Mahusiano yakikosa maono ni ngumu sana kudumu

brenda18

JF-Expert Member
Sep 17, 2013
5,687
5,272
Asubuhi ya leo nimejifunza kitu, inaweza isimguse kila mtu lakini yupo itakae mgusa kama ilivyonigusa mimi,

Hapa naongelea watu wenye nia ya mahusiano ya kudumu na si "hit and run"
Katika pita pita zangu nimesoma sehemu nikajifunza kama upo kwenye mahusiano na huna maono au hakuna maono ya mahusiano hayo basi ni ngumu sana kudumu mtakapopita kwenye misukosuko ya hapa na pale.

Mahusiano yoyote lazima yapite kwenye majaribu, inawezekana mmoja akapatwa na jaribu mara nyingi mambo yakiwa magumu sana tunakimbia hata kama tulikuwa na malengo mazuri tu kwenye mahusiano hayo

Kuna watu hawawezi kutimiza mwaka wakiwa kwenye mahusiano,kikitokea kitu kikaharibu mahusiano kidogo tu yupo tayari kuanza upya, kwa mwaka unaweza kujikuta umekuwa kwenye mahusiano na watu hata watatu,

Wapo ambao ni waoga kuoa au kuolewa, wapo pia waliooa na kuolewa na ndoa zao hazina maono pia huko mbeleni lazima washindwe chanzo cha ndoa nyingi kufa hawana maono ya pamoja (lack of vision) hivyo wakikumbwa na majaribu hatima yao wanaona ni kuachana ndoa si lelemama (japo sina experience nayo ila ni kitu nakiona kwenye jamii)

Kabla ya kuanza mahusiano hakikisha kitu ulichokiona kwa mwenza wako nayeye ndicho alichokiona mfano wewe umeona mbali mkifunga ndoa na kuwa na familia meanwhile yeye maono yake ni kukuchuna pesa na kutimiza malengo yake financially etc my dear hapo hakutakuwa na mahusiano imara na hapa ndipo wengi tunakosea

Tujitahidi kabla ya kuingia kwenye agano la ndoa tukitoa vigezo vyote vingine kama appearance, elimu etc lakini tuna maono yaliyo sawa, ndoa ni hatua tu ya kuwafikisha huko kwenye maono, hata mkikubwa na makubwa kiasi gani mkikumbuka vision mlizokuwanazo kabla ya ndoa mtavumiliana na kustahimili mapungufu yenu

Kwa ambao tayari wapo kwenye ndoa sijui cha kushauri kiukweli nimejitahidi kufupisha, sijui kama nitaeleweka maana sipo vizuri kwenye uandishi
Have a lovely weekend ahead
 
Ni wachache sana watakaoelewa..

Lakini kwenye ndoa wengi wanaingia kwa kigezo fulani... Wapo wanaoingia sababu ya watoto waliozaa bila kupanga, wapo wanaoingia sababu ya uwezo wa mwanaume na hata wengine kwa shinikizo la wazazi... Hapo ndo huiona ndoa chungu wakati wa misukosuko...

La mno ni kujihakikishia yule ulokonae ndo sahihi kwako, hakuna sababu ya kukurupuka
 
Kingine sio sababu shunie kaolewa na mie niolewe Dada umemaliza
 
Ni wachache sana watakaoelewa..

Lakini kwenye ndoa wengi wanaingia kwa kigezo fulani... Wapo wanaoingia sababu ya watoto waliozaa bila kupanga, wapo wanaoingia sababu ya uwezo wa mwanaume na hata wengine kwa shinikizo la wazazi... Hapo ndo huiona ndoa chungu wakati wa misukosuko...

La mno ni kujihakikishia yule ulokonae ndo sahihi kwako, hakuna sababu ya kukurupuka
Ahsante
 
Back
Top Bottom