Mahusiano yangu yaliyopita yameniathiri sana

King Nathan

Member
Mar 8, 2023
17
19
Wasalaam....

Naomba niende moja kwa moja kwenye huu uzi ndugu zangu, huku kipenga kikiwa tayari kimeshapulizwa

Twende kazi sasaaa.....

Ni mwaka sasa umepita tangu niachane na Ex wangu lakini mambo yangu hayapo sawa yaani hasa upande wa mahusiano, nilimpenda sana Ex wangu na yeye alikuwa ananipenda japo moyo wa mtu ni kichaka huwezi jua kwenye moyo wake alikuwa kamuweka nani ila niñahisi bado nampenda japo sitaki kuukubali ukweli kwani baada ya mambo kunifika shingoni mimi ndiye niliyeamua tuachane baada ya kuona mwenendo wa mwenzangu umebadilika, yaani si kwa makusudi bali kwa kulinda heshima yangu kama mtoto wa kiume mwenye misingi yake.

Uhusiano wetu ulidumu takribani miaka miwili na sikujua kama ipo siku itakuwa mwisho, maana kama kugombana tumegombana sana, kukaushiana wiki hadi mwezi imetokea sana lakini sio kuomba kuachana, Ila kuna kipindi mawasiliano yetu ghafla yalipungua, maana kuwasiliana kwetu ilikuwa ni kama Mchungaji na maombi au Mwamposa na mafuta ya upako au Shekhe na swala kuna kipindi naomba game nanyimwa kidizaini mara oooho leo sipo vizuri mara nipo bize yaani ili mradi tu asikose sababu japo sikuwa na wasiwasi kwani huwa inatokea wakati mwingine hatuchezi game mara kwa mara na mara nyingi mimi huwa ndio mpangaji wa ratiba ya ligi kuu . Ila sasa kipindi hiki hata mwenzangu akisafiri anakuwa aniambii tofauti na huko nyuma hata akirudi pia hasemi unashtukia tu huyu hapa, nilikuwa nikimuelekeza anaomba samahani yanaisha kiukweli iliniuma sana ila sikuwa na namna ukizingatia mimi ni mtu wake wa karibu, hali hii ilidumu kama miezi mitatu hivi hadi pale ilipotokea kuvunjika kwa pakacha

Ndugu zangu ukiona mtu ameamua kuandika hivi ujue mambo yamemfika shingoni. Basi nakuomba unipe muda wako ili tusonge na simulizi hii ya kukata na shoka

Kuna siku flani aliniambia anataka kuonana na mimi, mimi nikajua ni jambo la kawaida tu anataka tuongee tubadilishane mawazo kama wapenzi kwani kuna muda tulikuwa hatujaonana zaidi ya kuwasiliana tu. Nikajua mtoto kanimisss bhana Ilibidi nianze kudadisi ili kujua maongezi hayo yanahusu nini Ila baada ya kumshawishi sana ilibidi aniambie kuwa amefikiria ameona ni vema mahusiano yetu yafike mwisho, ukiona jambo kama hili nadhani hata kama ni wewe unavuta picha gani kichwani mwako aisee nilihisi moyo umeacha kutembea wakati nikiwa mzima kauli ile ilibadilisha taswira yangu ya furaha na uchangamfu kwa siku hiyo na kuwa ya huzuni

Mazungumzo yetu yaliendelea huku nikimshawishi abadili maamuzi yake japo kwa shingo upande alikubali lakini si unajua tena mtu akishapanga lake hawezi kurudi nyuma japo atakubali kwa shingo upande ili kukutuliza tu.

Basi jioni ya siku hiyo nilipanga tuonane kwa mazungumzo ili kuendelea kupata maridhiano zaidi si unajua tena maridhiano sio Chadema na Mama tu bali hata kwenye mapenzi pia yapo tena kwa ukubwa zaidi, lakini pia ukikipenda kitu chako siku zote huwezi kuwa tayari kukipoteza, utatumia hata mbinu za kivita ikibidi, hivyo niliamua kuuvaa uhusika kama wale Wazee wa Mabaraza ya usuluhishi kwenye ofisi za Kata hapa nchini mwetu basi bwana ilipofika jioni ya siku hiyo nikamcheki mtoto akaniambia nikifika nimshtue ili aje tulipopanga kukutana...

Nikasema poa. Siku hiyo ya jumapili dereva wa daladala la buza alikuwa anaendesha gari kama vile hataki yaani taratibuu mpaka nikawa namtukana kimoyo moyo maana lengo langu lilikuwa nifike haraka nikaonane na Bibie niliyekuwa nina hamu ya kuonana nae, Mungu si athumani nilifika salama bin salmeen nikamshtua Bibie akaja tukakaa sehemu tukaanza mazungumzo yetu cha ajabu mazungumzo yetu hayakuwa kama yale ya asubuhi tuliyozungumza bali yalikuwa ni maongezi flani hivi ya kawaida tu kama siku zote yaani kama vile hakuna kitu chochote kilichotokea, bila kupoteza wakti niliagiza vinywaji na chakula tukaanza kula huku mazungumzo yakiendelea. Muda ulipofika ilibidi tuagane na kila mtu arudi nyumbani kupumzika maana ilikuwa ishafika kama mida ya saa 4 hivi usiku.

Naomba niishie hapa nipatapo muda nawaahidi kuleta mwendelezo na kumalizia kisa hiki

Tabia za kitoto hizo.
 
Back
Top Bottom