Mahojiano ya Msigwa na Lema KTN: Serikali iongeze msisitizo kwenye somo la Kiingereza

Kwa miaka yote zaidi ya nusu karne na mapropesa wao wametufanya "the wretched of the earth"
 
Mods mmetumia weledi sana kubadili tittle ya thread, ilikaa kinafki flani hivi
 
Sikutaka kusoma wala kusikiliza saana ila langu ni lipi? ni hili:
WABONGO cc bado sanaa KWANIN tuwacheke kwakuwa hawakijui kingereza WAKATI sio lugha yetu!!! PEDRO alishindwa kuongea kingereza hvy CESC akamsaidia, PEP mpak kamtumia ARTETA km kocha msaidiz. Sasa cc nan wakujifanya kuponda ponda badala ya kuwapongeza
 
Mada zinazotawala sasaivi kwenye mitandao ya kijamii ni namna gan wabunge wawili tajwa halo juu waliovyoongea kiingereza Chao wakati wa mahojiano nchini Kenya. Wengi wakidai kua lugha hiyo ya malkia (yai)haikutendewa haki na wabunge baada ya kuoneka baada ya maneno yanatumika mara nyingi mfano actually.

Labda tukumbushane wadau kutojua kiingereza KWA mtanzania sio uzembe hii imetokana na sera zetu za elimu.
Wakati tunapata uhuru inchi za Africa miaka ya 1960s Kenya waliekeza zaid kwenye elimu ya awali na msingi kwa kiingereza.

Wakati sisi tz mkazo tuliweka kwenye elimu ya watu wazima ( UPE) tukiamini tunapata watalaam mapema waliokomaa kuliko kusubir watoto wa nursery wakue.

NB. Tuache kuangaika na vitu vidogovidogo ambavyo vinatuamisha kwenye mambo mazito. Tunaacha kuangaika na mgonjwa tunaangaika na LUGHA za kigeni. Pia viongozi lazima wajifunze kutumia lugha walioizoea badala ya kuvamia lugha ambayo hawaijui vizuri.
Sasa muda wote kujadili habari za mgonjwa kuna tofauti gani na kujadili waliyokosea kuongea kiingereza?
 
Concern yangu sio lugha bali content. Wametuaibisha kama Taifa. Shadow Foreign Minister ameonyesha kuwa na uelewa mdogo sana wa masuala ya region na mechanisms zilizopo ndani ya EAC kama EACJ etc Pili, kuongelea negatively heads of State wa nchi nyingine wakati hawakuwa subject ya mjadala kunaonyesha uchovu wa kidiplomasia wa Waziri kivuli wa Mambo ya Nje. Lakini kubwa ya yote na haya ni mawazo yangu tu- kuisemea nchi yako negatively kwenye Foreign Media tena ya nchi shindani na ya kwako ni kukosa uzalendo. I can imagine wanayosema kwenye vikao vya ndani na rafiki zao wa nje.
shikamoo yako kiongozi!
 
Hii lugha ni ngumu kwakweli. Hapa sisi wenyewe tunakuwa na uwanja mpana wa kujadili kwakuwa tunatumia kiswahili. Napendekeza huu mjadala uwe kwa lugha waliyotumia hao wabunge ili twende sawa, ama mnaonaje wakuu?
 
Sikutaka kusoma wala kusikiliza saana ila langu ni lipi? ni hili:
WABONGO cc bado sanaa KWANIN tuwacheke kwakuwa hawakijui kingereza WAKATI sio lugha yetu!!! PEDRO alishindwa kuongea kingereza hvy CESC akamsaidia, PEP mpak kamtumia ARTETA km kocha msaidiz. Sasa cc nan wakujifanya kuponda ponda badala ya kuwapongeza
Mmmhh kuhusu PEP Umetupeleka poriiiiiii asee, guardiola anaongeaa vizuri tuuuu English,Spanish, German to mention few
 
Mkuu, je ni kweli kwamba haujaelewa walichokukuwa wana maanisha?

Mtangazaji kuendelea na maswali mengine, kunaonyesha kwamba wameeleweka.

Kingereza ni kimoja ila kuna tofauti ya LAFUDHI na baadhi ya maneno huandikwa tofauti kulingana na sehemu/Nchi. Mfano USA na UK.

Kama kilivyo Kiswahili cha Tanzania, Kenya, Uganda....
Umeeleza vizuri kuwa zipo tofauti za maneno na lafudhi kulingana sehemu,na ndiyo mie nauliza kwani hao wameongea kiingereza gani hadi watu waje kuwajadili humu? Ni tofauti za maneno au lafudhi?
 
Nilimsikia mtaalaam mmoja akiwaambia wanafunzi wanaoenda kusoma nje kuwa moja ya faida za kusoma nje ni kutunisha misuli katika lugha ya kigeni,sasa nineamini.
 
Mahojiano ya Lema na Msigwa ndani ya KTN, nadhani Lema na Msigwa walikuwa wana mambo mengi ya kuiambia dunia lakini ukosefu wa maneno kadhaa ya kiiengereza kumewaficha sana.

Mfano neno dictator uchwara ukiliongea kwa kiingereza linapoteza uzito.

Lema kaongea 'actually' mara 83 kwnye interview ya dk 24.



Tunapotaka kuongelea kiingereza cha Rais inabidi tuangalie kwanza wapi tumekanyaga.

Language sio tatizo,
as long as unaongea points watu wata kuelewa tuu
wapo wale wanao ongea lugha nyingi, wakickia ukali wa points ulizo toa ata fanya kaz ya ku translate to other languages..
LUGHA SIO TATIZO kabisaaaaa... ¿
 
Back
Top Bottom