Maige: Majungu CCM yameniondoa uwaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maige: Majungu CCM yameniondoa uwaziri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by engmtolera, May 29, 2012.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  May 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD][​IMG]


  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Monday, 28 May 2012 20:35[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  0digg
  [​IMG]
  Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii,Ezekiel Maige a​
  Shija Felician, Kahama
  BAADA ya kimya cha muda mrefu tangu ang'olewe katika nafasi ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige ameibuka na kueleza kuwa moja ya sababu ya kuondolewa kwake kwenye nafasi hiyo ni majungu ndani ya chama chake CCM na kuonya, hali hiyo ikiendelea chama hicho kitakufa.Hii ni kauli ya kwanza kwa Maige kuitoa hadharani akizungumzia kuondolewa kwake kwenye nafasi hiyo tangu Rais Jakaya Kikwete alipofanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri Mei 4, mwaka huu yaliyomng'oa Mbunge huyo wa Msalala.

  Jana, Maige akiwa mjini Kahama katika mkutano wake na viongozi wa CCM wa Wilaya hiyo na Mkoa wa Shinyanga, baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili katika jimbo lake, alionya kwamba kwa hali hiyo, CCM kinaelekea kubaya.

  Katika mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM akiwamo Mwenyekiti wa Mkoa, Hamis Mgeja, Maige alisema baadhi ya wanaCCM wamekuwa vinara wa kushabikia majungu aliyoyaita ya ‘kipumbavu’ badala ya kutembelea wananchi na kujua matatizo yao. Akaonya: “Majungu ya kipumbavu ya aina hiyo, yatasababisha chama kife.”

  Alisema kitendo cha baadhi ya wanachama wa CCM kushabikia kuondolewa kwake kwenye uwaziri, kinaonyesha jinsi gani ambavyo wameonyesha kuwa na uelewa mdogo wa kisiasa akisema walidhani wanamkomoa... “Kumbe wanajikomoa wenyewe.”

  Alihoji ni lini CCM kimefanya mkutano kwenye jimbo lake licha ya kuwa na nyenzo zote za usafiri ikiwemo magari na pikipiki lakini, Chadema wasiokuwa hata na baiskeli wameweza kupita jimbo zima wakifanya mikutano yao na kugawa bendera zao kama njugu.

  Alisema endapo majungu hayo yataendelea kitakufa na kuongeza kuwa wazee zaidi ya 300wa jimbo lake wamemfuata wakimtaka awaeleze anahama lini CCM ili wamfuate atakapokwenda.
  Hata hivyo, Maige alisema alitumia busara zaidi kuwatuliza na kuwapa pole kwa yaliyomfika ya kuzushiwa tuhuma kwenye wizara kwa lengo la kumchafua.

  Ailipua Kamati ya Maliasili
  Akizungumzia Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, Maige alisema taarifa yake rasmi haiendani na ile iliyosomwa bungeni hali ambayo alidai ilikuwa na lengo la kumng’oa kwenye uwaziri.
  Maige alishangaa kuona Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Mbunge wa Kahama, James Lembeli akimzushia kile alichokiita taarifa hiyo ambayo si kweli akisema madai yaliyokuwemo yalifanyiwa uchunguzi wa kina lakini, kwa kuwa ilikuwa imepangwa kwa lengo la kumng’oa ilitekelezwa.

  Alimtaka Lembeli warejee kwenye meza ya mazungumzo yenye kuwaletea maendeleo wananchi wa Kahama: “Baada ya kutekeleza lengo lake la kumng’oa kwenye uwaziri,” akisema kabla ya kupata wadhifa huo walikuwa marafiki na walitembea pamoja kwenye majimbo yote ya Kahama na Msalala kwenye mikutano yao.
  Lembeli: Maige apangue tuhuma

  Lembeli akizungumzia madai hayo ya Maige, alisema anachopaswa kufanya waziri huyo wa zamani ni kujibu tuhuma zilitolewa na kamati kuliko kuendeleza chuki binafsi zisizokuwa na msingi.

  Lembeli alisema kwamba haingii akilini kuona kwamba yeye mtu mmoja anaweza kutoa ripoti ya kamati ya watu 30 na kuweka mawazo yake binafsi.

  “Anachokifanya kunituhumu mimi ni chuki binafsi za kukosa uwaziri. Anachotakiwa ni kujibu hoja za kamati. Nilichokisoma pale ni ripoti ya kamati yote ya watu 30. Anachokifanya ni makosa,” alisema Lembeli.

  Katika ripoti yake, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alisema Wizara ya Maliasili na Utalii ilikuwa ikiongozwa na Maige, ilituhumiwa kuhusika na upotevu wa Sh800 milioni za mazao ya misitu huku Kamati ya Maliasili na Utalii ikimtuhumu waziri huyo kwa kujimilikisha vitalu.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Majungu uchori wako?
   
 3. S

  SirBonge JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2012
  Joined: Jul 18, 2010
  Messages: 349
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 60
  Huyu jamaa akae kimya tu na ishakula kwake, kwani alizaliwa akiwa waziri?? hata kama hukufanya hayo makosa wengine wataendelea kuongoza hiyo wizara kwani lazima uwe wewe?? Acha ujinga Maige kaa kimya ujipange upya!
   
 4. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Aache kubwabwaja huyu dogo....Mbona alipokuwa waziri hakusema kuwa sisiem kuna majungu? au ndio sizitaki mbichi hizi? nenda kapumzike dogo ulizochota zinatosha sana usitutue machungu hapa!
   
 5. WOWOWO

  WOWOWO JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2012
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  [​IMG]
  Tafakuri Jadidi

  Maige asitafute visingizio, tatizo ni unafiki wetu!

  Johnson Mbwambo


  23 May 2012

  WIKI iliyopita, kwenye mfululizo wa makala zangu kuhusu unyonyaji unaofanywa na kampuni za kimataifa za madini katika nchi masikini ikiwemo Tanzania, nilieleza namna kampuni ya Glencore ya Uingereza ilivyouziwa migodi ya Kansuki na Mutanda huko DR Congo kwa bei ya kutupa.

  Kashfa hiyo iliibuliwa na asasi ya wanaharakati inayoitwa Global Witness. Katika ripoti yake Global Witness inasema kuwa, ndani ya mwaka mmoja tu watendaji wakuu sita wa kampuni hiyo wamekuwa mabilionea; ilhali Wakongo wa maeneo iliyoko migodi hiyo wanazidi kuteseka kwa umasikini.

  Baada ya kuisoma tafakuri hiyo, msomaji wangu mmoja anayefanya kazi katika mgodi wa Bulyanhulu alinitumia sms ambayo nimeshawishika kuichapa kama ilivyo ili nanyi muisome. Msomaji huyo aliandika hivi:
  “Ndugu yangu Mbwambo, nimefuatilia makala zako hizi kuhusu madini kwa wiki mbili. Ni kweli uliyoandika. Hata hivyo, si Congo tu ambako wageni wamekuwa mabilionea kwa kutumia madini yetu ilhali sisi wenyewe tumebaki masikini.

  “Tangu nimeajiriwa hapa kwetu kwenye mgodi wa Bulyanhulu, mameneja wote waliopita hapa sasa ni mabilionea. Gareth Taylor sasa anamiliki New Luika Gold Mine kule Chunya (Mbeya) na kampuni yake ya Shanta Mining inafanya utafiti wa madini maeneo mbalimbali nchini. Huyu alikuwa mtendaji mkuu wa Barrick kuanzia 2006 hadi 2009.

  “Mwingine ni Mike Mracek ambaye aliondolewa baada ya kuwasilisha bajeti iliyotaka kima cha chini cha mshahara cha sisi wafanyakazi kiwe shilingi milioni moja kwa mwezi kulingana na uzalishaji wa Bulyanhulu .

  “Mwingine ni Greg Walker. Huyu aliondolewa Bulyanhulu tayari akiwa bilionea. Alipelekwa kuwa mtendaji mkuu wa Australia na Pacific akiwa tayari bilionea, akaja Kevin Moxham akitokea North Mara naye aliondoka hapa akiwa tayari ni bilionea.

  “Mpaka sasa mgodi umechimbwa hadi kufikia mita 3,800 kutoka usawa wa bahari, na dhahabu inaendelea kutajirisha wakubwa! Kama taifa, tumekwisha.
  Sasa hivi mzalendo ukijifanya mjuaji unapelekwa gerezani Shinyanga. Wenzetu saba waliojifanya wapigania haki wako gerezani Shinyanga kwa kesi ya kusingiziwa kutaka kulipua mgodi, na cha kushangaza ni kuwa, serikali yetu haijali na inawaunga mkono wawekezaji hawa wa kigeni mia kwa mia katika kila jambo”.
  Hivyo ndivyo alivyolalamika msomaji wangu huyo wa Bulyanhulu. Kwa hakika, sina cha kuongeza. Niliamua kuichapa sms yake hiyo ili tu kuthibitisha kuwa si DR Congo tu ambayo imegeuzwa shamba la bibi na wawekezaji hao wa kigeni wa madini; bali hata Tanzania yetu.

  Baada ya kumaliza kuyasema hayo, nirejee katika tafakuri yangu ya leo ambayo inahusu kauli iliyotolewa na Ezekiel Maige - mmoja wa mawaziri waliotupwa nje na Rais Kikwete katika mabadiliko yake ya hivi karibuni ya baraza la mawaziri.
  Akiandika, wiki iliyopita, kwenye tovuti ya mijadala ya kijamii inayoitwa Wanabidii Forum, Bw. Maige alilalamika sana kung’olewa kwake uwaziri na Rais Kikwete.

  Aliandika kuwa, aling’olewa uwaziri kwa sababu ya kugusa maslahi ya vigogo wenye nguvu kubwa na ushawishi wa hali ya juu hapa nchini.

  Maige aliendelea kuandika kuwa, kwa maamuzi aliyokuwa akiyatoa wakati akiwa waziri, alijua fika kuwa hayawafurahishi vigogo hao na kwamba angeondolewa. Alisema kuwa mengi zaidi ataongea bungeni.

  Si hivyo tu; kwani waziri huyo wa zamani wa Wizara ya Mali Asili na Utalii anasisitiza: “Nawahakikishia wazalendo kuwa wamempoteza mpambanaji aliyejitolea kupambana na wahalifu angani, majini, porini, mijini, vijijini na nje ya nchi.”

  Hivyo ndivyo alivyolalamika Maige kuhusu kuondolewa kwake uwaziri. Sijui ni kwa nini aliamua kutumia njia hiyo ya kuandika mtandaoni malalamika yake hayo badala ya kuita waandishi wa habari na kujieleza – hatua ambayo ingetoa fursa kuulizwa maswali.

  Nina hakika angeombwa awataje vigogo hao wenye ushawishi mkubwa waliosababisha atoswe uwazirti. Je ni hawa Waarabu na Wazungu waliojenga mahoteli ya kitalii katika hifadhi zetu za taifa? Je, ni hawa vigogo wanaoendesha biashara za vitalu vya uwindaji? Au ni hawa magwiji wa biashara haramu ya kusafirisha magogo nje ya nchi?

  Vyovyote vile, Maige analalamika kuwa ameondolewa uwaziri kwa sababu ya kugusa maslahi ya vigogo wenye nguvu kubwa ya ushawishi nchini. Ingawa hakutaja majina ya vigogo hao, lojiki inatufanya tuamini kuwa vigogo hao wakubwa wana mahusiano ya karibu na Rais Kikwete.

  Nasema lojiki inatutuma tuamini hivyo, kwa sababu hakuna mwenye mamlaka ya kuteua au kumng’oa waziri, mbali ya Rais Kikwete mwenyewe.

  Kama Kikwete amemng’oa Maige uwaziri, na kama Maige mwenyewe anasema kung’olewa kwake ni kwa sababu ya kugusa maslahi ya vigogo hao wenye ushawishi mkubwa hapa nchini, basi lojiki ni kuwa Rais Kikwete na vigogo hao ‘la kwao ni moja’. Hiyo ndio mantiki iliyomo kwenye malalamiko ya Maige.

  Kwa hiyo, tunaweza kusema kuwa mbaya wa Maige si vigogo hao wenye ushawishi mkubwa, bali ni Rais Kikwete anayewakingia kifua. Sasa kama hivyo ndivyo, yaani kama Rais ndiye aliyekuwa akimkwaza, kwa nini Bw. Maige hakujiuzulu uwaziri kulinda heshima ya uchapaji kazi wake mzuri?

  Mathalan; kama alimkamata kigogo aliyekuwa akitorosha nje ya nchi nyara za serikali au wanyama hai, lakini alishindwa kumfikisha mahakamani kwa sababu ya kukingiwa kifua na Rais Kikwete, kwa nini hakuwasilisha kwa Rais barua ya kujiuzulu uwaziri?

  Nasema hivyo; maana, waziri yeyote mwadilifu na anayejali na kuheshimu kazi yake, hawezi kukubali kuendelea na kazi hiyo kama Rais anamkwamisha asishitaki vigogo wanaoongoza kwa uhalifu unaochafua wizara yake.

  Kwa maneno mengine, busara ni kwamba ukishakuwa na tofauti za kimsingi za kiutendaji kati yako (waziri) na Rais, hatua inayostahili kuchukuliwa ni wewe (waziri) kujiondoa kumtumikia rais wa sampuli hiyo – yaani unajiuzulu uwaziri, na tena baada ya kufanya hivyo unautangazia umma kwa nini umejiuzulu!

  Lakini Maige wetu hakufanya hivyo. Kwa maelezo yake mwenyewe kwenye mtandao, vigogo hao wakubwa wenye ushawishi mkubwa nchini (bila shaka ushawishi kwa Rais Kikwete) walimkwamisha kutenda kazi zake, sasa kwa nini hakujiuzulu uwaziri wakati huo; hasa ikizingatiwa kuwa vigogo hao wana ushawishi mkubwa kwa rais?

  Isitoshe, Maige wetu hakupata kamwe kulalamika juu ya kuwepo vigogo hao wanaomkwaza wenye ushawishi mkubwa nchini wakati bado akiwa waziri, bali tumeyasikia malalamiko yake hayo, kwa mara ya kwanza, baada ya kuwa ametemwa uwaziri!

  Hii ina maana kuwa, Bw. Maige si kiongozi jasiri. Si kiongozi asiyekubali kusutwa na dhamira yake. Kama kweli angekuwa na sifa hizo, basi, angeshajiuzulu uwaziri na kuufanya moyo wake uwe na amani kuliko kukubali kuendeshwa puta na vigogo hao wenye ushawishi mkubwa kwa Rais.

  Kama angefanya hivyo, sifa na jina lake vingebaki katika vitabu vya kumbukumbu za historia za mawaziri wetu jasiri walioweka ubinafsi pembeni na kuamua kuutema uwaziri baada ya kuibuka tofauti za kimsingi za kiutendaji kati yao na rais.

  Lakini kwa sababu hakufanya hivyo, historia itamtaja kuwa ni waziri aliyetemwa na rais kwenye baraza la mawaziri baada ya wizara yake kuhusishwa na ufisadi katika ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

  Kwa kuamua kulalamika sasa baada ya kuwa ameshatemwa uwaziri, Maige wetu anatuthibitisha tu kwamba ana hulka za kinafiki. Mbona hakueleza yote hayo ya kukwazwa na vigogo wenye ushawishi mkubwa alipokuwa bado waziri, na badala yake alisubiri ang’olewe uwaziri ndipo ateme cheche?

  Ndugu zangu, nimelizungumzia kwa kirefu suala hilo la Maige, kwa sababu linathibitisha, kwa mara nyingine tena, hulka ya mawaziri wetu wengi ya kupenda kuwa watu wa “ndiyo mzee” kwa rais, lakini waking’olewa uwaziri ndo huwa wakosoaji wakubwa wa rais husika.

  Hulka hii, ambayo tumepata kuiona kwa Profesa Jonathan Moyo wa Zimbabwe, ni ya kinafiki, na ndiyo maana namshauri Ezekiel Maige ajifungie tu mdomo wake; maana amechelewa mno kuufungua kwa kuponzwa na ‘utamu’ wa uwaziri!
  Labda nikumbushe kwamba nchi yetu hii imepata kuwa na viongozi wachache (wanaofaa kuigwa na viongozi wetu wa sasa) ambao walikuwa na ujasiri wa kujiuzulu, kwa hiari, vyeo vyao baada ya kutofautiana kiutendaji na wakubwa.

  Namzungumzia mtu kama Edwin Mtei (soma kitabu chake: From Goatherd to Governor) ambaye mwaka 1979 alijiuzulu uwaziri wa fedha baada ya kuwa na tofauti za kimsingi na Mwalimu Nyerere.

  Wakati huo, uchumi wa nchi ukiwa shaghalabaghala kutokana na vita dhidi ya Amin, Benki ya Dunia (WB) ilitaka tushushe thamani ya shilingi yetu na tubinafsishe mashirika ya umma ndipo tukopeshwe fedha.
  Mtei alikubaliana na matakwa hayo, lakini Mwalimu Nyerere hakuiona lojiki ya kupewa masharti hayo na Benki ya Dunia, na hivyo akakataa.

  Kutokana na hali hiyo, Mtei aliona hawezi tena kufanya kazi katika Serikali ya Nyerere, na hivyo akaamua mwenyewe, kwa hiari, kuutema uwaziri!

  Lakini wapo pia viongozi wa chini – wa hata ngazi ya u-DC ambao waliamua kuondoka serikalini, kwa hiari, baada ya kuibuka tofauti kubwa za mitazamo ya ki-sera na ki-utendaji kati yao na serikali. Katika orodha hiyo yumo mwanasafu mwenzangu na mwenyekiti wa bodi wa gazeti hili, Jenerali Ulimwengu.

  Hata majuzi tu hapa, tulipata kusikia habari za DC mmoja kule Mbeya aliyeamua, kwa hiari, kuuachia u-DC kwa sababu hiyo hiyo ya tofauti za kimisimamo.

  Ndugu zangu, viongozi wenye ujasiri wa aina hiyo na wasio wanafiki ndio tunaowahitaji Tanzania, na si hawa wanaosubiri watupwe nje ya uwaziri ndipo waueleze umma yaliyo ndani ya mioyo yao.

  Tunataka viongozi wasio wabinafsi na wasio tayari kusaliti dhamira zao. Tunataka mawaziri ambao wanaitumikia serikali kwa sababu tu wanaamini katika hiyo serikali na sera zake, na wanaamini katika uadilifu wa huyo rais anayeiongoza, na si kwa sababu ya imani zao kuwa uwaziri ni njia ya mkato ya safari ya kuutafuta utajiri!

  Tunataka mawaziri ambao kwenye vikao vya baraza la mawaziri wana ujasiri wa kumwambia rais ukweli kwa namna wanavyouona wao, na si kuwa watu wa “ndiyo bwana’ kwa kila jambo linaloletwa mezani na rais. Hatutaki viongozi ambao kwenye vikao ni ‘mabubu’ lakini nje ya korido za ukumbi wa mkutano ndo wa kwanza kulalamikia misimamo hii na ile ya kiutendaji ya rais.

  Kwa bahati mbaya wenye sifa hizo za kina Edwin Mtei ni wachache mno hapa nchini zama hizi. Walio wengi zama hizi wamejawa na unafiki tu; maana wanachokitafuta serikalini ni utajiri tu na si kutumikia wananchi.

  Ni nadra zama hizi kuwapata viongozi wenye ujasiri aliokuwa nao Edwin Mtei - ujasiri wa kumwangalia Nyerere usoni na kutofautiana naye kwa kumweleza alichokiamini moyoni. Viongozi wa sampuli hiyo wameadimika sana nchini zama hizi. Waingereza wangesema ni en-dangered species katika nchi yetu Tanzania.

  Tafakari!
   
Loading...