Decibel
Senior Member
- Nov 30, 2019
- 176
- 322
Salam Wakuu!.
Pitia hapa kidogo upate mawili matatu kuhusu hii inaitwa MAELEWANO RAFIKI NA ULIMWENGU (Harmonic relationship).
Kanuni ya msingi ya ulimwengu ni ile ya utaratibu(Order), pale utaratinu unapodumu na kupanuliwa kwa muda inaleta maelewano, maelewano haya na ulimwengu ni kama wimbo mzuri ambao mashairi, mtikisiko na sauti zinachezwa kwa wakati sawia muda wote.
Kila mtu, kila muundo wa uhai hufata maelekezo (notes) kwa sauti hiyo kuu ya Ulimwengu.
Pale maisha yako yanapokua katika utaratibu, malengo yako hutimia, maono yako unayafikia na maono yako hutimia na unakua na maelewano kamili na ulimwengu (Perfect harmonic relationship with Universe).
Maelekezo na mtikisiko ambayo ni maisha yako yanakua na maelewano mazuri na Universe.
Pale unapokua na maelewano mazuri na ulimwengu basi unakua katika njia nzuri kuelekea katika kutimiza lengo na kusudi lako (Mafanikio).
Pale maisha yako yanapokua nje ya utaratibu (Out of Order) yaani unapoishi tofauti na kanuni za ulimwengu (Universal Laws) basi malengo yako hayatimii, wala maono yako huyafikii.
JINSI YA KUJUA KAMA MAISHA YAKO YAPO NJE YA UTARATIBU.
Unajisikia hivi
Muda mwingi huna furaha,
Huna uhakika ni wapi unaelekea katika maisha yako,
Unahofia kuhusu baadae,
Una msongo wa mawazo'
Na muda mwingi huwa una hisia mbaya kwa kila kitu.
JINSI YA KUWEKA MAISHA YAKO KATIKA UTARATIBU
Unajifunza kuhusu kanuni na kujiweka mwenyewe chini ya hizo kanuni/ sheria. Vile unavyojiweka mwenyewe chini ya kanuni ndio unavyozidi kusogea katika mafanikio na kutimiza malengo au ndoto zako.
Jinsi unavyojifunza, kuzifanyia kazi na kujiweka mwenyewe chini ya hizo kanuni basi ndio unavyozidi kusogelea kutimiza malengo yako.
KUMBUKA:
Kanuni za ulimwengu zipo tokea kuumbwa kwa dunia na zipo zinafanya kazi muda wote bila kujali unafahamu au hufahamu, zinafanya kazi na zinaleta matokeo katika maisha yetu bila kujali ni mazuri au mabaya. Uzuri au ubaya wa matokeo inategemea na matumizi yake. Tuishie hapa kwa leo.
Ruksa kurebebishwa na kukosolewa. Karibuni na asante.