kuu kwa MTU Wa kuja ni bar tu ndiyo inaweza ikakusogeza au ujenge Guest house , ila kwa kujikita kwenye kilimo bora usogee Karagwe au Kyerwa ni Wilaya ambazo zimechangaka sana ki biashara hasa Kahawa, mahindi, maharage, viazi , etc.
 
Ukitaka kuwekeza kwenye kilimo mkuu kwa mtaji Wa 17 M , ni bora ukasogea Wilaya ya Karagwe au Kyerwa, maana Wilaya hizo ni mhimu kwa mazao ya biashara kama Maharage, viazi , mahindi hata mtama pia, pia kama unamalengo ya kuhamia moja kwa moja unaanzisha na kilimo cha Kahawa na migomba, but kwa Benaco kujikita kwenye kilimo sana naona hapafai, hapo kwa biashara za Bar utaweza kutokana namuingiliano Wa wanyarwanda na Wa Tz,
Nashukuru kwa ufafanuzi mkuu! Nilikuwa nafikiria juu ya kuishi na kuwekeza haka kapesa kangu Benaco lakini umechange kabisa mindset yangu na karagwe nilikuwa sina habari napo sana ila kwa sasa nitapazingatia na kupatafiti zaidi.

Ila kwa mkoa wa Ngara wapi ni sehemu nzuri ya kwenda kufanya biashara ya kilimo! Na pia nini ni bora kulima au kununua mazao toka shambani kwa mkulima?
 
mimi nimezurura sana ukanda huo,achana na huo mpango nenda karagwe kama jamaa hapo juu alivyoshauri,kwj mil 17 ndani ya miaka michache utakuwa mbali,kwanza huko benaco na rusumo mzunguko mdogo na ni maporini,risasi nje nje,ukimwi live,hata utamaduni wao ni wa kigeni,burundi na rwanda
 
Shukrani mkuu kwa uchambuzi jadidi huu, nimezingatia ushauri wenu na kwa sasa nimeanza kuitizama karagwe zaidi kuliko benaco na rusumo.
 
Nashukuru kwa ufafanuzi mkuu! Nilikuwa nafikiria juu ya kuishi na kuwekeza haka kapesa kangu Benaco lakini umechange kabisa mindset yangu na karagwe nilikuwa sina habari napo sana ila kwa sasa nitapazingatia na kupatafiti zaidi.

Ila kwa mkoa wa Ngara wapi ni sehemu nzuri ya kwenda kufanya biashara ya kilimo! Na pia nini ni bora kulima au kununua mazao toka shambani kwa mkulima?
Ni mkoa Wa kagera mkuu, sehemu nzuri ya kufanya biashara ni Wilaya ya Karagwe na Kyerwa ,kwa mkoa huu ni Wilaya mhimu sana maana kuna misimu 3 , kuna msimu Wa Kahawa ambao huanza mwezi Wa 6 hadi Wa 9 , na unachanganya sana kwa mtaji wako huo unatosha sana kuanza angalau na Tani 10 za Kahawa unakuwa unaizungusha kwa muda Wa miezi mitatu unaweza ukasema ulichelewa kuanza maana inalipa, baada ya hapo kuna msimu Wa maharage mwezi Wa 9 hadi 11, after that kuna Kahawa awamu ya Pili ambayo huwa ni chache hiyo inaenda kuanzia Wa 12 hadi Wa kwanza, unatulia kidogo , mwezi Wa Tano na sita maharage yapo , yakiisha unaunga Kahawa, hiyo ndo hali halisi ya kyerwa na Karagwe boc
 
Back
Top Bottom