TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Amani iwe kwenu wapendwa na hongereni kwa siku hii muhimu kabisa duniani.
Kiserikali leo ni siku ya Wafanyakazi duniani ambapo kitaifa kilele cha siku hii kinaadhimishwa Makao Makuu ya nchi yetu, Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli ndiye mgeni rasmi.
Katika imani ninayoiamini mimi(Kikanisa), leo ni sikukuu ya YOSEFU MFANYAKAZI(wale wenye imani moja na mimi wananielewa).
Mahubiri ya Paroko wangu kwa muda wote yalihusi siku hii ya Wafanyakazi. Mahubiri yake yamenigusa sana na hivi ndovyo yalivyokuwa:
"Miaka ya 1800 na mwanzoni mwa miaka ya 1900 yalitokea Mapinduzi makubwa ya kiuchumi katika bara la Ulaya na kidogo katika bara la Amerika. Kazi ambazo zilifanywa na watu zilifanywa na mashine. Mashamba makubwa ambayo yalilimwa na binadamu yalianza kulimwa na Matrekta, Gari ambalo lilihitaji watu wengi ili kuunganisha vipuri ili likamilike, kazi hiyo ilianza kufanywa na Maroboti. Matokeo ya Matumizi ya Mashine katika kazi zilizofanywa na binadamu yakawa ni wafanyakazi kupunguzwa kazi. Huu ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuundwa kwa makundi ya kutetea Wafanyakazi ili kupata haki zao. Kazi ikaonekana kuwa ni matezo, shuruba na ndiyo maana leo mtu akitoka kazini anaambiwa "POLE KWA KAZI SAWA NA POLE KWA MSIBA KWA ALIYEFIWA, BADALA YA HONGERA KWA KAZI" Kazi imekuwa sawa na msiba.
Katika kutetea haki za Wafanyakazi, DINI nazo hazikubaki nyuma, zikaandika juu ya kazi, umuhimu wa kufanyakazi kazi kwa ajili ya USTAWI WA JAMII na UKOMBOZI wa MWANADAMU na siyo kwa maslahi binafsi.
Wiki hii Magazeti yameandika sana juu ya MFANYAKAZI KUKATAA MSHAHARA WA MIL. 18 KWA MWEZI KWAMBA NI MDOGO. Msiba mkubw a kwa Taifa mtu kukataa mshahara wa mil.18 wakati huo watoto wa kule MASIKE-MARA wakisoma wakiwa wamekalia mawe, watoto wa kule KAMACHUMU-KAGERA wakikalia Mawe, watoto wa kule MAMAISARA-MANYARA wakikalia mawe, watoto wa kule LIZABONI-SONGEA wakikalia mawe, Wagonjwa kule Mwananyama wakikosa madawa n.k. hakika huu ni msiba wa Taifa. KAZI IMEBADILIKA KUWA NI KWA MASLAHI BINAFSI NA SIYO KWA USTAWI WA JAMII NA UKOMBOZI WA MWANADAMU
NDUGU zangu waumini nawaachia changamoto siku hii mnapoadhimisha sikukuu hii ya YOSEFU MFANYAKAZI mjitafakari ili mwende mfanye kazi kwa Ustawi wa jamii na siyo kwa maslahi binafsi"
Kwa kifupi hayo ndiyo yalikuwa mahubiri ya leo.