Sasa uwezo unao, tatizo ni nini?
Punguzeni ubahili. Princess wa Spain aliutoa mji mzima wa Bombay kwa Mfalme wa Uingereza kama mahari, itakuwa milioni nne hata gari hununui!
Mahari siku zote ni ya yule bint anaye olewa, wengi watu hawajui mahari ni kwa sababu ya kumprotect yule mwanamke from suffering abuse.Naomba kuuliza - sasa kwa mfano mimi YATIMA - hizo milioni 4 si inabidi nichukue mwenyewe??? SINA BABA - SINA MAMA - SINA MJOMBA WALA SHANGAZI - SIN BIBI WALA BABU
Sina hata Mama au Baba wa Hiyari - Nimekulia mitaani - nikafanya biashara ndogo ndogo - Mungu akanibariki - ikaukua kidogo - nikajua kununua mitumba - kuvaa - kusuka nywele - na NIMEPENDEZA - jamaa ndio anataka kunioa - MAHARI AMPE NANI?? SI ANIPE MIMI YATIMA AU???????????
Naomba ushauri wenu - Great Thinkers!!!!!:smile-big:
Bei gani is right. Maana unanunua mtumwa.
Kesho keshokutwa ukimtwika mkeo utumwa atakataa?
Halafu ndo wanawake hawahawa wanaodai usawa? Au hawa wengine?
The entire institution of marriage is disillusioned and in a state of collapse, what remains is utapeli na biashara.
Enzi za zamani miji ilikuwa mali ya mtu, ndio hiyo ilikuwa ikitolewa kama mahari. Enzi za siku hizi watu hawamiliki miji mizima lakini matajiri wenye uwezo wao, watoto wao wakiolewa hao wanaume huanzishiwa biashara, kampuni, au kununuliwa nyumba na makorokocho mengine. Tofauti ni kuwa hawaiti mahari bali zawadi.Kwa hiyo bidada maisha yangekuwa hivyo miji yetu yote si ingetolewa mahari pindi wakubwa waoanapo? Huyo Princess wa Spain alikuwa na uchungu gani na Boombay?
Nyie oleweni bure bwana, mnafanya ngono inazidi kuwapo pamoja na kuzalia nyumbani kwa sababu vijana wanaogopa bei zenu hizo....
M4 ndogo kwani we uliolewa/utaolewa kwa shilingi ngapi?
Mi mbona wife alikataa kuolewa kwa mahari japo nililazimisha kutoa?
Vyote vina umuhimu maana vinatumia vyote.kwa maana hiyo bei halisi ya ng'ombe sio muhimu, muhimu uwapelekee ng'ombe wao tu.
Sasa uwezo unao, tatizo ni nini?
Punguzeni ubahili. Princess wa Spain aliutoa mji mzima wa Bombay kwa Mfalme wa Uingereza kama mahari, itakuwa milioni nne hata gari hununui!
Wana Jamii Forum naomba kuwasilisha hapa mbele ya jukwaa hili
Nina mpenzi wangu kamaliza chuo now nataka nioe kabisa!! Tukiwa katika maongezi ya kawaida tu nikamdokezea
Hivi mahari yako ni kiasi gani mchumba wangu kaniambia millioni nne!!Kiukweli na mpenda sana lkn naona hio pesa nyingi japo uwezo wa kuitoa nianao Je Ndio mahari za siku hizi zilivo? Naomba ushauri wenu wana JF
Mwanamme anampa zawadi mwanamke kwa kukubali kuwa wake wa milele, kumzalia watoto na hata kuchukua jina lake wakati mwingi mwengine
Hakuna suala la utumwa hapo, mbona mwanamke anabadili jina na kuwa la mwanamme na hawi mtumwa wake?
Mtoto mnazaa wote na siyo mmoja wenu anamzalia mwenzake. Dhana ya kumzalia mwanaume mtoto inaendeleza yale yale ya mfumo dume.
Watumwa wa Marekani walibadishiwa majina yao na kupewa majina ya wamiliki wao. Binafsi sioni ubaya wa mwanamke aliyeko kwenye ndoa kubakiza jina la ukoo wake.
Mimi nazaa mtoto ila yeye namzalia, hivyo sote kuwa na huyo mtoto wetu kwa pamoja. Kukubali kubeba mbegu zake, tukachanganya vinasaba tukatoa mtoto, tayari mwanamke anafaa kupewa zawadi 😛oa
Ndio hapo nilipokusudia mie, kuwa watumwa walikuwa wakibadilishwa majina ya kuwa ya wamiliki wao lakini wanawake wanaobadilishwa majina kuwa ya waume zao mbona hatuwaoni kuwa watumwa?
Kama hatuwaoni basi na mwanamke kulipiwa mahari hakulazimishi kuwa ndio kanunuliwa na hivyo kuwa mtumwa
Sarufi uwanja mpana. [Kumchekea] haina maana kuwa wewe mwenyewe hucheki, unacheka kwa niaba yake au badala yake. Hivyo hivyo kwa [kumchezea]. Haina maana kuwa wewe huchezi, ni kuwa unacheza na unajichezesha mbele yake. Kwa hiyo kumzalia haina maana kuwa wewe mwenyewe huna chako. Unazaa kwa ajili yako na yake.Bado sikubali kuwa unamzalia. Ni unazaa mtoto wenu. Ukisema unamzalia inakuwa kama vile huyo mtoto si wako bali ni wake peke yake.
Utumwa una sura nyingi. Wanawake kubadilisha majina yao na kuchukua ya waume zao inakaribiana na utumwa.
Kulipiwa mahari ni kuendeleza dhana ya mwanamke kuwa object. Mahari ina objectify wanawake na ina-run counter na juhudi za kuleta usawa na wanaume
Mwalimu Gaijin upoSarufi uwanja mpana. [Kumchekea] haina maana kuwa wewe mwenyewe hucheki, unacheka kwa niaba yake au badala yake. Hivyo hivyo kwa [kumchezea]. Haina maana kuwa wewe huchezi, ni kuwa unacheza na unajichezesha mbele yake. Kwa hiyo kumzalia haina maana kuwa wewe mwenyewe huna chako. Unazaa kwa ajili yako na yake.
Inaweza ikawa si utumwa lakini kuna kupoteza identity. Si jambo linalonipendeza.
Hapa nadhani suala ni unalipa kwa nani? Kama baba wa mtoto na mume mnabadilishana mtoto kwa mahari, inaweza kuwa na mantiki hiyo uliyotaja. Lakini ikiwa ni binti mwenyewe ndie anaepanga mahari, na ndie anaekabidhiwa hicho alichopewa kama tunzo au tunu kutoka kwa mume wake mtarajiwa, sioni ila hapo.
Ni njia moja wapo ya kuonyesha mapenzi tu. Pata picha mwanamke kadai atungiwe shairi, linaletwa linasoma....how romantic is that?! :redfaces:
Tukumbuke kuwa mahari si lazima yawe mali.
Loud and Clear Nyani NgabuBado sikubali kuwa unamzalia. Ni unazaa mtoto wenu. Ukisema unamzalia inakuwa kama vile huyo mtoto si wako bali ni wake peke yake.
Utumwa una sura nyingi. Wanawake kubadilisha majina yao na kuchukua ya waume zao inakaribiana na utumwa.
Kulipiwa mahari ni kuendeleza dhana ya mwanamke kuwa object. Mahari ina objectify wanawake na ina-run counter na juhudi za kuleta usawa na wanaume.
Bit of some slight business issues here and there but all is well happy to see you aroundEbwanaweeee......ulikuwa wapi? Duh