Mahusiano Barabarani. .....

Mahusiano Barabarani. .....

Habari za mchana,

Nimekuwa na shughuli nyingi kipindi hiki cha kufunga mahesabu ya mwaka kiasi kwamba nakosa muda wa kujiachia kinaga ubaga nikiwa humu, Yaani naingia kwa kuibia kisha narudi kazini.

Kilichonisukuma kuja hapa leo pamoja na kubanwa na kazi ni tukio nililokutana nalo leo. Asubuhi wakati nakuja kazini niko mwenyewe kwenye usafiri na nimefungulia mziki sauti ya kati, mziki unaoimba naupenda vilivyo hivo nikifika eneo la mataa au kwenye foleni basi najikuta aidha napiga makofi au nachezesha mwili kana kwamba nacheza huo mziki husika.

Nikiwa naendelea hivo huku nasuuzika na kutoiona safari ndefu na akili yangu inakuwa imejaa furaha hata nikikutana na stress kazini haziniumizi sana.

Nilifika kwenye moja ya viungia barabara kulikuwa na mataa ya kuongozea magari, ilikuwa sehemu ya kupita magari matata kwa wakati mmoja wote tumesimama tunasubiri mataa yawake tu kanyani pedeli na kuondoka.

Kama kawaida mie nikawa na swing na mziki wangu shingo image uza kichwa upande wa kulia nikaonda ndani ya gari wako watu wawili, mwana mama ndo anaendesha na mwana baba amekaa kiti cha abiria. Wote walikuwa wametizama mbele kama wanasubiria taa iwake waondoke. Nikahisi hawa watakuwa wanandoa, kwanza ni kama wamenuniana, hawaongei hata kidogo na huwa inasemekana ukiona kwenye gari mwanamke na mwanaume kika mmoja anaangalia upande wake au hawaongeleshani au wamenuniana basi hao ni wanandoa. Hasa baba ndo alikuwa sirias kwelikweli....

Nikasema ukute huyu baba hiyo gari ni ya mkewe, yaani mke ndo kakopa kununua gari... ukute mwanaume alikuwa na pesa na magari mwanzoni ila hakulaza mkewe aguse magari yake baadae mwanaume amefilisika mke bado anakipato walau anampa lifti mumewe ila ndo hawaongeleshani. Nikajikuta nawazaa baadae nikajiweka aaaghh hainihusu nikachukua mbele bado taa inawaka nyekundu nikaendelea kuimba na kucheza mziki wangu.

Shingo na kiherehere inanigeuza kichwa upande wa kushoto hapo nikakuta kuna gari inasubiri kukata upande wa kushoto muda wote mie nacheza huku napiga makofi na kuimba wakati huo huo nawaza alikuwa akinitizama. Nikipogeuka kumtazama tukakutana uso kwa uso, tukajikuta wote tume tabasamu huyu kaka nae alikuwa mwenyewe kwenye gari.

Haikuchukua hata sekunde tatu taa zikaruhusu kuondoka. Sasa mie nikajikuta nacheka zaidi maana yeye kumbe muda wote ananitizama ni kama anasema eeh wee dada unapenda kuimba na kucheza.....

Baada ya pale akili ikaniambia. .....

Kasie kwanini watu wakiwa kwenye mahusiano wanalala chumba na kitanda kimoja wakitoka nje wanaonekana wazi hakuna mawasiliano au mahusiano mazuri?

Mie niko singo na huwa nakuwa na stress zangu lakini hata nikinuniana na mtu kwenye gari nakuwa nakula mziki happy day, happy Kasie.

Yule mkaka nahisi atakuwa kaoa ila kwakuwa hakuwa na mkewe kwenye gari pengine akaweza kutabasamu hata kama aligombana na mkewe nyumbani. Ila kama angekuwa na mkewe kwanza asingeweza kunichekea siajabu nae angekuwa amenuna.

Hivi kwanini wenye mahusiano ya ndoa huwa wananuniana kwenye gari? Mie hata kama usafiri ndo huo mmoja bora nipande zangu daladala kuliko kwenda njia nzima kimyaa, kwanza nnavopenda kuimba ningekuwa na mume angesema nampigia kelele.

Pia najiuliza kwanini ni rahisi sana kwangu kuwa na mahusiano mapya barabarani. .... siku hizi nimeacha tuu kuyaripoti ila yako mengii.

Kama mmoja wiki iliyopita alinipita kwa speeds akiwa anaendesha mark X halafu nikaja kumkera mbele kasimama amewasha taa za hazard. Akanisimamisha kuomba msaada nikasimama akanifata na kuelezea shida yake.... nikamjibu kiutani mbio zote zile kumbe unakwama mbele tu kachoka wote, hadi leo hii tu marafiki.

Huyo ndo Kasie na mahusiano barabarani, narudi kazini sasa baadae.

Kasie Matata Mahaba.
Umejua kunichota Kasie una undugu na mwanafasihi mahiri nini maana umeweza kuipamba hadithi yenye tukio maalum lakn imeshen lugha tam.
Hongera sana inasisimua sana story yko.[emoji8][emoji39]
 
You have a point Kasinde.Kumbukumbu zangu zinanituma kuwa siku ambazo hatuongei na wife kwenye gari huwa tunakuwa tumetibuana,au nakuwa nina mambo yangu kichwani nawaza.Ni mara chache.Mimi sinaga marafiki wengi hivyo mke wangu ndio rafiki yangu mkuu.Ni muongeaji.Si rahisi kunyamaza ukiwa naye.
 
Kumbe ndo wewe eeh
 
Kumbe ndo wewe eeh

Hahahahaa wewe ni yupi? Yule uliyekuwa peke yako upande wa kushoto kisha tukachekeana au yule mliyenuniana na mwenzi wako?

Ndo mie huyo Kasie Matata.
 
You have a point Kasinde.Kumbukumbu zangu zinanituma kuwa siku ambazo hatuongei na wife kwenye gari huwa tunakuwa tumetibuana,au nakuwa nina mambo yangu kichwani nawaza.Ni mara chache.Mimi sinaga marafiki wengi hivyo mke wangu ndio rafiki yangu mkuu.Ni muongeaji.Si rahisi kunyamaza ukiwa naye.

Hata sielewagi kwanini huwa inakuwa hivo. Maana hata mtu na mchepuko wake, wakigombana huko kwenye gari mmoja atambembeleza mwenzie tena kwa mahaba ili wakifika waagane kwa mabusu motomoto.

Wenye ndoa sasa.... mauno wiki kwenye gari hakuna kucheka wala kuongea hata kujambiana sijui kama wanajambiana maana baada ya hapo mnaweza Angus kicheko na story zikaanzia hapo.
 
Umejua kunichota Kasie una undugu na mwanafasihi mahiri nini maana umeweza kuipamba hadithi yenye tukio maalum lakn imeshen lugha tam.
Hongera sana inasisimua sana story yko.[emoji8][emoji39]

Aiseeh hata sijui mtu yeyote mwenye ujuzi wa kuandika kwa fasihi andishi au simulizi.

Asantii.
 
Basi inabid tufundshane huu ujuz ili niwe sehm ya wasimulizi hodar, najua hapo utajiuliza itakuwkuw vp xaxa?[emoji23][emoji23]
 
Mimi mwenyew mkew wangu kanuna
ana ujauzito nampigiaga simu kumsabahi
jana mchana nikampigia kujua maendeleo yake
Nyanya Mbichi: kamuuliza umekula
Wife:Sijala
Nyanya Mbichi:kwa nini?
Wife:Sina chakula
Nyanya Mbichi :kivipi?
Nyanya Mbichi:si unajua hali ulionayo hutakiwi kukaa muda mrefu na njaa
Wife: Sina mtu wa kumtuma mjini!
Nyanya mbichi:Yaishe
saa tatu nikamtumia sms ya usiku mwema hakujibu

Asubuhi nikamtext Kazi njema akajibu

mchana nikampotezea
usiku nimekausha nae kakausha

anapenda sana kununa nuna
sijuwi nifanyaje?
 
Back
Top Bottom