Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,811
- 6,506
Wahenga walisema, Bahati haiji mara mbili.
Huwezi kutumia mbinu zile zile za mapambano mara mbili kwa adui huyo huyo ukategemea kupata ushindi hasa ikichukuliwa aliyekuwa mpiganaji mwenzako kwa sasa ndiye adui yako.
Mbinu anazozitua Lowassa kwa sasa ni zile zile ambazo alizitumia katika mchakato wa mgombea Urais mwaka 2005 uliomwingiza Ikulu Rais Kikwete lakini ukaacha majeraha makubwa ndani ya CCM.
Mbinu hizi kwa sasa CCM wamezistukia na mbaya zaidi, anawakaanga wapambe wake kwa kutumia hizo hizo mbinu zake za zamani.
Ni siku mbili zimepita ambapo tulisikia kwenye vyombo vya habari kelele nyingi zikisema madiwani zaidi ya 18 wametimkia CHADEMA kwa sababu ya kile kinachosemwa, kupinga maamuzi yaliyofanywa Dodoma na wana CCM katika kumpata mgombea Urais kwa tiketi ya CCM.
Hawa Madiwani walikuwa ni kama mbuzi wa kafara ili kuitisha na kuitingisha CCM ili impigie magoti Lowassa wapambe wake.
Kuzifahamu vizuri mbinu za Lowassa pitia thread hii,
Baadhi ya Madiwani, wamegundua kama wanachuuzwa na kwa maana hiyo, wengine wamerudi CCM haraka ili kuchukua fomu za Udiwani.
Mzee mwenye kile tuliaminishwa maamuzi magumu yuko kimya wakati wapambe wake hawafahamu hata hatima zao za kisiasa na kimaslahi. Jeshi lake lililokuwa vitani kwa nguvu ya pesa limesambaratishwa na Wazee wa CCM wakati kwa sasa kamanda wao hajulikani aliko!
Wapambe wake wanashindwa nini kuelewa? Lowassa alishasema, hawezi kuondoka CCM!
Kwa habari zaidi, ungana na ITV Local News,

Hali ya kisiasa kati ya CCM na Chadema katika wilaya ya Monduli imegubikwa na sinto fahamu na kuwachanganya wananchi wasijue pakuelekea baada ya madiwani kumi kati ya kumi na nane wa CCM waliyo daiwa kuhamia Chadema kusema bado wapo CCM na tayari wamesha chukua na kurudisha fomu za kutetea nafasi zao huku wananchi wakiwataka wanasiasa waache kuwachanganya kwa kuwafanya wajinga.
Wakizungumza na ITV baadhi ya madiwani waliyo daiwa kuondoka CCM wamesema kauli hizo hazikuwa za kweli kwakuwa baadhi yao walikuwa hawaja hafiki mpango huo na kwamba wanaendelea kuheshimu taratibu za chama chao huku wakidai wanatetea nafasi zao kupitia CCM.
ITV ilimtafuta mwekiti wa madiwani waliyo hama aliyekuwa diwani kata ya Lepurko Julias Kalanga ambaye amesema kilichopo ni baadhi ya watu kukosa kujiamini katika jambo wanalolifanya na kwamba wanataka kuficha moto usiyo fichika na kuwachanganya wananchi lakini siku ikifika ukweli utajulikaka huku katibu wa CCM mkoa wa Arusha Alphonce Kinamhala akithibisha madiwani hao kuchukua fomu za kugombea kupitia CCM na kwamba hizo zilkuwa mbinu za watu kuichafua CCM.
ITV ilizungumza na wakazi wa Monduli ambao wameonesha kusikitishwa na hatua ya wanasiasa kutokuwa wakweli na kuwataka wasiwachanganye kwani wananchi wa sasa siyo wa miaka ya nyuma pamoja na yote lakini watafanya maamuzi yenye maslahi kwao na siyo vinginevyo.
Last edited by a moderator: