Mahusiano yanapaswa kuchukua muda gani hadi kufikia ndoa?

jean phillipe beyun

Senior Member
May 18, 2015
142
167
Wadau nawasalimu,

Mtu mmoja humu jamvini katika mkasa wake alitaja kuwa mahusiano yao yana umri wa 3 yrs, watu wakawa wakali wakiuliza 3 yrs yote hiyo mnasubiri nini hasa?

Haya mdau mwingine katika mkasa wake alidai uhusiano wake ulichukua miezi sita wakafunga ndoa, baadae akapata matatizo makubwa kwenye hiyo ndoa, wadau humu jamvini wakaanza kumshambulia kuwa mmefahamiana kwa miezi sita tu mkafunga ndoa?

Sasa nimeona niulize ni muda upi haswa ndio muda sahihi wa kufahamiana katika relationship hadi kufikia ndoa?

Uhusiano unapaswa kuchukua muda gani ndipo muoane?

Na je kudumu kwa ndoa kunategemea na muda mliofahamiana? Au mliokaa kwenye relationship?
 
ukipata mtu sahihi hata wiki 1 inatosha.

mnaweza kufahamiana miezi 3 ndoa ikadumu wengine wanafahamiana miaka 3 ndoa haidumu.

vijana wa sasa tatizo hatuna uvumilivu mtu anahesabu kasoro za mwenzake lakini yeye kasoro zake hazioni.
 
Wadau nawasalimu

Mtu mmoja humu jamvini ktk mkasa wake alitaja kuwa mahusiano yao yana umri wa 3 yrs, watu wakawa wakali wakiuliza 3 yrs yote hiyo mnasubiri nn hasa?

Haya mdau mwingine ktk mkasa wake alidai uhusiano wake ulichukua miezi sita wakafunga ndoa, baadae akapata matatizo makubwa kwenye hiyo ndoa, wadau humu jamvini wakaanza kumshambulia kuwa mmefahamiana kwa miezi sita tu mkafunga ndoa?

Sasa nimeona niulize ni muda upi haswa ndio muda sahihi wa kufahamiana ktk relationship hadi kufikia ndoa?

Naomba wana jamvi mtofautishe uchumba na uhusiano wa kimapenzi wa kawaida. Uchumba ndio haupaswi kuchukua mda mrefu, uchumba maximum unapaswa usichukue zaidi ya miezi 6. Lakini urafiki wa kimapenzi unaweza kukaa for as long possible hadi mtakapokuwa tayari kuingia ktk hatua ya uchumba na hatimae kufunga ndoa.

Hivyo unapokuwa katika uhusiano wa kimapenzi ni vyema wapenzi wakapata mda wa kutosha wa kuweza kuchunguzana na kubaini kama huyo mwenzi wake aliyenaye kwenye mahusiano ana sifa za kuwa mke/mume wake wa ndoa au la. Ila pia si vyema sana

Lakini kumbuka ngoja ngoja yaumiza matumbo na haraka haraka haina baraka. Hivyo si vyema ukakaa mda mrefu kwenye uhusiano wa kimapenzi kama kweli una nia ya kufunga ndoa na huyo mwenzi wako lakini si vyema kuwahi pia. Kama unaona huyo mwenzi uliye naye hafai kuwa mke/mume basi ni vyema umueleze ukweli na umuache aende zake kuliko kumpotezea mda na kumpa matumaini ambayo hayapo.
 
Muda haujalishi sana bali effort mnayotumia kujuana. Miezi 6 inatosha hata chini ya hapo kama mlipata muda wa kujuana zaidi na kuelewana.
 
Wadau nawasalimu

Mtu mmoja humu jamvini ktk mkasa wake alitaja kuwa mahusiano yao yana umri wa 3 yrs, watu wakawa wakali wakiuliza 3 yrs yote hiyo mnasubiri nn hasa?

Haya mdau mwingine ktk mkasa wake alidai uhusiano wake ulichukua miezi sita wakafunga ndoa, baadae akapata matatizo makubwa kwenye hiyo ndoa, wadau humu jamvini wakaanza kumshambulia kuwa mmefahamiana kwa miezi sita tu mkafunga ndoa?

Sasa nimeona niulize ni muda upi haswa ndio muda sahihi wa kufahamiana ktk relationship hadi kufikia ndoa?

Uhusiano unapaswa kuchukua muda gani ndipo muoane?

Na je kudumu kwa ndoa kunategemea na muda mliofahamiana? Au mliokaa kwenye relationship?
Ndugu ukifuatilia comment za humu utapasuka kichwa....
 
Naomba wana jamvi mtofautishe uchumba na uhusiano wa kimapenzi wa kawaida. Uchumba ndio haupaswi kuchukua mda mrefu, uchumba maximum unapaswa usichukue zaidi ya miezi 6. Lakini urafiki wa kimapenzi unaweza kukaa for as long possible hadi mtakapokuwa tayari kuingia ktk hatua ya uchumba na hatimae kufunga ndoa.

Hivyo unapokuwa katika uhusiano wa kimapenzi ni vyema wapenzi wakapata mda wa kutosha wa kuweza kuchunguzana na kubaini kama huyo mwenzi wake aliyenaye kwenye mahusiano ana sifa za kuwa mke/mume wake wa ndoa au la. Ila pia si vyema sana

Lakini kumbuka ngoja ngoja yaumiza matumbo na haraka haraka haina baraka. Hivyo si vyema ukakaa mda mrefu kwenye uhusiano wa kimapenzi kama kweli una nia ya kufunga ndoa na huyo mwenzi wako lakini si vyema kuwahi pia. Kama unaona huyo mwenzi uliye naye hafai kuwa mke/mume basi ni vyema umueleze ukweli na umuache aende zake kuliko kumpotezea mda na kumpa matumaini ambayo hayapo.

Nimeipenda....
 
Mi nadhani unakaa nae huyo unaetaka akuoe/umuoe muda wowote unaoona na utakaporidhika kuwa anafaa kuwa pamoja na wewe katika ndoa unaoa/olewa hata kama ni miaka ama siku chache tu ilimradi tu uwe unamfahamu ni mtu wa aina gani ili asikupe shida kuishi nae mkishafunga ndoa
 
jaman swala la ndoa ajuaje ni Mungu tuu.ushasema mda wa kuchunguzana iv nan atajiweka waz akat unajua unachunguzwa?? mi nna ushahid wa familia yetu,ndugu wa ukoo alikua akiishi nyumban kwetu,uyu dada aliolewa bila kupima kipind cha urafiki wala uchumba.can u imagin,alikutana na mtu within a weak wakaanza kuishi pamoja na mpaka sasa tayar wana ndoa na watoto watatu tena amani iko tele japo kupishana kupo.sasa we jitie mwerevu kumchunguza mtu miaka 17 alaf unasema hafai
 
Kumfahamu mtu vizuri na hadi pale utakapo kaa nae kwa mda fulani lakini ile ya kuonana tu weekend na sio rahisi kumchunguza mtu kwani kila mmoja wenu anakua anaonyesha kumjali mwingine kwa hali ya juu. Kama utapata mtu ambaye unaona anakufaa basi fanya maamuzi sahihi.mapungufu yapo kwa kila mmoja kwan hakuna aliyekamilika.
 
mi siungi mkono hoja yakuchunguzana
 
jaman swala la ndoa ajuaje ni Mungu tuu.ushasema mda wa kuchunguzana iv nan atajiweka waz akat unajua unachunguzwa?? mi nna ushahid wa familia yetu,ndugu wa ukoo alikua akiishi nyumban kwetu,uyu dada aliolewa bila kupima kipind cha urafiki wala uchumba.can u imagin,alikutana na mtu within a weak wakaanza kuishi pamoja na mpaka sasa tayar wana ndoa na watoto watatu tena amani iko tele japo kupishana kupo.sasa we jitie mwerevu kumchunguza mtu miaka 17 alaf unasema hafai
mi siungi mkono hoja yakuchunguzana
 
ukipata mtu sahihi hata wiki 1 inatosha.

mnaweza kufahamiana miezi 3 ndoa ikadumu wengine wanafahamiana miaka 3 ndoa haidumu.

vijana wa sasa tatizo hatuna uvumilivu mtu anahesabu kasoro za mwenzake lakini yeye kasoro zake hazioni.

Unachosema mkuu ni sahihi kabisa ninao mfano halisi kwa moja wa majamaa zangu yeye alifahamiana na mwenzie ndani ya mwezi akaoa.
 
Kumfahamu mtu vizuri na hadi pale utakapo kaa nae kwa mda fulani lakini ile ya kuonana tu weekend na sio rahisi kumchunguza mtu kwani kila mmoja wenu anakua anaonyesha kumjali mwingine kwa hali ya juu. Kama utapata mtu ambaye unaona anakufaa basi fanya maamuzi sahihi.mapungufu yapo kwa kila mmoja kwan hakuna aliyekamilika.
Siku hizi wanachunguzana kwenye Whatsapp
 
TATIZO HUMU KILA MTU ATAKUJI KWA UZOEFU WAKE KWENYE MAHUSIANO.
1.ALIYEKAA NA MTU MDA MREFU HALAFU WAKATEMANA, ATAKWAMBIA KUWA MUDA MREFU HAUFAI
2.ALIYEKAA NA MTU MDA MFUPI THEN AKAMUOA YAKAMKUTA YALIYOMKUTA , ATAKWAMBIA BORA UKAE MDA MREFU MJUANE.

KWA MFANO KUNA JAMAA ALIJUANA NA DEMU MIEZI 6 AKAWEKA NDANI, BUT WALIKAA MWAKA TU, JAMAA AKASEMA SIWEZI SIWEZI KUKAA NA YULE MWANAMKE HATA IWEJE, SO IMAGINE JAMAA AKAHAMA NYUMBANI AKAMUACHIA NYUMBA YULE MWANAMKE NA MTOTO WAKE MDOGO YEYE AKAENDA KUPANGA. SO MTU KAMA HUYO UKIMUULIZA HILI SWALI WATEGEMEA AKUJIBU NINI?.....ALL IN ALL MUDA UFAAO WANAUJUA WALIO KWENYE MAHUSIANO, MDA UTAKAPOFIKA THEN WATAOANA NA SIO KUWAWEKEA TIMELINE KWAMBA LEO AU KESHO!!!
NI HAYO TU KWA LEO.
 
Wadau nawasalimu,

Mtu mmoja humu jamvini katika mkasa wake alitaja kuwa mahusiano yao yana umri wa 3 yrs, watu wakawa wakali wakiuliza 3 yrs yote hiyo mnasubiri nini hasa?

Haya mdau mwingine katika mkasa wake alidai uhusiano wake ulichukua miezi sita wakafunga ndoa, baadae akapata matatizo makubwa kwenye hiyo ndoa, wadau humu jamvini wakaanza kumshambulia kuwa mmefahamiana kwa miezi sita tu mkafunga ndoa?

Sasa nimeona niulize ni muda upi haswa ndio muda sahihi wa kufahamiana katika relationship hadi kufikia ndoa?

Uhusiano unapaswa kuchukua muda gani ndipo muoane?

Na je kudumu kwa ndoa kunategemea na muda mliofahamiana? Au mliokaa kwenye relationship?

Mimi Uhusiano ulikua mwezi mmoja nikawa nimeshakata shauri mwenzangu kukubali ilichukua miezi miwili na nilimshawishi sana ... ndoa yangu ilidumu kwa miaka 10 kwa amani sana mpaka mapenzi ya Mungu yalipotekelezwa... amani kwa maana ya amani kweni alikua mtu muhimu haswa kwenye maisha yangu kila siku ilikua kama tumeonana siku hiyo.. tulitoka out .... kama tuna date..... sometimes tulikwenda honeymoon ya utu uzima nje ya nyumbani hata wengine walidhani bado tu wapenzi na hatuishi pamoja..... hakuna formular Ni Mungu tu atangulie njia ..... mmnaweza mkakaa miaka kumi mkizini na mkaishia kuoana huku tayari mmeshachokana yaani mnaoana kwa aibu ya watu au influance ya familia na watoto mapenzi yalisha isha zamaaani........ LAA TAKRAB ZINAA
 
Back
Top Bottom