Mjusi Sharobalo
JF-Expert Member
- Sep 4, 2025
- 7,442
- 12,712
Msamaha si kwa ajili ya yule aliyekukosea, ni zawadi unayojipa mwenyewe. Ni kuamua kuacha kubeba mzigo wa maumivu. Samehe, weka mzigo chini, na songa mbele ukiwa mwepesi. Ukitaka kwenda haraka nenda peke yako. Lakini ukitaka kufika mbali, nenda na wenzako.
Thamani ya maisha haipimwi kwa mali, bali kwa watu unaogusa mioyo yao na wanaogusa moyo wako. Furaha sio kituo cha mwisho, bali ni namna ya kusafiri. Usisubiri kupata kila kitu ili uwe na furaha.
Tafuta furaha katika vitu vidogo vya kila siku; hewa safi, tabasamu la mwanao, kikombe cha chai. Kabla ya kutibu mti, chunguza mizizi yake. Kabla ya kumhukumu mtu, jaribu kuelewa hadithi yake. Kila mtu anapigana vita ambayo huijui... Mjusi na tafakari.