Mahusiano na Mali

huskryderz

Member
Dec 23, 2011
27
25
Mdau anaomba ushauri:

Jamaa amewahi kuwa na mwanamke kwa muda wa miaka 10 wakiwa kwenye mahusiano wa kimapenzi, walifanikiwa kuanzisha biashara ikasajiliwa kwa jina la mwanadada ambaye mchumba/mpenzi wake na pia wakajenga nyumba kupitia kipato cha mwanaume na walifanikiwa kuzaa watoto wawili.

Lakini mwanamke ameomba kuachana na mwanaume kwa sababu ambazo mwanamke anadai kuwa anahitaji kuishi maisha yake sasa.

Kumbuka hawa watu hawakuwa wameoana ila mwanaume alipambana kuweza kuinua uchumi akiamini kuwa tayari ni watu wamoja wenye malengo ya kujenga familia yao na baaadae watafika kwenda kwa wazazi kufuata taratibu zingine za ndoa.
 
Aandike kuwa katoa sadaka nguvu yake yote na aanze process ya kutafuta vingine.

Iwe ni fundisho kwake pia kuwa mwanamke haandikishwi jina katika kitu chochote isipokuwa kile ulichodhamiria kumpa kama zawadi.
 
Mdau anaomba ushauri:

Jamaa amewahi kuwa na mwanamke kwa muda wa miaka 10 wakiwa kwenye mahusiano wa kimapenzi, walifanikiwa kuanzisha biashara ikasajiliwa kwa jina la mwanadada ambaye mchumba/mpenzi wake na pia wakajenga nyumba kupitia kipato cha mwanaume na walifanikiwa kuzaa watoto wawili.

Lakini mwanamke ameomba kuachana na mwanaume kwa sababu ambazo mwanamke anadai kuwa anahitaji kuishi maisha yake sasa.

Kumbuka hawa watu hawakuwa wameoana ila mwanaume alipambana kuweza kuinua uchumi akiamini kuwa tayari ni watu wamoja wenye malengo ya kujenga familia yao na baaadae watafika kwenda kwa wazazi kufuata taratibu zingine za ndoa.
Huyo ndugu hana nguvu yoyote kwa huyo binti,na binti kashamjua vya kutosha kashapiga na hesabu za makadirio ya miaka 10 mbele,kashajihakikiahia usalama wake wa kimaisha, rafiki atumie busara kubwa sana juu ya huyo mwanamke ili aibuke mshindi laa sivyo utampoteza

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom