Mahusiano ya mtandaoni

Just Nana

JF-Expert Member
Jul 27, 2023
500
1,001
Wasalam wapendwa,

Jana wakati nalala kuna moment ilinijia kichwani, nikajikuta nacheka kwa nguvu sana, miaka kadhaa nyuma nilipata mpenzi kupitia mtandao, ulikua ni Instagram.

Niwe tu muwazi sikua serious na hayo mahusiano ila nilitaka tu kufahamu inakuajekuaje ,mi ni mtu naependa kujaribu vitu kadha wa kadha, wale mama nisipitwe na jambo, ili mradi halidhuru afya, sipendagi kusimuliwa kwakweli.

Basi bhana, katika kupost tupicha twangu kadhaa, kuna mwamba akawa analike karibia kila post, akawa amenifollow pia, offcourse he was totally stranger, never knew him before, we just met on Instagram.

Days go on, urafiki ukakua hadi nisipoingia insta akawa anaacha text DM ,like 'are u good' , alot of halla and so on.

Ikafika point akaomba namba just to check on me kwa time sipo online, na kupata kufahamiana zaidi plus kuweza kuchart watsaap, nikaona sio mbaya nikampa namba baada ya kuangalia picha zake na kufatilia vitu anapost, watu anakua nao na mambo kama hizo.

Basi bhana maukaribu yakaongezeka, kuchekiana kwa sana, mambo yakahamia watsaap sasa, jamaa anakomaa kinoma noma, miamala ikaanza kutumwa (mwanaume akifika hiki kipengele nakuaga nishampitisha kwa asilimia karibia 85), ila kumbuka sijaonana na jamaa na hana papara na hilo.

By that time jamaa alikua anafanya masters hapo chuo UDSM, nami nilikua na mishe zangu za hapa na pale hapa mjini lakini jamaa hakua na papara ya kuonana kabisa, alinambia yupo bize kwaio tuwasiliane tuuuu, kwa sababu miamala ilikua inasoma hakuna kitu ilikua mbaya.

After few good months, jamaa akanambia ana feel like ni muda muafaka wa kuonana, nilipatwa na kiraruraru balaa, ile siku nilipata usingizi kwa taaabu sana, kile kiraruraru ni zaidi ya kusubiria Necta Exams, ni zaidi ya kusubiria interview ya kazi umeisotea sana.

Hatimaye kukakucha bhana, meeting point ilikua mlimani city, alinambia tuonane saa nane mchana, maana ni muislam alitaka aingie masjid then anione, ilikua ijumaa nakumbuka kabisa.

Kwa sababu niliona ni open space nikasema sio mbaya acha nijilipue, nikahakikisha mependeza, sikwenda mbali sana na vile natokelezeaga kwa pic za insta, maana kama alipenda zile picha sidhani kama alihitaji niibuke na baibui, so nikawa tu normal ila hofu kama yote, itakuaje? asiponipenda je? Na vitu kama hizo.

Nisiwachoshe sana , the meeting was successful alhamdulilah, alikua ni mzuri kuliko pic za insta, damn his camera...confidence kama ikakata hivi, nadhani aligundua hilo, akajitahidi kuniweka sawa, na kila kitu ikawa poa.

Itoshe tu kusema he was one of my best lovers, one of the best moments nilipata kwa relationships, kila tukipata wasaa ananikumbushaga 'ulijua unakuja kukutana na mtu wa aina gani mama, ulikua kama umepanick hivi kuniona...'

Hebu tupe nawe experience yako ya kudate mtandaoni, mlifanikiwa kuonana, ilikuaje first meeting, was it fun or disappointing? Bado upo na huyo kiumbe?

Mine was marvellous kwaiyo ni kitu ambayo sijawahi juta kujaribu.

Wasalaaam.
 
Ngoja waje..sie wengine tunakutanaga vituo vya daladala tunakimbiwa
Ukiomba buku tu ya salio limekuishia unashangaa uko blocked

NB:situmii mitandao yoyote wala sijipost na sijawahi hayo mahusiano.ndo nasubiri Jf kama itanibariki haya
Ohhhh , hopefully utapata hata hapa my dear, sasa kwanini unaomba buku la nauli....mi sikuwahi omba hela alijiongezaga tuuu, hata hivyo mi mzito kuomba hela aseeee, unipe darasa
 
Back
Top Bottom