MMASSY
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 290
- 193
Ogopa sana kushindana na mtu aliyepoteza mwelekeo wa maisha....mtu huyo ni hatari sana kwani hana cha kupoteza wala hana mpango wowote na maisha yake ya baadaye kutokana na kujikatia tamaa.....
Mtu aliyepoteza mwelekeo wa maisha ni yule asiyeweza kusimamia mambo yake na kujali mambo yake na familia yake bali hutumia muda wake mwingi kufuatilia maisha ya watu wengine akiwa na lengo la kupotosha na kuchafua watu.Ni yule anayefuatilia madhaifu au mapungufu ya watu na kuyashikilia na kueneza mabaya ya watu kuliko mema yao kwa sababu anatamani na wengine wapoteze mwelekeo kama yeye........
Ni vyema kuwa makini na mtu wa aina hii na tumia hekima ya kutomsikiliza huku ukijiendeleza kufikia malengo yako ili uwe bora kuliko jana.Usikubali maneno yake yajenge kiota kwenye kichwa chako na usikubali moyo wako uumie kwa sababu yake maana shetani anamtumia kama chombo cha kukukatisha tamaa ili ushindwe kufika kwenye hatima yako iliyotukuka.
Kumbuka Bibiblia inasema siku zetu za kuishi si nyingi,tumia nafasi uliyopewa na Mungu kulifanya kusudi lake na fanikisha malengo yako!!
"Maisha ni safari,Marufuku kukata tamaa,nafasi yako bado ipo"
Kwanini usinipe jina kabisa nikakuwekea kitabu chako chenye kichwa hicho cha habari hapo juu? Usikose madini haya
Jerome Mmassy
Mwandishi Mwandamizi na Mkurugenzi Mtendaji.
Holy Hands Book Project
+255758673441