Mahiza: Wenye vyeti vya kughushi sasa kukiona

Mahiza: Wenye vyeti vya kughushi sasa kukiona

Ibrah

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2007
Posts
2,730
Reaction score
536
Tumaini Msowoya, Iringa

SERIKALI imeahidi kushughulikia tatizo la vyeti bandia na shahada hewa ambazo zinazozidi kushika kasi na kupoteza mwelekeo wa taaluma nchini.

Akizungumza katika mahafali ya pili ya Chuo Kikuu cha Ruaha(Ruco) cha mjini Iringa, Naibu Waziri wa Elimu na Mafuno ya Ufundi, Mwantumu Mahiza,alisema tatizo la kughushi vyeti limesababisha kuwepo kwa viongozi wasio na maadili hali inayosababisha kukwama kwa maendeleo ya Taifa.

"Kuna tatizo kubwa la badhi ya watu kutafuta shahada kwenye mitandao wakijitafanya wasomi, serikali haitaendelea kulifumbia macho tatizo hilo kwa sababu ndilo linalotuletea viongozi bomu," alisema.

Awali Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo aliwataka wasomi nchini kufuata maadili ya taaluma zao, ili kuleta ufanisi Katika utendaji wa kazi.

Alisema ikiwa wasomi watafuata maadili ya taaluma zao, wimbi la viongozi wasiofaa watapungua.

WAKATI huohuo, Lauden Mwambona anaripoti kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha elimu Mkwawa(Muce) kwamba serikali imeombwa kuboresha mazingira ya chuo hicho kwa majengo na miundombinu mbalimbali ili kuweze kufikia hadhi kamili ya Chuo Kikuu.

Mwenyekiti wa Baraza ka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
Peter Ngumbuli alisema hayo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye mahafali ya kwanza ya Muce ambapo wahitimu 797 walitunukiwa shahada.
" Chuo ni kipya, hivyo kuna ulazima wa kujengamiundombinu kama vile madarasa, ofisi, maabara, mabweni nyumba za wafanyakazi

Source-Mwananchi, 15 Des.2009

Huyu Mama inaonekana yumo ndani ya Serilaki ya JK lakini hajui msimamo wa Bosi wake. Bosi wake alishatamka na kutoa msimamo kule Geita kwa Chitalilo pale ilipobainika kuwa Mbunge wa Chama chake ameghushi vyeti. JK alisema kelele za Wapamgaji hazimzuii mwenye nyumba kulala usingizi.
Au Bosi wake kabadili msimamo?
 
jamani huo ni usaniii mtupu. sasa hivi karibia baraza zima la mawaziri ni kama "nyoka wa wanne star" hana meno, hana sumu ya kudhuru aliye karibu naye!!!.
if she dares then aanze na mawaziri wanaotuhumiwa!!!
 
jamani jamani haya mambo hayawezekani tangu nimekuja nyumbani hizi story zipo tu kuna jamaa anaitwa msemakweli alitueleza elimu ya waheshimiwa kazaa ndani ya cabinet kuwa hamna kitu wengine tumesikia wameanza kusoma tena huyu mama anatupotezea muda kwani wapo viongozi wengi wanayoysema na kuelekeza hayaendani na elimu zao habari ndio hiyo
 
Back
Top Bottom