MAHOJIANO: LUSINDE NA CLOUDS FM - khs matusi yake katika uchaguzi mdogo Arumeru Mashariki

Bazazi

JF-Expert Member
Aug 18, 2008
2,806
3,476
Kama mjuavyo, BAZAZI sio mkazi wa eneo moja, ni nyanaume inayozurura tu hivyo ninaomba msamaha iwapo uzi huu nitakuwa naurudia. Tarehe 04/04/2012 Clouds FM ilifanya mahojiano na Mbunge wa Mtere CCM Mhe!? LIVINGSTONE LUSINDE kuhusiana na matusi yake katika huko Meru hasa Leganga. Kilichonivutia ni haya yafuatayo (unaweza kusikiliza mwenyewe: shusha attachment).

1: CDM ni chama makini, hivyo nami ni mtu makini ndio sababu walinichagua kugombea ubunge.
2: Nilipandwa na JAZBA baada ya matusi ya muda mrefu ya CDM .
3: Maneno mengi niliyoyasema sio ya kweli bali ni kashfa tu.
4: Kwa kawaida ngumi ya kurudishia huuma zaidi kuliko iliyoanza.
5: Mimi sitaki kiju-defense.
6:Najutia niliyoyatamka naomba msamaha.
7: Sidhani kama kuna matusi bali vionjo vikali. baadhi ya watu wanapenda vionjo vikali hivyo wakati mwingine lugha kali ni muhimu.
8: Ni BinAdamu wawili tu YESU KRISTO na MTUME MOHAMAD ndio wahakuwa na nyongo, Nilipandwa na jazba tu.
9: Mimi suala la heshima halinisumbui sana, qani ni watu haohao walimuua YESU na kumpiga MOHAMAD.
10: Hakuna chama chochote cha siasa ambacho kina uwezo wa kutatua matatizo yote ya nchi.

Kwa kumalizia Kibonde alimtwanga na Kigongo hiki. Mhe LUSINDE kichaa akikuvua nguo utakaa au utamkimbiza bila nguo. LUSINDE: Nitakaa KIBONDE: aksante sana.(Kwangu hilo lilikuwa tusi kwake naye bila kujua akauvaa MKENGE; kazi qeliqeli).
 

Attachments

  • Mahojiano; Clouds FM na Lusinde.zip
    15.7 MB · Views: 21
Kama mjuavyo, BAZAZI sio mkazi wa eneo moja, ni nyanaume inayozurura tu hivyo ninaomba msamaha iwapo uzi huu nitakuwa naurudia. Tarehe 04/04/2012 Clouds FM ilifanya mahojiano na Mbunge wa Mtere CCM Mhe!? LIVINGSTONE LUSINDE kuhusiana na matusi yake katika huko Meru hasa Leganga. Kilichonivutia ni haya yafuatayo (unaweza kusikiliza mwenyewe: shusha attachment). 1: CDM ni chama makini, hivyo nami ni mtu makini ndio sababu walinichagua kugombea ubunge. 2: Nilipandwa na JAZBA baada ya matusi ya muda mrefu ya CDM . 3: Maneno mengi niliyoyasema sio ya kweli bali ni kashfa tu. 4: Kwa kawaida ngumi ya kurudishia huuma zaidi kuliko iliyoanza. 5: Mimi sitaki kiju-defense. 6:Najutia niliyoyatamka naomba msamaha. 7: Sidhani kama kuna matusi bali vionjo vikali. baadhi ya watu wanapenda vionjo vikali hivyo wakati mwingine lugha kali ni muhimu. 8: Ni BinAdamu wawili tu YESU KRISTO na MTUME MOHAMAD ndio wahakuwa na nyongo, Nilipandwa na jazba tu. 9: Mimi suala la heshima halinisumbui sana, qani ni watu haohao walimuua YESU na kumpiga MOHAMAD. 10: Hakuna chama chochote cha siasa ambacho kina uwezo wa kutatua matatizo yote ya nchi.Kwa kumalizia Kibonde alimtwanga na Kigongo hiki. Mhe LUSINDE kichaa akikuvua nguo utakaa au utamkimbiza bila nguo. LUSINDE: Nitakaa KIBONDE: aksante sana.(Kwangu hilo lilikuwa tusi kwake naye bila kujua akauvaa MKENGE; kazi qeliqeli).

.

bazazi[SUP]*[/SUP] nm ma- [a-/wa-] conman. (Kar)


conman
n tapeli.


* source: Kamusi ya TUKI

.
 
kwa kifupi, na kwa swali alilouliza KIBONDE na kwa majibu ya Lusinde;
Ni dhahiri kabisa kuwa Lusinde alikuwa na ni KICHAA.
 
kwa kifupi, na kwa swali alilouliza KIBONDE na kwa majibu ya Lusinde;
Ni dhahiri kabisa kuwa Lusinde alikuwa na ni KICHAA.

Alikuwa anapayuka na alikosa kumbukumbu (mwendelezo) ya mahojiano kabisa. Swali la Kibonde lilimdhalilisha sana. Lakini ndiyo aina ya wanasiasa wetu hiyo, "unatukana", "unatoa kashfa" kisha bila hofu wala soni unakiri kuwa "uliyosema hayakuwa na ukweli" na watu wanakuacha uondoke na ngozi yako!
 
Lusinde ni kichaa, na alishasema mwenyewe kwahiyo hata wananchi anaowawakilisha walikosea kumchagua
 
.bazazi[SUP]*[/SUP] nm ma- [a-/wa-] conman. (Kar)conman n tapeli.* source: Kamusi ya TUKI.
Sasa DOTWORLD ndio umechangia nini? Naamini kama huna mchango ni bora kusoma na kusepa. Huu pia na aina mojawapo ya uendawazimu kama wa Lusinde. Nani aliyekuomba utafasiri jina langu na pia qanini hujaifafanua na avatar yangu kama wewe ni mjuvi wa mambo. Kua mwanakwetu au endelea kutembelea kwa watoto wenzio FB. JF ni eneo la watu wazima kiakili. Bazazi ni Bazazi
 
Nafikiri ifike wakati wanasiasa watangaze sera na si matusi na pindi wakitoa matusi ama ahadi za uwongo basi wananchi wawanyime kura ndio itakuwa fundisho kwao.
 
1: CCM ni chama makini, hivyo nami ni mtu makini ndio sababu walinichagua kugombea ubunge. ]


Nimeipenda hii kuwa chama chake ni makini na yeye ni makini- Kwa maana nyingine yeye ni kipmo cha watu makini huko sisiem ndiyo maana walimchaugua wakamwaacha tingatinga.. tafakari upate akili... naona haya kama matusi kwa chama chake na wapiga kura wake
 
lusinde alisema,kama viogozi wa chadema ni vichaa wa kulogwa mimi ni kichaa wakuzaliwa kudadadeki!!!akheri viongozi wa cdm vitapona kupitia wataalam wa jadi je chake kitapona kweli?
 
umakini9 wa watoto wa vigogo unapimwa kuanzia lusinde,adam malima..........................na kuendelea.
 
huyo lusinde ni kichaa kabisa na juzi kati nimemsikia kiongozi wake akiyabariki hayo matusi eti Lusinde alijibu mapigo. Kwa ufupi sera ya ccm ni matusi. watakuwa wameishiwa uongo wa kudanganya wananchi.
 
Nafikiri ifike wakati wanasiasa watangaze sera na si matusi na pindi wakitoa matusi ama ahadi za uwongo basi wananchi wawanyime kura ndio itakuwa fundisho kwao.
Haswaaa, ndivyo walivyofanya mashujaa wa Arumeru!
 
Back
Top Bottom