Mahojiano ya Diamond katika kipindi cha leo tena, amkubali mtoto wa Hamisa kuwa wake

Kukua ni kuishi kwingi na kuishi kwingi ni kuona mengi!!!

Walioona mengi wote wanafahamu kwamba HAKUNA MWANAUME MWENYE FAMILIA ambae eti atakuwa tayari kukubali kupiga mimba nje tena wakati jambo lenyewe likiwa bado bichi!!!

Wote waliokua na kuona mengi wanafahamu kwamba wanaume wengi wamezaa nje ya ndoa zao lakini kwa muda mrefu inabaki siri isiyofahamika na mke/hawara halali wa mpiga mimba!!!

Waliokua na kuona mengi wanafahamu kwamba wanaume huu wakilikoroga wanachofanya ni ku-accept full responsibility na kuendesha mengine kimya kimya! Na ni kutokana na ukweli huu ndio maana watoto wengi wa nje ya ndoa huwa wanaungana na familia ya baba wakati wameshakuwa wakubwa. In most cases, above 10 years!!!

Kwamba huwezi kumkana mwanao naona unapindisha ukweli! Hakuna aliyesema suala la kumkana mtoto hapa kwahiyo usipende kupotosha!!! Hoja ni kwamba, mwanaume aliyepiga meechi za mchangana atafanya siri inayofahamika na yeye, hawara aliyepigwa mimba, ndugu wa hawara, na ndugu wa mume peke yake. Atakayefichwa hapa ni mke na familia yake na lengo kuu ni kutoleta mgogoro wa kifamilia!!

Na hicho ndicho alichofanya Diamond! Alikubali mimba from the beginning, familia yake ilifahamu na familia ya Hamisa alifahamu! Alichofanya yeye ni kujaribu kumficha Zari!!!

Kwavile Diamond ni public figure, kingine alichofanya ni kuificha jamii kwa sababu, kuifahamisha jamii ingekuwa ni sawa na kumfahamisha Zari sekunde hiyo hiyo!!!

Sasa kama yote hayo huyafahamu nashindwaje kukuambia inawezekana hujakua?! Hata wanawake wenyewe endapo tunatoa suala la u-team hapa wote wanaweza kukubaliana na Mond unless mwanamke mwenyewe awe ni aina ya Hamisa! Watakubaliana na Mond kwa sababu, unaweza kuta miongoni mwao tayari wamezaa na mwanaume mwenye familia lakini bado hiyo ni siri ambayo mke hafahamu!!!

Kutokana na hilo, ndipo hatimae utafahamu JF imevamiwa na nani hasa! Mtu kama mimi au wewe!!!!
Ambao hawajapevuka hawaelewi hayo
 
Kwa kiasi fulani nilikuwa nam-admire sana Diamond kimziki na maisha yake na Zari na family. Lakini baada ya tukio hili la ku-cheat nimemdharau. Nafahamu Waislamu wanaruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja, lakini sidhani kama wana afiki tabia ya michepuko.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom