Maisha bora dubai........

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,875
Familia Nzima Wajinyonga Kukimbia Hali Ngumu ya Maisha (Read 6 times) Mwali Newbie
star.gif

Posts: 3



Familia Nzima Wajinyonga Kukimbia Hali Ngumu ya Maisha
« on: Yesterday at 05:48:46 PM »
Watu watatu wa familia toka India yenye makazi yake katika mji wa Dubai wamefariki dunia baada ya kujinyonga huku mtu wa nne ambaye ndiye aliyetoa wazo hilo la kujinyonga amenusurika maisha yake.

Kwa mujibu wa gazeti la Gulf News, baba mmoja wa Kihindi aliwashauri wanae wawili na mkewe wajinyonge kwa wakati mmoja ili kukimbia hali ngumu ya maisha iliyokuwa ikiwakabili.

Siku ya jumatano mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 40, mkewe mwenye umri wa miaka 38, mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 22 na mtoto wao wa kike mwenye umri wa miaka 20 walijifunga kitanzi na kujitundika kwenye feni la kwenye dari la nyumba yao iliyopo kwenye maeneo ya Karama mjini humo ili wafariki wote kwa wakati mmoja.

"Baba wa familia hiyo alikiri kuwa yeye ndiye aliyetoa wazo la kujiua", alisema Mkurugenzi wa kitengo cha makosa ya jinai cha Dubai, Khalil Ebrahim alipokuwa akiongea na gazeti hilo.

Baba huyo aliwaambia polisi kuwa kitanzi chake kilichoropoka toka kwenye feni na hivyo kunusurika maisha yake wakati mkewe na watoto wake hawakuwa na bahati kama yake na wote walifariki dunia.

Familia hiyo iliacha barua ikisema kuwa hali ngumu ya kiuchumi ndiyo iliyowafanya wachukue uamuzi huo.

Mwanaume huyo alikuwa akimiliki duka la nguo lililopo kwenye ghorofa alilokuwa akiishi na familia yake. Biashara yake ilikuwa haimuendei vizuri kama kawaida.

Dubai inakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi na madeni makubwa kufuatia mtikisiko wa mfumo wa fedha duniani.
 
Mtoa wazo alikuwa hayuko serious nini? Kawaacha wenzake walazimishe kutangulia mbele ya haki
 
Huyo mzee alikuwa mzanii. Kwanini hakuwasaidia wenzake baada ya kitanzi chake kuchoropoka?
 
mmmhhhhh....mm watu wajanja humu duniani...hicho kitanzi kilichoropoka kwa bahati kweli au?
umaskini mchungu..
 
Back
Top Bottom