Mahusiano na afya yako 2011

Speaker

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
6,324
2,238
Tunapo ingia tarehe 1.12.2011,...siku ya kwanza kabisa katika mwezi wa mwisho wa
mwaka,....Umeweza kujiuliza mahusiano yako yamekuwa vipi katika mwaka huu wote?

Sio lazima yawe mahusiano ya kimapenzi,hata mahusiano yako na wazazi wako,...
mahusiano yako na wakwe zako,...mahusiano yako na rafiki zako,...mahusiano yako na
majirani zako yamekuwaje?

Kama yamekuwa mazuri unadhani ni kwanini?
Kwa ufupi tu,nadhani kila mmoja ana majibu yake juu ya jinsi gani mahusiano yake
yamekuwa mwaka huu,...lakini kama yamekuwa mabaya na unataka kuyarekebisha ili
yaende vyema,basi asilimia 80% ya matatizo yanaanzia kwako.
CHUKUA HATUA.

La msingi kabisa katika siku hii,tarehe 1st december kila mwaka,inachukuliwa kama siku ya ukimwi duniani.
Umechukua mda wako mwaka huu kupima damu yako ili ujue hali ya afya yako?
Kama ni negative hongera,....lakini unakumbuka kujilinda usiambukizwe virusi vya ukimwi?

Kama ni positive pole sana,sio mwisho wa maisha,namfahamu mtu aliye jitambua ana virusi vya ukimwi
toka mwaka 2001 na mpaka leo ukimuona wala huwezi hisi ni muathirika,...swali kwako,.....
Mwaka huu ume okoa maisha ya watu wangapi kwa kuepuka kuwaambukiza?

Una wafahamisha vipi wengine kuhusu hali hiyo na hali halisi ya ukimwi?
TWENDE TUKAPIME AFYA ZETU.


Hayo yote tisa,lakini kumi ni ndugu zetu wengi wamepata ajali katika mwaka huu,....
wapo walio pungukiwa damu na wakawa wanahitaji kuongezewa,...wapo walio fariki kwa kukosa damu...
hakuna kiwanda kinatengeneza damu ila ni mimi na wewe kujitolea maana hauwezi jua damu unayotoa leo
yaweza kuokoa maisha ya ndugu yako au wewe mwenyewe pale utakapo hitaji,.....
UMETOA DAMU MARA NGAPI MWAKA HUU?

Nimetoa mara mbili,na Ijumaa 2nd december nitatoa kwa mara ya tatu,wewe je?

Iweni na mwisho mwema wa mwaka,....i can't wait to see my family this holiday.
HIV IS REAL,BE FAITHFUL TO GOD,.......
 
mimi nimejitahidi kuongeza ka nyumba kadogo kamoja,si mbaya.Tena nimevuta humu humu mmu,wenzangu vipi 2011 kuna mwingine kapata mzigo kupitia mmu mwaka huu?
 
Kwa wanafunzi niliwahi kuwa n signature=GRADUATE WITH ''A's'' NOT WITH AIDS....
 
Asante kwa ushauri mzuri, na wewe pia usisahu kwenda kupima!


Mara nyingi hua napata majibu yangu baada ya kutoa damu.
Lakini tofauti na kutoa damu mara tatu kwa mwaka huu peke yake,
nimepia mara mbili which makes it a total of 4tyms na kesho itakua mara ya
tano kwa mwaka huu,...wewe je?
 
Toka asubui nahamasisha watu wakapime humu wote wamegoma loh
 
Asante kwa ushauri mzuri,
Nimeshatoa damu mara mbili,na kupima mara mbili,
Na kesho naenda kupima kwa mara ya tatu kwa mwaka huu,
Najua watu wengi wanaogopa kupima,lkn sure ama telling u ukimipa na kujua afya yako kuna raha ya pekee,
Unakuwa full confidence hata inapotokea wakati wa kufanya maauzi ktk mahusiano yani unakuwa na msimamo coz unajijua!!!
 
asante kwa ushauri mzuri,
nimeshatoa damu mara mbili,na kupima mara mbili,
na kesho naenda kupima kwa mara ya tatu kwa mwaka huu,
najua watu wengi wanaogopa kupima,lkn sure ama telling u ukimipa na kujua afya yako kuna raha ya pekee,
unakuwa full confidence hata inapotokea wakati wa kufanya maauzi ktk mahusiano yani unakuwa na msimamo coz unajijua!!!
yaani watu hawajui tu raha ya kupima unakuwa na maamuzi sahihi kabisa kwenye mahusiano
 
yaani watu hawajui tu raha ya kupima unakuwa na maamuzi sahihi kabisa kwenye mahusiano
Asante mamito,
Tatizo tu ni uoga wa kuchukua hatua ya kwenda kupima!
Ukijijua hutakubali mtu akuambukize unakuwa makin zaidi.
 
sasa smile unategemea isingekuwa safi wangeichukua ya nini afterall wanakwambia hapo hapo kama damu yako safi au sio safi and you know what they mean by saying that
sasa toka mwezi wa pili jamani mmmmmmmmmh????????
 
Sasa Smile unategemea isingekuwa safi wangeichukua ya nini afterall wanakwambia hapo hapo kama damu yako safi au sio safi and you know what they mean by saying that
Unapewa ushauri nasaha kabla ya kutoa?
Maana hawawezi kukwambia damu yako si safi kama hujapenda wewe mwenyewe!
 
Back
Top Bottom