Maisha bora kwa kila Mtanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha bora kwa kila Mtanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Luteni, Mar 3, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Watanzania milioni 8 washinda njaa kila siku(very sad)
  • Ni idadi inayokaribia waliopiga kura mwaka 2005

  WATANZANIA wapatao milioni 8.4 wanashinda na njaa au kulala njaa ili kukabiliana na ukali wa maisha, utafiti umeonyesha. Kwa mujibu wa utafiti wa Synovate uliofanyika kati ya Septemba na Desemba 2009, wananchi wanaahirisha milo kwa sababu hali ya kiuchumi ya Watanzania milioni 20 imezidi kuwa mbaya.

  Mbali na wale waliopunguza bajeti zao (asilimia 43), na wale walioamua kuacha kula baadhi ya milo kwa siku (asilimia 21), watu milioni 11.2 (wanaowakilishwa na asilimia 28 ya wahojiwa), walisema hawajachukua hatua zozote dhidi ya kuongezeka huko kwa gharama za chakula wakati watu milioni 1.6 (asilimia 4) walisema wamekopa kutoka kwenye benki za biashara na hawajui jinsi ya kurejesha mikopo hiyo.

  “Idadi ya wale waliosema kuwa hali zao za kiuchumi zimebakia vile vile ilikuwa ni watu milioni 16.8, ambao ni asilimia 42 ya wahojiwa.
  “Ni watu milioni 1.4 sawa na asilimia 4 tu ya waliohojiwa, ndio waliosema maisha yao yameboreka, huku watu wengine milioni 2 sawa na asilimia 5 ya waliohojiwa wakisema hawajui,” alisema meneja huduma wa Taasisi ya Synovate, Jane Meela.

  Kwa mujibu wa utafiti huo, idadi ya waliosema hali zao za kiuchumi zimekuwa mbaya zaidi ilikuwa kubwa zaidi kwa upande wa wanawake kuliko wanaume, wakati wanaume kidogo walisema hali zao za kiuchumi zilibakia vile vile.

  Kwa kuzingatia kipimo cha maendeleo ya jamii, kisiasa na kiuchumi (SPEC), wananchi milioni 17.2 pia wamelazimika kupunguza matumizi yao ya vitu vya nyumbani kutokana na kupanda kwa gharama za mahitaji ya msingi.

  Matokeo hayo yalitolewa na meneja utafiti na mawasiliano wa taasisi hiyo, Abdallah Gunda na meneja huduma, Meela, katika mkutano wao na wanahabari uliofanyika juzi jijini Dar es Salaam.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...