Maisha halisi ya watanzania

Tyrone mofekeng

JF-Expert Member
Mar 19, 2017
694
609
Kwa wanaoishi vijijini, Imani zao ni za kichawi. Wao hulaumu kila baya, iwe maradhi Au balaa lolote kua ni matokeo ya uchawi wa mtu fulani. Hasa wazee wenye macho mekundu. Inasikitisha sana.

Kwa wanaoishi mijini wao hawaamini kua wanaweza kupata maendeleo yoyote bila kupitia kwa mganga. Watanzania wanaishi nyumba moja ya vyumba sita familia sita na wameridhika kabisa.

Pia hupenda sana umbea. Hakuna hata mmoja aneona umbea ni kitu inayofaa kukemewa. Wameweka mbele umbea na kusemana vibaya.

Na wana wivu wa kupindukia kwa mmoja mmoja ambae ataonekana kama vile ana nafuu ya maisha.

Wanapenda sana kujikweza. Akitokea mmoja kasafiri Au kupata pesa kidogo. Atataka kila mtu ajue kua yeye ni tajiri mkubwa. Haoni shida kutaja kiasi alichokipata kwa kuzidisha sifuri kadhaa. Na atataka kila mtu ajue kua kasafiri huku na huko hata kama si muhimu.

Wakikusaidia ni lazima kila mtu inaewezekana kufikishiwa taarifa afikishiwe. Hawezi tu kukusaidia kwa moyo safi. Ni lazima atumie hilo kujipa kiki.

Hawapendi kutumia deodorant kujaribu kuzuia harufu mbaya ya makwapani ambayo ni adha hasa sehemu za maofisini. Na sijui kwa nini wakitoka chooni huacha sakafu ikiwa maji matupu kiasi cha kufanya kua kinyaa kwa mtu mwengine kutumia.

Wanadharau kazi zinazofanywa na watu wengine hata kama wenyewe hawana kazi. Hawaoni kua yoyote inayofanywa na mtu mwengine ni kazi kama sio ofisini. Sijui kwa nini.

Hii inatokana na nini? Watanzania wanateseka hivi nchini kwao mpaka lini. Kwa nini hawana tumaini kabisa la maisha yao. Kwanini wanajiliwaza kwa kujilinganisha na watanzania walio chini zaidi. Hivi Kuna njia yoyote ya kuwazindua kutoka kwenye kadhia hii
 
May god bless us poor Tanzania's sometimes kweliiii inaumiza jamaa angu wamemroga kisa DV 1 form four 16 cjui taifa linalaana ili au nn sielewi elewi.
 
Sema yote ila jamaa zetu apo jirani hawana Utu kabisa! Mambo mengine nikukosa hofu ya Mungu tu! Ila Africa hasa ukanda huu wa mashariki,kusini na west tabia zetu zinafanana sana!
 
Sasa wewe nyama ya kuku imebaki jana unaimwaga wakati wenzio wana mwaka hawajala kuku? Unataka wakufanyeje?
 
Back
Top Bottom