Kazi zoote hizo nalipwa shilingi za kitanzania 60,000 Cash mkononi kila baada ya siku 30 maana mpaka jumapili napigika, mgongo umeanza kupinda natembelea kifimbo kama kile cha mzee kifimbo cheza.
Nashkuru huu mshahara umenisaidia sana nimejenga nyumba ya vyumba vitatu na sebule na nyumba za uani za kupangisha, nina usafiri wangu wa boda vespa ya kuendea kuteseka kwa muhindi, nina somesha watoto wawili shule kubwa hapa mjini ada si chini 2M kwa Mwaka mzima.