Mahitaji gani yanahitajika katika Sekta Binafsi

Orton

Member
Jun 4, 2010
8
0
Na Christine Kilindu (CTI)

Ni lazima sekta binafsi ziwe na miundombinu mizuri ya kiuchumi ambayo itaboresha ufanisi katika kufanya biashara kwa gharama nafuu na pia kusaidia kuchangia ustawi wa uzalishaji mali. Miundombinu hiyo ni pamoja na kuwepo kwa nishati ya umeme ya kuaminika, barabara zinazopitika, pamoja na maji ya kutosha. Aidha, ni muhimu pia kuwepo na sheria thabiti itakayosimamia masuala hayo.

Miundombinu
Tunashukuru kwamba nishati ya umeme, barabara, na maji yahahitaji mpango mkakati wa muda mrefu, uwekezaji mkubwa wa sekta za umma na sekta binafsi zenye dhamira ya dhati ya kutekeleza miradi iliyokusudiwa.
Wito kuhusu uboreshaji wa miundombinu ulianzishwa na CTI na VIBINDO kati kati ya miaka ya 1990, na mnamo mwaka 2002 TCT nayo ilianzishwa kwasababu hakuna biashara inayoweza kuendeshwa bila kuwepo kwa nishati ya umeme ya kuaminika na ya bei nafuu, miundombinu bora ya usafiri na ugavi wa maji ya kutosha. Tunaziomba sekta za umma na sekta binafsi kushiriki katika kuwekeza kwenye uzalishaji wa umeme, maji, na miundombinu ya usafirishaji kwa sababu japokuwa kuna miradi inayoendelea, lakini bado safari yetu ni ndefu, na kasi iliyopo ni ndogo.

Sheria elekezi na Kanuni Madhubuti

Biashara huwa zinakua na kustawi zikiwa zinasimamiwa na kuongozwa na sheria elekezi na kanuni madhubuti. Japokuwa kwa ujumla sababu hii hua haieleweki wala kukubaliwa sana, ni lazima ieleweke kuwa kukosekana kwa usimamiaji wa sheria na kanuni madhubuti kumechangia sana kuwepo kwa tatizo la rusha nchini Tanzania. Kuna mambo mengi mno yanatolewa bure kwa watu wenye ushawishi mkubwa, vigogo kusamehewa (ulinzi) kutokana na sheria ambayo inasimamiwa na watu wakubwa waliopo maofisini, kwa kawaida inawajumuisha wanasiasa na watumishi waandamizi wa utumishi wa umma. Wanasiasa na watumishi wa umma wana nguvu sana katika kukiuka sheria za nchi. Tabia hiyo imeenea sana nchini Tanzania na inachangia sana katika kulipoteza pato la serikali. Mazoea hayo pia husababisha ukosefu wa haki za msingi kwa sababu inalinda wahalifu waliojificha. Siyo tu kwamba rushwa inawagharimu wafanyabiashara bali pia ni mchezo mchafu unaochezwa na kuwanufaisha wale wanaouhusika nao.

Kwa bahati mbaya, rushwa imeenea hadi kwa watumishi wa ngazi za chini za utumishi wa umma. Wafanya biashara wanatembelewa na wakaguzi kutoka mamlaka mbalimbali. Tunaona thamani za kaguzi zinazofanywa na mamlaka mbalimbali ni ndogo kwakuwa mara nyingi hatma ya kaguzi hizo ni kutishiwa kufungiwa biashara isipokuwa pale tu utakapoamua kulipa kitu kidogo. Mara nyingi kaguzi hizi zinakua ndio chanzo cha ulafi kubughudhiwa, na rushwa.


Uboreshaji wa Mfumo


Katika mwaka 2000, CTI iliandaa ripoti juu ya mfumo wa sheria na kanuni ambazo iliainisha sheria na kanuni mbalimbali zinazohusiana na biashara. Baadhi ya sheria na kanuni hizo zilikuwa zinapingana, na hivyo kuwachanganya wale wenye jukumu la kuzifuata au kuzitumia.


Ripoti hiyo ilisaidia kuanzishwa kwa Programu juu ya uimarishaji wa mazingira ya Biashara nchini Tanzania (BEST Programme). Kwakuwa mambo mengi yanahitaji kufanyika, CTI inakusudia kufanya utafiti mwingine kwa msaada wa BEST-AC utakaopendekeza njia bora za kusimamia biashara. Washauri wetu wakuu ni Ghana na Rwanda ambako tutajifunza ni jinsi gani wanazitumia kanuni zao vizuri katika masuala ya biashara. Bila shaka tutapendekeza kupitishwa kwa tathmini juu ya athari za kanuni (RIA) na / au Udhibiti wa guillotine. Hizi ni taratibu ambazo zimekuwa zikitumiwa na nchi nyingine, zikiwemo baadhi ya zile za Afrika Mashariki, ambazo zimekuwa na mafanikio ya kuvutia na kuongeza urahisi wa kufanya biashara. Matokeo ya kuiga mifumo hiyo ni pamoja na uboreshaji uchumi wa nchi hizo.
 
Back
Top Bottom