Maisha ya advance tabu

Maisha ya advance tabu

kwa kukusaidia uza hiyo smartphone kisha soma kama unafanya pepa kesho hapo utatoka maana hamna namna
 
Pole sana, ufumbuzi wa tatizo lako ni huu. Ukiona mambo hayapandi tafuta wanaoweza wafundishe baadhi ya topics, unaweza watafuta wenzako hata wanne, kila mmoja akufundishe topic tofauti, baada ya mezi kadhaa utakuta umemsliza topic nne kwa wakati mmoja, pia upende kusoma bila kukata tamaa ukikwama mahali uliza usikae kimya, ukienda likizo muda wote tumia kwenda tuition cover topics nyingi utakavyoweza, ili ukienda shule uwe unazipitia ili zikae kichwani, muda utakuwa nao kwakuwa shule za serikali muda wa kujisomea upo sana. Kingine usimsahau Mungu mtegemee kabidhi masomo yako kwa Mungu kila wakati, usisubiri wakati wa mitihani ndo umkumbuke Mungu. Jiamini utafanikiwa. Ni maombi yangu Mungu akufanikishe ufaulu vizuri na chuo kikuu uende.
 
Relax, concentrate kwenye masomo weka bidii zako zote wewe kama wewe, shuleni usiangalie nani anasomaje nani ana kesha darasani hivo vitu vinavunja moyo kila mtu ana akili zake na namna yake ya kucatch vitu kama akili yako ni ya kusoma umerelax soma hivo kama akili yako inahitaji msuli wa sina ndugu soma hivo
Usipende discussion ya watu kibaooo utajiona tabularasa bure cheki watu wawili ambao wapo vizuri kichwani muwe mnadiscuss ni vema pia ujipe likizo huku jf huu muda wa kutoa thread na kukaa kujibu comments ungekua ushagain kitu..... All the best
 
Yahhh mi niko milambo boyz,ila Mazigazi unavyosema hama kombi unamaanisha nn mana itakuwa ni kitu cha kushangaza kidogo kwanza shule gan unahama comb ssiv,na kumbuka term ya kwanza ndo ishaisha sa sijakwelewa unamaanisha nn
Dogo watu tumepiga PCB acha uvivu:
Kilichonifanya mimi nitoke ni syllabus. Tafta iyo kiti kwa masomo yote. Usimeze kila kitu. Soma kwa technic.

Kama kuna nilosoma nao humu watatoa ushuhuda. Tulikuwa na group letu linaitwa G3. Kazi za group ni;

Kutungiana pepa tatu kila week yaan Bios- J tau, Chem J tano na Phsys ijumaa. Weekend ni correction ya pepa zote. No time to waste.

Utasema mlikuwa mnasoma sa ngapi. Mchna ndo ulikuwa mda wa kusoma. Sometime pepa zilipigwa usiku. Na kila mwanagroup ilikuwa lazima atunge pepa na ahakikishe anajua solution za maswali aliyotoa.

Group lilikuwa na watu nane; wote sasa hivi wanaofisi zao mjini hakuna alopiga chini.

Dogo kusoma na kujipanga.
 
Kjn mwanaume alie jituma hashindwi
Watu tuliwai pata 7%ya mechanics nusura tukimbilie egm ila tulipo kaza tulichomoka we komaa

Math na chem simple make sure unakuwa nondo kila sector then physics ina wababe wake km sio mbabe choose topic za kukutoa na komaa nazo .utachomoka

Angalizo
Usiwekeze kwenye physics utachinjwa kifo cha boko haram
Physics sitaki hata kuisikia. Ni kweli anatakiwa afanye bidii kama anauwezo wa tuition asome topic zote maana kwa mziki ule shule hata iweje hawawezi kumaliza topic zote labda kama wanaburuzwa. Ila pia ajue kabisa Phys ni nyoka wa mdoamdoa meupe na meusi. Yaana nani kaona nani hajaona. Mwisho wake huwa haujulijani hata kama unakesha unapiga tonics
 
Physics haitabiliki kvile hata uwe mzima vp inaweza kukusaliti hadharan ukabaki unalia pekeyako
Namba na chem...make sure unandaa banda kwanza hz huku physics mdogo mdogo
 
Mdogo wangu bora hata ulivyoamua kusoma hiyo combination ungekuja kule PCB na CBG ungekutana na life cycle yangu ndo ungenikubali maana lazima unimeze
 
Kama unakutana na topic inakushinda ka gugo kuna mengi sana online, uliza gugo chochote na peruzi hata websites zinazosaidia kwabmaswali na majibu na yamepatikanaje yapo.

Pia angalia kama kuna swala lingone nje ya shule linakufanya uone kila kitu kigumu ulitatue, ukiendelea hivi haitakusaidia.

Unaweza ingia mitandaoni basi fata mwalimu wa zaidi wa kukugundisha nae ni kupitia google.com au dot inchi utakayo kama google.co.uk mengi uwa sawa na nchini.

Nakutakia masomo mema.
 
Fanya hivi,soma kwanza zile topic nyepesi nyepesi kwenye kila somo. Kwa mfano,kwa A.Maths soma STATISTICS,SETS,CALCULATING DEVICES,COMPLEX NUMBERS,COORDINATE GEOMETRY 1. Baada ya hapo utaanza kufurahia mengine utaanza kuyaelewa vema. Usikimbilie hzo topic ngumu maana zitakukatisha tamaa. Usijali naamini utafanya vizuri. Nilpitia kipindi kigumu Kama hicho lakn mambo yalikuja kunyooka na sasa nipo chuo nadunda.
 
Mm nakushauri kuwa uchuhue juhudi binafsi kwa kuwa kufikia malengo yk ta shule ila walimu wa physics na mathematics wapo ila uwatafute ili wakusaidie
 
Hawa ndo wale wa kubadilisha mahala pa S wanaweka X
E.g
Mtumishi> Mtumixhi
Sasa> Xaxa

Pumbafu kabisa...

anyway we wa Advance Masomo ya hio combination unayosoma je una msingi mzuri??Unayamudu vilivyo??Hayo ni mambo ya msingi ambayo ulipaswa kujiuliza kabla ya kuanza kusoma!!
Milambo naifahamu ni shule ya serikali Changamoto nazifahamu mf. Ukosefu wa waalimu hasa katika masomo yako...
misosi duni..
Mi nimesoma bweni (nsumba boys) pia katika shule za sekondari so naelewa mambo yalivyo..ningependa nikusihi tu Ondoa dhana ya Ugumu katika masomo hayo..pia jitume kusoma kwa bidii,,fanya sana group discussions ndo siri ya mafanikio huko ulipo,,Likizo jiimarishe kwenye Tuitions soma piga topics na uzielewe Mwisho wa Siku Mungu atakujalia utapasua...Jitume mtoto wa kiume,,Fight!!Kumbuka unapigania maisha yako na ya familia yako pia kwa baadaee usikate tamaa!!
Mkuu umesoma Nsumba mwaka gani? Tujuane tafadhali
 
Back
Top Bottom