Mahubiri Archelais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahubiri Archelais

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andrew Nyerere, Jun 24, 2010.

 1. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #1
  Jun 24, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  HTML{height:100%;cursor:text;} BODY{padding:3px;border:0px;margin:0px;} .PlainText,.HTML{font-family:'Lucida Console' !important; font-size: 80%;} P{margin:0em !important;padding:0em !important;} BLOCKQUOTE,UL,OL{margin-top:0em !important;margin-bottom: 0em !important;padding-top:0em !important;padding-bottom:0em !important;} *{text-indent:0in !important;} SPAN.squiggly{border-bottom:dotted 1px #f00} Nusu ya kwanza ya August,hili kundi la mitume lilikweka makao yake makuu katika miji ya Kigiriki ya Archelais na Phasaelis.ambapo walipata uzoefu kwa mara ya kwanza ya kuwahubiria watu ambao,karibu wote siyo Wayahudi-Wagiriki,Warumi,na Wasiria-kwa sababu Wayahudi wachache waliishi katika hii miji miwili ya Kigiriki.Katika kukutana na hawa raia wa Kirumi,mitume walikutana matatizo mapya katika kuueneza ujumbe,na vipingamizi vipya kwa mafundisho ya Yesu. Katika moja ya mijadala ya jioni na mitume wake, Yesu alisikiliza kwa makini kuhusu hivi vipingamizi kwa injili ya ufalme wakati wale kumi na mbili walipoongea kuhusu uzoefu wao na watu waliokuwa na kazi nao.

  Swali lililoulizwa na Philip lilikuwa mfano wa matatizo yao. Alisema Philip,''Mwalimu,hawa Wagiriki na Warumi wanaupuuzia ujumbe wetu. Wanasema kwamba mafundisho kama haya yanawafaa tu wanyonge na watumwa. Wanasisitiza kwamba dini ya wapagani ni bora kuliko mafundisho yetu kwa sababu inawashajiisha watu wawe na nguvu,gangari,na wenye nafsi ya kushambulia[aggressive character]. Wanasema kwamba wana uhakika kwamba wewe unataka kuwabadili watu wawe jamii legelege ambayo haipingi kitu chochote, ambayo baada ya muda itatoweka duniani. Wanakupenda,Mwalimu,na wanakiri wazi kwamba mafundisho yako ni ya kimbinguni na yanafaa kabisa,lakini wanataupuuzia. Wanasisitiza kwamba dini yako siyo ya dunia hii,kwamba watu hawawezi kuishi unavyofundisha. Na sasa ,Mwalimu,tuwaambie nini hawa watu?''

  Baada ya Yesu kusikiliza vipingamizi kama hivi kwa injili ya ufalme vikitolewa na Thomas,Nathaniel,Simon Zelotes na Mathew,aliwaambia wale kumi na mbili;

  ''Nimekuja katika dunia hii kufanya utashi wa Baba yangu na kufunua nafsi yake ya upendo kwa watu wote. Hiyo,ndugu zangu,ndio kazi yangu. Na hili jambo moja nitalifanya ,bila kujali kueleweka vibaya kwa mafundisho yangu na Wayahudi au wale ambao sio Wayahudi wa kizazi hiki au kizazi kingine. Lakini usisahau kwamba hata upendo wa kitakatifu unao nidhamu zake. Upendo wa baba wakati mwingine unamlazimu kuyazuia matendo yasiyokuwa na hekima ya mtoto wake anayofanya bila kufikiri. Mtoto haelewi wakati wote nia ya upendo na hekima ya nidhamu ya kuzuia ya baba yake. Lakini nakueleza kwamba Baba yangu wa Paradiso anaitawala mbingu ya mbingu[universe of universes] kwa nguvu ya upendo wake. Upendo ndio kitu kikubwa kuliko vyote katika vitu vya kiroho. Ukweli ni ufunuo unaoweka huru,lakini upendo ndio mahusiano ya juu kuliko yote. Na hata kama hawa watu wenzenu wakifanya makosa gani katika jinsi wanavyoiongoza dunia leo,katika siku zijazo hii injili ninayowaeleza itaitawala hii dunia. Lengo la mwisho la maendeleo ya binadamu ni kutambua kwa heshima ubaba wa Mungu na kuanzisha kwa upendo udugu wa watu.

  ''Lakini nani amekuambia kwamba injili yangu imelengwa kwa wanyonge?Je,ninyi mitume wangu mnafanana na wanyonge? Yohana alikuwa mnyonge? Mnaniona mimi kama nimetawaliwa na woga? Kweli,watu maskini wanaokandamizwa wanahubiriwa. Dini za dunia hii zimewasahau maskini,lakini Baba yangu hachagui watu. Isitoshe,maskini wa dunia hii ndio wa kwanza kuitii injili ya toba na mapokeo ya kuwa wana. Injili ya huu ufalme inapaswa kuhuburiwa kwa watu wote-walio Wayahudi na ambao sio Wayahudi,Wagiriki na Warumi,tajiri na maskini,walio huru na ambao hawako huru na pia kwa usawa kwa vijana na wazee,wanaume na wanawake.

  ''Kwa vile Baba yangu ni Mungu wa upendo na huruma na anapendezwa na tabia ya huruma,usiwe na mawazo kwamba utumishi katika huu ufalme ni wa kupumzika na kupiga miayo. Safari ya kupanda kwenda Paradiso ni safari ya kusisimua wakati wote,kuyafikia maisha ya milele kwa vitendo vya ukakamavu. Utumishi wa ufalme duniani utakuhitaji uwe na ushujaa wa kiume kwa kadiri ya uwezo wako wote. Wengi wenu mtauawa kwa uaminifu wenu kwa injili ya huu ufalme. Ni rahisi kufa vitani wakati ujasiri wako unaimarishwa na kuwepo kwa makomredi wapiganaji wenzako,lakini inahitaji ushujaa wa juu zaidi wa kibinadamu na kujitolea kwa shwari na peke yako kuyaweka chini maisha yako kwa upendo wa ukweli ambao uko moyoni mwako.

  ''Leo,wasioamini wanaweza kuwatania kwamba mnafundisha injili ili watu waishi bila kupinga chochote,waishi bila ugomvi,lakini ninyi ni watu wa kwanza ambao mnajitolea ,mlolongo mrefu utafuatia wa waumini wa dhati wa injili hii ambao wataishangaza dunia kwa uaminifu wao kwa haya mafundisho. Hakuna majeshi yoyote ya dunia yamewahi kuonyesha ujasiri na ushupavu kuliko ambavyo utaonyeshwa na ninyi na wale watakaowafuata kwa uaminifu ambao watakwenda kwa dunia yote kuelezea habari njema ya ubaba wa Mungu na undugu wa watu. Ushujaa wa mwili ni aina ya chini kabisa ya ushujaa. Ushujaa wa akili ni ushujaa wa juu zaidi wa kibinadamu,lakini ushujaa wa juu zaidi ni kuwa mwaminifu bila kulegeza msimamo kwa kweli za roho. Na ushujaa wa nama hiyo ndio ushujaa wa mtu anayemjua Mungu. Ninyi wote mnamjua Mungu,ninyi kwa kweli ni maswahiba wa Mwana wa Mtu.''
   
Loading...