Selwa
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 573
- 577
Weekend hii nimemsindikiza mshkaji kupeleka barua ya kuomba uchumba kabila flani ivi ni watu wa Ruvuma, tumekula tumekunywa weee manyama na mishkaki binti familia inajielewa na binti mwenyewe matata sana kweli mshkaji kajitutumua hatuachi kumsifia yule mlimbwende. kasoma pia ana kazi nzuri hapa mjini na kagari kake kadogo ana tubiashara vya hapa na pale maduka maboutique in short binti yuko vizuri hana misele wala shobo . Cha kushangaza tumefika kwao mshenga anatuambia mahari ni biblia wazazi na ndugu washasema. Duh nimeshangaaa. huyu binti hawezi akawa na shida?